Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,427
Habari wanaJF,
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu muumba mbingu na nchi kwa kumuwezesha mpenzi wangu kujifungua salama mtoto wa kiume.
Sio siri nimekuwa ni mtu niliyetamalaki furaha sana kila nikimtazama kijana wangu mpya.
Lakini kuna ushauri wa mtoto akafungwe kikamba kinaitwa "Mvuje" wanasema ni lazima afungwe ili kumuepusha na mambo mabaya na asiwe anaweweseka usiku wa manane wala kulia muda wa usiku.
Niliposhirikishwa kuhusu suala hilo nimekataa katakata lakini nimeanza kupewa vitisho kuwa mtoto atapata matatizo. Kwakweli wanaJF, mpaka sasa nimeshikiria msimamo wangu kwakuwa sioni mantiki ya kufunga kikamba hicho. Lakini kila nikiambiwa kuhusu matatizo hayo napata mashaka sana ikizingatiwa ndio mtoto wa kwanza.
Je, kuna ukweli wowote kwamba kijana wangu atapata matatizo asipofunga "Mvuje"
CC: mshana jr