Fundi milionea mtarajiwa au mfungwa mtarajiwa?

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,348
559
Nimeona kwenye TV ya Tanzania (TBC) jana kuwa kuna fundi mmoja amekamatwa kwa kutengeneza mizani ambazo hazikidhi ubora.

Tanzania tumezoea kuagiza mizani toka Kenya, lakini huyu baba, kwa kuona soko la mizani TZ ni la wachovu pia, wasioweza kumudu bei ya hizo originals, alitumia ujuzi wake na local materials, kama sikosei akatengeneza mizani ambazo zinauzika vizuri tu, kwa maoni yangu huyu ndio sifa kubwa ya mwalimu wake, huyu ni independent thinker wa siku za sasa, huyu ni fundi anayetamani, anayepanga na kutekeleza ndoto yake, huyu analijua soko.

je huyu ni milionea mtarajiwa???

Au ni mfungwa mtarajiwa kwa kuwa ametengeneza bidhaa bila kukidhi viwango?

Wataalamu tusaidieni
 
ilitakiwa wamuendeleze huyu mzee! aah Tanzania nakupenda kwa moyo wote
 
Yule ndugu yake na EWURA anayeitwa Wakala wa Vipimo si ndio kazi yake hiyo ya kupita madukani na kukagua mizani ? Akikuta haifai anaichukua na kuondoka nayo.
 
huyu ni independent thinker wa siku za sasa, huyu ni fundi anayetamani, anayepanga na kutekeleza ndoto yake, huyu analijua soko. Au ni mfungwa mtarajiwa kwa kuwa ametengeneza bidhaa bila kukidhi viwango?

Hana tofauti na Babu wa Loliondo. Lakini Mbona Babu yeye alipewa ushirikiano na Serikali hadi ulinzi?
 
Nimeona kwenye TV ya Tanzania (TBC) jana kuwa kuna fundi mmoja amekamatwa kwa kutengeneza mizani ambazo hazikidhi ubora.

Tanzania tumezoea kuagiza mizani toka Kenya, lakini huyu baba, kwa kuona soko la mizani TZ ni la wachovu pia, wasioweza kumudu bei ya hizo originals, alitumia ujuzi wake na local materials, kama sikosei akatengeneza mizani ambazo zinauzika vizuri tu, kwa maoni yangu huyu ndio sifa kubwa ya mwalimu wake, huyu ni independent thinker wa siku za sasa, huyu ni fundi anayetamani, anayepanga na kutekeleza ndoto yake, huyu analijua soko.

je huyu ni milionea mtarajiwa???
Au ni mfungwa mtarajiwa kwa kuwa ametengeneza bidhaa bila kukidhi viwango?

Wataalamu tusaidieni

kwa maoni yangu huyu mzee ni miongoni mwa watu wachache wanaohitajika na tanzania yetu ya leo, anahitaji kuendelezwa na akawa msaada kwa taifa letu masikini, hadi kufikia kutengeneza hizo mashine inaonyesha ana uelewa mkubwa katika hayo maswala labda kuna kipengele kimoja kidogo tu ambacho eidha anakisahau au hajagundua kwamba kinashusha ubora wa bidhaa anazozitengeneza au anafahamu kila kitu mpaka hilo tatizo lenyewe lakini kutokana na mtaji mdogo na gharama kubwa za matengenezo inabidi afanye hivyo kubalance mapato na matumizi ili mwisho wa siku asije akafilisika!

huyu sio mfungwa mtarajiwa bali bilionea mtarajiwa, hakuna haja ya kwenda kununua mashine hizo nchi za nje na kuzinufaisha nchi hizo wakati kumbe tunaweza kuzitengeza sisi wenyewe, baadala ya kumfungulia mashitaka huyo mzee nilikuwanashauri:
mzee huyo ambaye binafsi naweza kumwita shujaa ahojiwe juu ya bidhaa anazotengeneza matatizo ama changamoto anazokumbana nazo, nini anahisi kingeweza kufanyika ili kuweza kuongeza ubora wa mashine zake kisha serikali imwezeshe ili aweze kutengeneza mashine bora zaidi na ikiwezekana kijengwe kiwanda ambacho atafanya kazi kama mfanyakazi wa serikali hatimaye tuachane na ununuzi wa hizo mashine nje ya nchi.
 
Huwa napandwa na hasira sana na hii serikali inayovamia matukio badaala ya kuangalia chanzo na kukitumia/kukiendeleza kwa njia chanya.

Kuna yule kijana aliyekuja na namna ya kutengeza simu COSTECH wakmbeza heti hana lolote ni utundu tu wa mitaani,basi kaishia zake........tatizo hatujui kuthamini chetu.....bado tuna fikra za kitumwa zaidi

Wako jamaa wanatengeza magobole lakini wanawindwa kisa wanasaidia majambazi,badala ya kuwekewa taratibu bora za ubunifu wao
 
Back
Top Bottom