WanaJF!
Ni wazi kuwa wananchi na hasa wapenzi wa CHADEMA wangependa kujua ni nani kati ya viongozi waliopo mwenye nafasi kubwa ya kuongoza chama hicho kwenye nafasi ya uenyekiti katika ngazi ya taifa.
Ni ukweli kuwa CHADEMA kwa sasa ni chama kikubwa cha siasa nchini, hivyo kwa hadhi hiyo uchaguzi wake ni lazima uwe na hamasa kulinganisha na chaguzi za vyama vingine, hivyo ni haki kwa wananchi kuwa na shahuku na uchaguzi wa CHADEMA.
Katika penya penya zangu na uchunguzi mkubwa nilioufanya kwenye chama hicho, nimegundua kuwa ndani ya CHADEMA kwa sasa ni bwana Godbless Lema ndiye mwenye nguvu na nafasi kubwa ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA taifa.
Itakumbukwa kuwa Godbless Lema ni mbunge wa Arusha mjini, na pia mzaliwa wa Kilimanjaro na ina semekana ana ujamaa na bwana Mbowe, hivyo kwa maelezo haya ni wazi kuwa ametimiza vigezo vikuu vya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA taifa.
Aidha, ndugu Lema kwa sasa anapigiwa 'promo' na mwenyekiti wa sasa, bwana Mbowe, kwa kuhakikisha ana ambatana nae kwenye mikutano mikubwa kwa midogo ya CHADEMA, na pia bwana Mbowe bila kificho uwa ana msifu Lema kuwa ndiye 'jembe' la CHADEMA.
Lakini vilevile ningependa ieleweke kwamba, katika mchakato wa kumpata mwenyekiti au kiongozi mwingine yeyote ndani ya CHADEMA kwenye ngazi ya taifa, vigezo vifuatavyo sio vya muhimu sana;
i) ELIMU, angalau mwombaji awe na elimu ya kidato cha nne, nadhani hii bwana Lema atamudu.
ii) UZOEFU, ni CHADEMA pekee ambayo utoa nafasi kwa mtu kuwa kiongozi pasipo kukitumikia chama kwa kipindi cha angalau miaka mitatu.
iii) MAADILI, hili halizingatiwi kabisa, na imeonekana likiwekwa kama kigezo cha kupata kiongozi ndani ya CHADEMA ni wengi watakosa nafasi.
Hivyo basi, ni wazi kuwa kama sifa tajwa hapo juu zimepuuzwa na CHADEMA katika mchakato wa kumpata mwenyekiti wa chama hicho, ni ukweli usio pingika kuwa Godbless Lema ana andaliwa kuirithi mikoba ya Mbowe.