mathematics
JF-Expert Member
- Feb 21, 2012
- 3,324
- 1,116
umefunika chakula vizuri kabisaa, hakuna nafasi ya kuingia mdudu yeyote, ila bahati mbaya ukasahau kukiweka kwenye friji. siku kadhaa zinapita unafunua chakula unakuta kimeharibika na funza tele wamejaa, wametokea wapi hawa funza?
nyama ipo ndani ya mfuko au chombo bahati mbaya imeoza unakuta funza kibao, tena wakubwa, wanatokea wapi hawa funza??!!
hawa funza huwa wanatokea wapi? ninajiuliza mara nyingi sijawah pata majibu!!
Kuna mamilioni ya bacteria wanaotuzunguka ambao hawaonekani kwa macho ndio huleta haya yote na si kwenye vyakula tuu bali hata mwili hasa sehemu zako za siri na mdomoni
Kuna mamilioni ya bacteria wanaotuzunguka ambao hawaonekani kwa macho ndio huleta haya yote na si kwenye vyakula tuu bali hata mwili hasa sehemu zako za siri na mdomoni
mkuu hao bakteria wasionekana kwa macho wanabadilikaje kuwa funza?
Funza si kiumbe kinachojitegemea. Funza ni hatua mojawapo ya viumbe fulanifulani, kama vile nzi. Hivyo basi, uonapo funza, ujue kuna mdudu ametagia mayai yake hapo na yameanguliwa. Jua kuwa funza ni hatua tu Mkuu
Mzee Tupatupa
mkuu chombo kinafunikwa hakuna nafasi ya kupita mdudu, hata hao nzi hawawez kupenya na kutaga mayai. lakini ukifunua chombo unakuta funza!
Baada ya kurutubishwa kwenye hicho chakula hubadilika na kuwa funza
Mkuu hapa natofautiana na wewe. Bacteria hawezi kubadilikA kuwa funza. bacteria atabaki kuwa bacteria. Funza ni hatua mojawapo ya ukuaji wa viumbe hasa wadudu ambao wanapitia hatua za metamorphosis (complete au incomplete).
Mayai hutagwa hata kabla ya kufunikwa
Mzee Tupatupa
Umefunika chakula vizuri kabisaa, hakuna nafasi ya kuingia mdudu yeyote, ila bahati mbaya ukasahau kukiweka kwenye friji.
Siku kadhaa zinapita unafunua chakula unakuta kimeharibika na funza tele wamejaa, wametokea wapi hawa funza?
Nyama ipo ndani ya mfuko au chombo bahati mbaya imeoza unakuta funza kibao, tena wakubwa, wanatokea wapi hawa funza?
Hawa funza huwa wanatokea wapi? ninajiuliza mara nyingi sijawahi pata majibu!!