Furaha ya Migogoro ya Serikali

Furaha ya Migogoro ya Serikali

Kutokana na Ndege yetu kuzuiwa na mahakama kuu nchi South Africa, nimepitia mitandao ya kijamii kusoma maoni ya watu ambao ni wananchi na wanufaikaji pengne wa kila miladi inayoihusu Serikali.

Jambo la kusikitisha watanzania wanafurahi kwa kitendo cha ndege yetu kuwekewa kizuizi.

Kabla sijawalaumu nimejiuliza maswali

1. Kwanini wanafurahi serikali inapokuwa kwenye migogoro fulani?

Swali hili limekuja baada ya kujiridhisha kuwa si hili tu la Air Tanzania bali imekuwa ni jambo la kawaida wananchi kufurahi pale nchi (serikali) inapokuwa kwenye migogoro.

2. Je Serikali inajifunza nini kupitia wananchi wake wanapofurahi pale inapokuwa na migogoro ya aina hii?

3.Je kama nchi tunapaswa kufurahi au tuwe na namna nyingne ya kufikisha ujumbe kwa serikali ili kuwajibika inavyopaswa?

4.Je Serikali inajua chanzo pelekewa kwa wananchi kufurahia pindi inapokuwa na migogoro? Kama ndio je haioni kutafta suluhisho la tatizo?

Pamoja na maswali yangu lakini Leo ningependa kujua swali msingi ni Kwanini tunafurahi nchi inapoingia kwenye migogoro?
 
So tatizo ni ushirikishwaji kwa wananchi kama wadau wakubwa wa miladi na maendeleo yao

Ukosefu wa uwazi kwa wananchi

Watu kubanwa pale wanapotoa maoni kuhusu nchi yao (uhuru)

Asante sana Kiongozi

Aswaaaaa, hayo ndiyo majibu. Wananchi wanaipenda sana nchi na rasilimali zao.
 
Uvunjwaji wa katiba

Je kama Mwananchi unaiwajibishaje serikali ambayo umeiweka madarakani
Sasa si serikali inatuua

Tufanyeje sasa

Inatuua wananchi

Inatupiga risasi

Inatusakizia kesi

Haitaki kukosolewa

Inaumiza wananchi wake

Inakiuka katiba

Point ni nyingi sana broh hapo nimekupa chache wenzangu wataendelea
 
Umeongea kwa uchungu sana..,
wananchi wengi hufurahia kwa sababu ya uonevu unaofanywa na watumishi wa serikali. kwa mfano uhamiaji nida polisi rita ardhi tra nk huwezi kupata haki yako hata kama una docment zote lazima usumbuliwe usumbufu huu huwafanya wananchi kuchoka na kukata tamaa ya serikali yao pia ajira hakuna wataajiriwa watoto wa viongozi tu wengine mkafuge samaki mjiajiri. hivi juzi tu imetoka scholaship china serikali imepeleka wanafunzi wengi waameagwa na ndali chako nenda kaangalie waliokwenda scholaship ni wakina nani watoto wanani ambao ndio wengi offisi za serikali hazina mpangilio ya kuhudumia wateja na bahati mbaya umkute mwanamke offisi yoyote utajuta kama hukusumbuliwa. kwahiyo wananchi wamebaki na wao kufurahia serikali inapopata matatizo
 
Hapa nadhani ni ATCL vs Fast Jet!

Tulipozuia ndege yao pale JNIA nadhani walikuwa na wao wanatupigia mahesabu.
 
Hahahahah hilo nalo ni tatizo kufikilia uchawi baadala ya msingi wa tatizo..

Mimi siamini kama ni uchawi, naamini kuna sehemu hapapo sawa, pande zote mbili kwa serikali na wananchi wake ambao ndio wenye serikali
Sijasema uchawi per say, nimeongelea hali ya kuwa na hulka za kichawi, uchawi ni hali ya kutopenda maendeleo ya wengine, hata serikali yako, ni roho mbaya
 
KIBURI CHA VIONGOZI WA AWAMU YA 5 WAFUASI WAO.
waliponunua ndege walitusema Sana wapinzani na wengine wakasema ni Mali ya CCM.
Leo ndege ikamatwe nihuzunike Kwa lipi?
wakati sio Mali yangu ni ya CCM?
Na Mimi na CCM kama chui na paka.
 
Wanaofurahi ni wale vigogo na familia zao waliotumbuliwa, wenye vyeti feki, mafisadi na wana ufipa.
Huko kutumbuliwa kwa wenye vyeti feki kumekusaidia nini endapo Patrol ya Serikali inazidi kupanda kila mwezi?
 
Lakini zile ndege hazijaandikwa CCM wala kupakwa rangi ya kijani

Ninadhani la msingi ni viongozi kuwa viburi na pengne kutukuza uchama zaidi kuliko kuwatumikia wananchi..

Je kuna haja ya kuweka sheria kiongozi akichaguliwa hapaswi kujihusisha na shughuli za chama? Yaani chama kijiendeshe kama taasisi tu baada ya uchaguzi kuisha ili kuweka usawa na uwajibikaji wa viongozi?
KIBURI CHA VIONGOZI WA AWAMU YA 5 WAFUASI WAO.
waliponunua ndege walitusema Sana wapinzani na wengine wakasema ni Mali ya CCM.
Leo ndege ikamatwe nihuzunike Kwa lipi?
wakati sio Mali yangu ni ya CCM?
Na Mimi na CCM kama chui na paka.
 
Mi katika yote magu nimempendea kutumbua vyeti feki, ila kasoro kawapendelea majeshini.
Mishahara ya waliotumbuliwa inaenda wapi, mbona payroll ya Serikali haijawahi kushuka?
 
Kama tunadhulimiwa tuna haki ya kufurahi dhulmati anapofikwa na majanga
 
Hayo unayajua wewe.ila wenzio hawajui
Lakini zile ndege hazijaandikwa CCM wala kupakwa rangi ya kijani

Ninadhani la msingi ni viongozi kuwa viburi na pengne kutukuza uchama zaidi kuliko kuwatumikia wananchi..

Je kuna haja ya kuweka sheria kiongozi akichaguliwa hapaswi kujihusisha na shughuli za chama? Yaani chama kijiendeshe kama taasisi tu baada ya uchaguzi kuisha ili kuweka usawa na uwajibikaji wa viongozi?
 
Nikusahihishe sio wananchi, sema wanamitandao, hiki tunachoongea haps jaribu kumpigia simu ndugu yako kule kijijini mlize kuhusu ndege kukamatwa atakushangaa. Ujinga tulio nap sisi wanamtandao hatujui watanzania wako wapi.
Nikirudi kwenye mada yako, uwezi kuisemea vizuri serikali kama ulikuwa una makandokando au mnufaika Wa makandokando kisha serikali ikakata mirija au ukafukuzwa. Chunguza vizuri wote wale wanaotukana na kuisema ovyo mitandaoni ni wahanga. Watataka wawe na hati miliki ya Tanzania, rais anavyo fanya mageuzi ya kimfumo kuziba mianya ya upigaji roho zinawauma, hakuna linguine zaidi ya kuwa mijitu yenye roho mbaya wanataka watanzania walipe ada za shule za milioni walipe private hospital wakati hawana uwakika Wa milo mitatu. Watatukana sana ila wameshikwa korodani na koleo.
 
Duh, Dada umetumia nguvu nyingi sana kuandika huu upupu.
Kikubwa muda ukifika tutaongea lugha moja.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom