Fursa Bomba la Mafuta kwa watanzania-UPDATES

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
bomba.jpg


Wakuu.
Tanzania na Uganda zimesaini mkataba wa mwisho kuanza ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani bandari ya Tanga nchini Tanzania .

Ni heshima Kubwa nchi yetu ya Tanzania kupata fursa hii ya bomba la mafuta kupita nchini Tanzania ambao utapita mikoa 8, Wilaya 24 na vijiji 184.

Kuna faida nyingi sana kama Taifa tutapata kutokana na uwepo wa mradi huu wa bomba la mafuta.

Wakati wa ujenzi Watanzania wengi watapata fursa ya ajira ambapo jumla ya ajira 40,000 zitapatikana. Ajira za ufundi, ulinzi, upishi, usafiri, fursa za malazi, na huduma za kifedha.

Lakini hali ilivyo inaonesha watanzania wapo kimya sana na wenzeetu uganda wamekwisha changamkia fursa .

Mimi nipo hapa Kagera ambapo kutakuwa na kambi mbili za mwanzo kabisa wakati bomba linajengwa nchini Tanzania kutokea huko Uganda.

taarifa zote za mradi huu zinawekwa katika website kuu (kwa sasa) . ile ya mradi ambayo ni
EACOP – East African Crude Oil Pipe Line lakini waganda wanatumia website mahususi na vyombo vyao kusaidia wananchi wao kupeana tarifa mapema.

Fursa zinatangazwa na zitaendelea kutangazwa lakini ukifuatilia vyombo vya habari vya uganda unaona kabisa kuwa ajira nyingi,tenda zinaweza kutupita kama watanzania maana hatuna tarifa mpya za kila siku juu ya kinachoendelea.



Note:Mimi siyo mfanyakazi wa hiyo kampuni wala mwajiriwa bali najitolea kuwakumbusha watanzania fursa hizi kwa lugha rahisi tu ili vijana wetu na jamii yetu ijue kinachokuwa kinaendelea maana inaonesha sisi tunashindwa vitu vinapowekwa kwenye maandishi. maana hadi sasa kuna fursa nyingi zimekwisha tangazwa kupitia website hiyo na magazeti kongwe ya kila siku.

Napatikana pia twitter..>https://twitter.com/bukobaonline?lang=en


======================

1:Kituo cha kupata taarifa za kila siku.
Kituo kikuu kipo nchini Uganda lakini hapa Tanzania kituo kikuu cha kutoa taarifa kipo Jijijini Dar Es Salaam kupitia hii anuanwi.

Total EAST Africa Midstream B.V,
Msasani Peninsula,
429 Barabara ya Mahando, Kitalu D,
S.L.P 38568,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Simu: +255 22 2214100/4102/4103
Barua pepe : EACOP.info@total.com

2:Ajira ambazo zimetangazwa hadi march 2021
Ajira zilizotangazwa hadi sasa bonyeza hapa.>> AJIRA BOMBA LA MAFUTA


3:Zabuni ambazo zimetangazwa hadi march 2021
Zabuni mbalimbali zilizokwisha tangazwa had sasa Bonyeza hapa==>> ZABUNI BOMBA LA MAFUTA

Rejeo za JF



 
TANGAZO KWA UMMA

Shukrani kwa nia yako ya kutaka kushiriki katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Mradi wa EACOP una sera ya ugavi iliyowazi na inayoelekeza kuwa fursa inatakiwa kutangazwa katika magazeti nchini Tanzania na Uganda na kuwekwa katika ukurasa wa tovuti ya Mradi wa EACOP. Tangazo lolote la Maombi ya Kuonyesha Nia (EOI) linalotangazwa bila kuzingatia hatua hizi linatakiwa kutiliwa mashaka na kutambulika kuwa haliusiki na Mradi.

Ukiona tangazo lolote la Maombi ya Kuonesha Nia katika Mradi wa EACOP linalotia mashaka tafadhali toa taarifa katika kituo chochote cha polisi karibu yako, Mamlaka ya Serikali za Mtaa au katika Mradi wa EACOP. Maombi yote kuonesha nia yanatakiwa kuwasilishwa kwa Mradi kupitia njia zilizotangazwa. Maombi yatakayo wasilishwa kwa njia zisizo rasmi hayatozingatiwa.

Mradi una mchakato wa wazi wa kutoa fursa kwa waonesha nia na unaozingatia uwezo. Washindani wanachaguliwa kwa kuzingatia vigezo na kwa kuzingatia sheria za ajira za nchi husika nchini Tanzania na Uganda. Unashauriwa kuendelea kutembelea ukurasa wa tovuti ya Mradi wa EACOP ili kuweza kupata taarifa za Maombi ya Kuonesha nia kwa wakati.

- Mwisho
Kwa taarifa zaidi au kufanya mahojiano kwa ajili ya vyombo vya habari tafadhali wasiliana nasi kupitia:'

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano,
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki – Tanzania / Uganda Mariagoreth Charles / Stella AMONY
Simu ya ofisi: +255 22 2214100/4102/4103 au +256 (0) 204 916 157
Simu ya mkononi: +255 699 000 341 au +256 794 888 157
Baruapepe : mariagoreth.muangirwa@external.total.com au stella.amony@external.total.com
Tovuti: www.eacop.co.tz au www.eacop.com
 
Asante Boss kwa kutumegea japo fursa tuzifahamu, sisi watanzania wengi hua hatuna muda wa kutafuta mambo kama haya ya maana tunapenda kufuatilia mambo ya muziki
 
Asante Boss kwa kutumegea japo fursa tuzifahamu, sisi watanzania wengi hua hatuna muda wa kutafuta mambo kama haya ya maana tunapenda kufuatilia mambo ya muziki

Tubadilishe vijana wetu mdogo mdogo. hakuna wa kumlaumu bali sisi wenyewe.
 
Kuhusu Fidia kwa litakapopita bomba iko hivi

Watu walioathirika wanajulikana na kusaidiwa kama ipasavyo
Mikataba salama na kila kaya iliyoathirika, kulipa fidia na kuwa na mipango ya kuwawezesha kujipatia tena kipato na kuzisaidia familia kuhama kwenye eneo hilo (kwa wale wanaochagua fidia ya mali kwa ajili ya kuhamisha makazi, kuwasaidia kuhamia kwenye eneo jipya).

chanzo:EACOP – East African Crude Oil Pipe Line
 
Mimi nasubiria zabuni ya kusupply mbao. Sijui kama zinahitajika kwenye hii kazi?
Inawezekana tu. sema watanzania wengi wanafanya biashara kama ya udalali. wengi hawana anuanwi rasmi...vitu kama kampuni au bussines name,TIN au leseni kwa biashara zao. wanapotaka kutoa tenda lazima hivyo vitu vizingatiwe. aidha wengi wetu tunataka mteremko na hizo bidhaa hazitoshelezi na hatutaki kuungana na wenzetu kama uganda.

mfano.
wakitaka mbao mfano ellfu 20 na kuendelea sijui kama wabongo wanaweza..

lakini tujaribu tu
 
tumia computer badala ya simu.. kwangu inafunguka
View attachment 1753821

Zote zinafunguka kasoro ya ujenzi nimetumia laptop bado haifunguki hata hivyo nilichokuwa nakitafuta nimekiona, majina ya kampuni ya yaliomba list ishatoka yapo kwenye tovuti ya EWURA.

Hili tangazo lilitola siku nyingi sana mwaka jana na Kampuni zilifanya Maombi na nimeona kwenye Database ya Ewura
 
Inawezekana tu. sema watanzania wengi wanafanya biashara kama ya udalali. wengi hawana anuanwi rasmi...vitu kama kampuni au bussines name,TIN au leseni kwa biashara zao. wanapotaka kutoa tenda lazima hivyo vitu vizingatiwe. aidha wengi wetu tunataka mteremko na hizo bidhaa hazitoshelezi na hatutaki kuungana na wenzetu kama uganda.

mfano.
wakitaka mbao mfano ellfu 20 na kuendelea sijui kama wabongo wanaweza..

lakini tujaribu tu
Shukrani kwa ushauri, sisi kampuni tunayo na vielelezo vyote vipo. Cha msingi ni kupata updates na connections na mzigo unaoatikana wa kutosha tu.
 
Back
Top Bottom