Furaha ya maisha ni kitu muhimu sana, tajiri kaamua kufungua duka la matunda na kushinda huko

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Huyu ni tajiri mwenye nyumba nyingi za kupanga.

Siku moja nikiwa barabarani, niliona duka la matunda lenye mazingira safi likiwa na viti na meza kwa ajili ya wateja.

Nilipofika pale, nilimkuta tajiri huyu akiwa na mazungumzo yaliyoonekana kuwa yamenoga sana. Nilidhani ni mteja, nikaenda kumsalimu. Akainuka, tukajuliana hali, na aliniambia kwamba duka hilo ni lake. Alinikabidhi machungwa matatu, na nilijaribu kumlipa, lakini alisisitiza nisiwe na wasiwasi, kwani ilikuwa ni mara yangu ya kwanza.

Nilichogundua ni kwamba, duka hili halikuwa sehemu ya biashara ya kawaida. Ni mahali pa kupumzika, kushinda, na kukutana na watu kwa mazungumzo, kwani hata eneo analoishi mitaa imejaa utulivu.

Najua humu ndani watu wengi ni introverts watashangaa

Mtu ana uhakika wa pesa, mitaa anayoishi imetulia sana, hizi ni mbinu za kuchangamana na watu, huko kwake kumepoa sana, fuatilieni hata watoto waliofanikiwa wanapotaka kuwaleta wazazi seheu zenye mazingira tulivu, wazazi huwa wanaboreka haraka na kutaka kurudi huko kunakoonekana kuna kelele.
 
Masharti ya mganga
 
Nilichogundua ni kwamba, duka hili halikuwa sehemu ya biashara ya kawaida. Ni mahali pa kupumzika, kushinda, na kukutana na watu kwa mazungumzo, kwani hata eneo analoishi mitaa imejaa utulivu.
Uingereza?
 
Code ngumu sana hii
 
Hata huku kwetu yupo tajir wa hvyo,kwanza duka lake ni kama ofis kwa ajili ya kukutana nae pia ni kama kijiwe cha kukutana na rafik zake na wafanyakaz wake ambao zinaiva

Anauza vitu kama maji na pombe na mahitaji ya nyumban,dukan kwake kuna viti kabisa kwa ajili ya washikaj na wanaomuhitaj
 
Sisi waTanzania tumeathiriwa sana mambo ya kichawi kiasi kwamba mtu akiona jambo geni kwenye fikra zake badala ya kulichanganua na kunoa bongo yeye anarahisisha kwa kusema tu uchawi.....

Huo ni mkwamo wa fikra na udumavu wa ubongo.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…