ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,261
- 4,443
Anahitajika fundi mzoefu wa Ujenzi wa nyumba mkoani Arusha:
Eneo la Ujenzi ni tambarare lina ukubwa wa mita 7 kwa 10 Vipimo vya nyumba vinavyotakiwa ni vyumba vitatu vya kulala vyenye ukubwa wa mita 2.5 kwa 2.5 sebule yenye ukubwa wa mita 3 kwa 3.5 jiko lenye ukubwa mita 1.7 kwa 2 dining yenye ukubwa wa mita 2 kwa 2 vyoo vitatu vyenye ukubwa wa mita 1 kwa 1.3.Veranda moja.
Materials zilizopo ni kama ifuatavyo:
Fundi anayehitajika na kwa ajili ya kuseti msingi,kupandisha boma,kupaua,kufanya finishing,kufitisha milango,kufitisha madirisha,kuweka tiles na kufanya wiring.
Kazi inatakiwa ikamilike ndani ya siku 30 tangu siku ya kuanza.
Kinachotakiwa kufanywa na fundi ni kutoa hesabu ya gharama ya ufundi,ambapo atakuwa analipwa kwa awamu tatu yaani kwa siku kumi kumi na mgawanyo wa kazi utakuwa kama ifuatavyo:
Fundi anayehitajika lazima awe na timu ya wasaidizi wa kutosha na ambao atawakabidhi majina na mawasiliano nao kwa foreman ambao watapewa muongozo wa hatua za kazi ingawa msimamizi wa kazi atakuwa ni fundi mwenyewe.
Fundi awe mkazi wa Arusha na awe na angalau kazi tano za ujenzi ambazo alishafanya kwa hivi karibuni kwa jaili ya kuonyesha na awe na ramani kadhaa ambazo ataonyesha kwa mtoa kazi.
Kazi inatakiwa ianze mwanzoni mwa mwezi wa tatu.na ikamilike kabla ya Pasaka.
Angalia mpango wa kazi uliotajwa hapo juu na uainishe kila kazi na gharama zake yaani labour charges.Na angalia kwenye materials zile ambazo unaona zimezidi weka punguzo na zilizopungua weka nyongeza.
Tuma maelezo yako kwenda kwenye pm au kwa email kwenda
mdaumzalendo1@gmail.com.
Wote watakaotuma gharama zao iwapo watakuwa wanaishi Arusha basi watakutanishwa na mtoa kazi kwa ajili ya kujadili mapendekezo yao kwa pamoja na kisha mtoa kazi ataamua kazi atampa nani.Ni muhimu kueleza idadi ya kazi ambazo umezifanya katika kipindi kifupi kilichopita,gharama ya kazi hizo,muda uliotumia mpaka kukamilisha na maeneo kazi hizo zilipo na kama tunaweza kwenda kuziona.
Karibuni sana kwa fursa hii adhimu.
Wasalaam
PBK

- Tofali zipo 1500
- Mbao zipo 4x2 futi 1200(Zitatumika pia kwenye draft ya ceiling),3x2 futi 750 bati 50 za mita 3
- Cement ipo mifuko 60
- Mchanga Upo Lori 3
- Mawe yapo Lori 3
- Rangi zipo Lita 100 mchanganyiko wa maji na mafuta
- Gypsum powded ipo mifuko 20
- Gypsum board zipo pieces 40
- Tiles zipo floor tiles box 20,wall tiles box 6
- Maji yapo pipa 10
Fundi anayehitajika na kwa ajili ya kuseti msingi,kupandisha boma,kupaua,kufanya finishing,kufitisha milango,kufitisha madirisha,kuweka tiles na kufanya wiring.
Kazi inatakiwa ikamilike ndani ya siku 30 tangu siku ya kuanza.
Kinachotakiwa kufanywa na fundi ni kutoa hesabu ya gharama ya ufundi,ambapo atakuwa analipwa kwa awamu tatu yaani kwa siku kumi kumi na mgawanyo wa kazi utakuwa kama ifuatavyo:
- Kuseti msingi na kuchimba siku moja.
- Kujenga msingi na kupandisha boma line mbili za tofali siku 2
- Kumwaga floor slab siku moja
- Kupandisha boma mpaka lenta siku 2
- Kufunga lenta siku moja
- Baada ya hapo mapumziko siku mbili
- Kupandisha line mbili siku moja
- Mapunziko siku nne
- Kupaua,yaani kutengeneza kenchi na kuweka bati siku nne wakati huo huo madirisha na milango yanafitishwa
- Kupiga draft siku 3
- Kufanya wiring siku mbili
- Kuchapia ndani na nje siku tatu
- Kuweka ceiling siku 2
- Kuweka tiles siku tatu
- Kupiga rangi nje na ndani siku tatu
- Kuweka vioo siku moja
- Kupiga fensi ya tofali siku mbili line 7