Fundisho juu ya Agano

Fundisho juu ya Agano

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Je, Agano ni nini?

Agano ni mapatano baina ya mtu na mtu ama baina ya pande mbili na ambalo linawafunga wote wawili . Agano huwa linaambatana na kanuni za Agano ambazo hazipaswi kuvunjwa na zinapaswa kushikwa kama kanuni ambazo zinaunda agano. Mifano ya Agano ni Agano baina ya Mungu na Nuhu [Mwa9:9-17], Agano baina ya Mungu na Abrahamu [Mwa17:1-21], Agano Baina ya Ibrahimu na Abimeleki[Mwa21:27-32,], Agano baina ya Isaka na Abimeleki [Mwa 26:26-33], Agano baina ya Yakobo na Labani [Mwa31:43-54].

Agano la kwanza
Agano la kwanza ni agano ambalo Mungu alifanya na wana wa Israeli, ili awe Mungu wao nao wawe watu wake. Mungu alifanya Agano na wana wa Israeli kwa kanuni ama mkataba wa Amri kumi. Amri kumi zinaitwa Amri za Maagano, ama wakati mwingine zinaitwa Agano la Mungu. [Taz Torati 4:13, na Torati9:9-15] Mungu aliwakutanisha wana wote wa Israel chini ya Mlima, na kisha akazitangaza Amri kumi kwa ngurumo, na radi na tetemeko na giza guu na Moto uliowaka mpaka mbinguni, na kisha Baadaye akafanya Agano na Wana wa Israel kwa Mujibu wa Amri kumi na kwa Mujibu wa Sheria zile zingine na hukumu zake na Maagizo yote ambayo Mungu aliyaagiza kwa kinywa cha Musa ambazo zilikuwa ni mafananuzi ya Amri kumi, na sheria zilizoagizwa ili kuwalinda waisraeli wasipotoke. [Taz Kut19 na Kuto 20]. Agano baina na Mungu na Wana wa Israeli lilikuwa kama ifuatavyo: “Musa aliwaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote ambazo Mungu alimwagiza; na kisha wana wa israel wote wakamjibu Musa kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda.

Ndipo Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ng'ombe. Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa wana wa Israel; nao wakasema, Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii.

Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote. [Kut24:1-8]. Ndipo Baada ya Mungu kufanya Agano na wana wa Israel, aliwapa Upendeleo Musa na Haruni, na Nadabu, na Abihu na watu sabini Miongoni mwa wana wa Israel, wapande Mlimani ili wauone Utukufu mkuu unaomfunika Mungu, na waliruhusiwa kuona Miguu ya Mungu ambayo ilikanyaga sakafu ya mbinguni ambayo mfano wake ni kama yakuti samawi kama mbingu zenyewe kwa usafi wake. Kisha wakafanya Sherehe wakala na kunywa [Kut24:9-11]

Kwa nini Agano la Kwanza liliondolewa.
Agano la Kwanza liliondolewa kwa sababu Wana wa Israeli hawakudumu katika agano la Mungu bali walilivunja Agano lake na Kumuua Mfalme wao na Mungu aliyefanya nao Agano. Walipolivunja Agano la Mungu na Mungu aliwakataa Wana wa Israel kama watu wake. Biblia yasema hivi: “Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana. [Waebrania 8:9]. Waisraeli walitia Muhuri wa uasi wao kwa kumkataa Kristo, Mfalme wao na Mungu wa Baba zao, na kuwaua mitume wa Yesu. Kristo alipokufa na Agano ambalo Alifanya nao zamani nalo likavunjika. Biblia yasema hivi: “Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote.[Zekaria11:10].

Lakini pia agano la Kwanza liliondolewa kwa sababu lilijengwa juu ya kafara na damu za wanyama ambazo kwa zenyewe hazikuweza kuondoa dhambi, na kwamba ziliagizwa ziwe kama vivuli vinavyowakilisha kafara na damu ya Kristo, na ambavyo vitakoma wakati Kristo atakapokuja, Yeye aliye kafara halisi. Kuhusu Makafara Biblia yasema hivi; “Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. [Ebr10:4-7].

Na tena maandiko yanasema hivi: “Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. [Ebr10:1-2]. Hivyo agano la kwanza liliondolewa kwa sababu ya Upungufu kwa upande wa Wana wa Israel kwa sababu hawakulishika, na pia kwa sababu ya Upungufu kwa upande wa makafara kwa sababu kwa Yenyewe hayakuweza kuondoa dhambi. Maandiko yanasema hivi: “Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili [Waebr8:7]. Na tena Biblia inasema hivi: “Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka. [Waebr8:13]

Ni kipi katika Agano la kwanza ambacho hakikuondolewa?
Ingawa Agano ama makubaliano ama mapatano baina ya Mungu na wana wa Israeli yalivunjika, Mkataba wa Agano ama mbao za Agano, ama Sheria za Agano yaani zile Amri kumi ziliendelea kubaki hata milele kuwa Kanuni za wale wote watakaoitwa kuingia katika Agano na Mungu. Kuhusu sheria hizi Maandiko yanasema hivi: “Mimi sitalihalifu agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo, [Zaburi89:34].

Amri kumi sii tu kwamba zilikuwa ni Sheria za Mungu ambazo aliwapa Wana wa Israel, na ambazo alifanya nao Agano kwa Hizo; Bali pia Amri kumi za Mungu zilikuwa ni Sheria za Mungu ambazo zilitolewa kwa ajili ya wanadamu wote. Wote watakaomjia Mungu na kufanya Agano naye hawatapewa sheria zingine Zaidi ya Amri kumi. Amri kumi za Mungu ni kamilifu na wala haina mapungufu wala unyonge wowote. Biblia yasema hivi: “Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima. [Zab19:7].

Amri kumi ni mafunuo ya Utakatifu, haki, na wema wa Mungu. Biblia yasema hivi: “Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. [Warumi7:12]. Amri kumi ni mafunuo ya Upendo wa Mungu. Biblia yasema hivi; “Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. [War13:9-10]. Amri kumi za Mungu ni za Milele.

Biblia yasema hivi: “Haki yako ni haki ya milele, Na sheria yako ni kweli. [Zab119:142]. Amri kumi ziliandikwa kwa kidole cha Mungu. Biblia yasema hivi; “Bwana akanipa zile mbao mbili za mawe zimeandikwa kwa kidole cha Mungu; na juu yake yameandikwa maneno mfano wa yote aliyosema nanyi Bwana mle mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano. [Torati9:10]. Kazi ya Mikono ya Mungu inadumu Milele wala haiwezekani kuizidisha kitu wala kupunguza kitu. Biblia yasema hivi: “Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.

[Mhubiri3:14]. Ni Amri hizi ambazo Yesu Mwenyewe alizishuhudia kuwa ni vyepesi Zaidi Mbingu na nchi vikatoweka kuliko itanguke hata Nukta ya torati. Biblia yasema hivi: “Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. [Math5:18]. Na tena Biblia yasema hivi: “Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati. [Luka16:17]. Amri hizi ndizo zinazojulisha dhambi. Biblia yasema hivi: “Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani. [Warumi 7:7]. Na sheria hizi ndizo zitakazowahukumu watu siku za Mwisho. Biblia yasema hivi; “Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru. [Yak2:12]

Agano la pili
Agano la Pili ni Agano ambalo Mungu alifanya na watu wake kwa njia ya Yesu Kristo. Kuhusu Agano hili Unabii wa Biblia unasema kwamba Yesu angefanya Agano na watu wengi kwa Mda wa Juma moja. Biblia yasema hivi “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu. [Daniel 9:27].

Yesu alipokufa pale msalabani mwaka 31AD[Nusu Juma ya unabii wa Daniel] Msalaba wa Kristo uliondoa Agano la kwanza na Sadaka zake za kuteketezwa na makafara yake yote na mifumo yote ya Patakatifu pa kidunia, Ukuhani wa kidunia, na sikukuu zote ambazo zilikuwa ni vivuli vinavyomwakilisha Kristo; na kulisimamisha Agano la pili, Na Kristo mwenyewe akawa Mjumbe wa Agano jipya na Damu yake mwenyewe ikawa damu ya utakaso ya Agano jipya. Mwaka 34 AD kulingana na Unabii wa Daniel[Nusu ya pili ya juma la unabii wa Daniel], Wana wa Israeli walitia Muhuri wa uasi wao, kwa Kumpiga Stefano mawe na kuliudhi kanisa. Ndipo mitume wakaachana na Wayahudi na kuzambaza injili kwa watu wa mataifa.

Kuhusu Agano Jipya Biblia yasema hivi: “Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. [Waebr8:6]. Katika Agano jipya Watu wa Mungu wanatakaswa kwa damu ya Yesu mwenyewe. Biblia yasema hivi: “wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. [Waebr9:12-15].

Agano la pili na Amri kumi
Agano la Pili halikufuta zile Amri kumi, bali Amri kumi ziliendelea kuwa kanuni za Agano jipya kama vile ilivyokuwa katika Agano la kwanza.

Wakati ambapo Agano la kwanza ama mapatano ya kwanza yaliondolewa na Mungu akawakataa wana wa Israeli kama taifa wasiwe tena watu wake tena kwa sababu ya Uasi, na akaondoa mifumo yote ya makafara ambayo hayakuweza kwa yenyewe kuondoa dhambi, Amri kumi za Mungu zilibaki kuwa mafunuo ya tabia yake, na kanuni ya wote ambao wataingia katika Agano jipya. Agano la pili liliwaanzisha Wakristo kuwa Israeli ya Kiroho , na Wana wa Ibrahimu kwa njia ya Imani. Hakuna Sheria zingine ambazo Mungu aliwapa Israeli ya Kiroho Zaidi ya zilezile Amri kumi ambazo walipewa israeli ya kale ya kimwili. Kuabudu sanamu ama Uzinzi ama kuua bado inabaki ni dhambi katika Agano jipya sawa na ilivyokuwa katika Agano la Kale.

Katika Agano jipya Amri kumi zinaandikwa mioyoni Mwa wakristo na sii kwenye vibao vya mawe. Biblia yasema hivi: “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu. Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao. Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena. [Ebr8:10-12]

Mbarikiwe sana.
 
yaani Ubarikiwe sana kaka nimejifunza somo hili jumapili na mchungaji yangu mengi ya andishi hilo hakuyazungumza ahsante kwa maarifa haya,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom