Funzo kwa wanachama wa SACCOS wote

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
SACCOS yadaiwa kufilisika na pesa za wanachama

SACCOS moja mjini Makambako mkoani Njombe yadaiwa kushindwa kutoa pesa kwa wanachama wake hali iliyozua taharuki na kuzusha madai ya taasisi hiyo kuwa huenda imefilisika.

makambako.jpg

BAADHI ya wakazi na vikundi vya wajasiriamali mji mdogo wa Makambako wamelalamikia kutopata pesa zao walizo ziweka kama akiba katika Saccos ya Makambako na kuomba mrajisi wa ushirika kuchunguza kama pesa zao zipo na kama hazipo kutaifisha mali za Saccos ili kurejeshewa pesa zao.

Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya wananchi waliojiwekea pesa zao katika Saccos hiyo kwa nyakati tofauti mjini Makambako wamesema kuwa wameshindwa kulipa ada za watoto wao kutokana na Saccos hiyo kutokuwa na fedha na kila wanapokwenda kuambiwa wasubiri ama kuambiwa warudi siku nyingine na mara nyingine kupewa pesa kidogo kidogo.

Wamesema kuwa wanamuomba mrajisi wa vyama vya ushirika kufika katika Saccos hiyo ili kuzinusuru pesa zao na kuwa waliamini kujiwekea akiba katika Saccos hiyo lakini inavyowafanyia wanahisi imefirisika.

Baadhi ya wanachama walioeleza masikitiko yao ni Fatuma Sharima mamalishe, Claud Mwinuka Mwanakikundi, Aldofu Msiliga, Mwanachama, Prisca Amri.

Baada ya kufika katika ofisi ya Saccos hiyo meneja wake amedai kuwa yeye sio msemaji na kusema kuwa mwenyekiti wa bodi ndiyo msemaji wa Saccos hiyo lakini hakuwepo na alikuwa nje ya ofisi huku akikili kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuwapa walio weka akiba.

Naye afisa ushirika wa halmashauri ya mji Makambako aliondoka ofisini kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari na baada ya kupigiwa simu yake haikupatikana licha ya mweyekiti wa halmashauri kukiri kuwepo kwa suala hilo.

makambako%20saccos1_0.JPG

makambako%20saccos.JPG



Chanzo: SACCOS yadaiwa kufilisika na pesa za wanachama | East Africa Television
 
SACCOS ni Mali ya wanachama wenyewe. Wanaochagua viongozi( bodi ya uongozi),huajiri watumishi yenyewe kwa kupitia bodi iliyochaguliwa na wanachama. Huchagua kamati ya usimamizi yenye jukumu la kusimamia mwenendo wa uendeshaji wake na kulinda mali za chama chao. Inapotokea kasoro yeyote wenye Mali( wanachama) wanapaswa kujua na kuchukua hatua. Mrajis ni mfuatiliaji wa mwenendo wa uzingatiaji wa Sheria,kanuni na taratibu. Anawajibu pia wa kusaidia kuchukua hatua. Ni vizuri tunapowekeza tufuatilie mwenendo wa tulio wakabidhi mali zetu.
 
SACCOS ziko Kenya, kule ukienda utakutana na SACCOS zinamitaji mikubwa kuliko hata baadhi ya benki za huku Bongo, Na kenya ndo nchi yenye SACCOS nyingi
 
Kenya walijifunza kwetu wakatenda tulichowafundisha. Sisi tunatenda tusichosema na tunasema tusichotenda. Siyo SACCOS tu, fuatilia Maprofesa wa kilimo na mifugo SUA,wanachofundisha sicho wanachofanya. Wanewkekeza sana( japo siyo wote) kwenye Baa na nyumba za kulala na siyo ktk kilimo na Ufugaji. SACCOS nzuri au mbaya chanzo chake ni sisi wamiliki. Tunataka mtu mwingine au serikali itengeneze nzuri ndipo sisi tufaidi. Ni mawili ama tunapenda kudeka au hatujui SACCOS ni nini na nani ni mmliki wake.
 
SACCOS ziko Kenya, kule ukienda utakutana na SACCOS zinamitaji mikubwa kuliko hata baadhi ya benki za huku Bongo, Na kenya ndo nchi yenye SACCOS nyingi
Mkuu kwani Kenya ina uhusiano gani na hofu ya kufilisika kwa SACCOS?
 
Back
Top Bottom