Wewe vumilia tu kaka, Baada ya miaka kumi watu watakuja kujua kwamba uliwatangulia vibaya sana kuwa na vision. Kama ilivyo Bongo wakati huo nadhani watu wengi watakuwa wameshaku-copy.
Mimi binafsi simfahamu muhusika anayefanya biashara hii lakini nina sababu 3 kubwa za kumuunga mkono:
1. Hili suala la ku-anlock kwa mtindo huu nalifahamu, lipo na nimewahi kulifanya. Hivyo hakuna kiroja kipya hapa.
2. Matapeli huwa hawaipendi paypal kwa sababu Paypla hurudisha fedha za wateja kisha humfatilia muhalifu. Sasa jamaa ameweka paypla kwenye web yake.
3. Nimepitia website yake nimejifunza kwamba huyu sio tapeli, nasema hivi kwa sababu binafsi nimewahi kuibiwa kwenye eBay. Nilinunua HTC Advantage miaka mingi nyuma, ingawa nilirudishiwa fedha zangu na Paypal matapeli huweka vivutio viwili katika mitandao yao:
a. Huweka vitu vingi vya thamani kubwa na vyenye kuvutia mno
b. Hutangaza urahisi wa bei ili kuwa vutia wengi.
Huyu jamaa ana simu zake chache ambazo ni used, kwenye sehemu ya simu mpya hana hata simu moja. Hivyo uzoefu unonyesha huyu si tapeli kama ambavyo wengine wameanza kumshutumu. Mwisho namuunga mkono kwa sababu lazima na sisi tuwe tech driven. Tutaendelea kuiogopa teknolojia mpaka lini?