Fumbo pasua kichwa 4: Nani alimuua Bwana Kizito?

Fumbo pasua kichwa 4: Nani alimuua Bwana Kizito?

Kati ya Mama na mfanyakazi wa ndani kuna mmoja kati yao ni muhusika nina hakika hakuna umbali mkubwa sana kati ya alipokuwa mfanyakazi wa ndani na hapo sebuleni alipokuwa mzee...maana kama kuna mtu alipita hapo au kuingia ndani basi wa kwanza kumjua au kumsikia ni mfanyakazi wa ndani na kwa case hiyo lazima angesikia..

Lakini nikijaribu kufikiri zaidi ni nani kati ya mfanyakazi na Mama nani ana interest kwenye kifo moja kwa moja nitakwambia ni mama maana kwa vyovyote kinacho mkuta mzee hasa kifo yeye lazima awe mmoja wa warithi wa mali za mzee huyu.

Kuna uwezekano huyu mama alimvizia Mzee kwa nyuma na kumpiga na kitu kizito na kurudi kule juu na kujifanya anaendelea kusoma kitabu halafu huyu

Hivyo muuaji ni huyu Mama
 
kwakua ni fumbo,nami ninalijibu ki fumbo Fumbo..
Bwana KIZITO hakuuawa na mtu yeyote,hlo jina lake lina akisi taswira ya mtu aliye na mwili mkubwa(Mnene),Hivyo alikufa pengine kwa presha,mshtuko wa Moyo n.k
Na hakuna mtu aliyekamatwa,ila walihojiwa kawaida tu
 
Muuaji ni mke wake, maana alikuwa maktaba anasoma magazeti, akaja na gazeti moja wapo kusingizia kuwa mzee alikuwa anasoma gazeti!
 
Fumbo ni hiyo tarehe 25 julai ya mwaka 2010 inaangukia JUMAPILI..hivyo mfanyakazi wa usafi alitakiwa kuwa katika shughuli zake za usafi kwa kuwa
1. jumapili sio siku ya kazi kwa dhl
2. Dhl inapokelewa na muhusika na kusainiwa kwamba amepokea Mtu husika wakati mzee kizito alikuwepo ndo alifaa kupokea.
 
Binafsi nitasema mpishi (Cook-not cooker!?) maana hakuna maelezo alikuwa wapi wakati wa tukio hilo. Kama neno cooker lilikuwa na maana ya Jiko then suspect ni mke maana ana maslahi na kifo cha mumewe na pia moja ya vitu vinavyokuwepo kwenye 'maktaba yao' ni magazeti. Hivyo bwana Kizito aliuawa maktaba.
 
Jibu hapo ni mpishi kwa maana hakua na kitu anafanya wengne wote walikua na kaz zao
Embu nipe like zangu bwana mtambuz
 
kuna possibility kubwa kuwa mke wa kizito kwanini......siku ya mauaji mfanyakazi mmoja wa nje (gadner)hakuwa na kazi kama ingekua ni kuchukua mzigo ulioletwa na DHL ilibidi aende yeye...sasa ilikuaje Mke aliamua kumtuma kwa makusudi mfanyakazi wa ndani ili apate nafasi ....na ukiangalia yeye ndie MTU wa kwanza kutoa taarifa kabla ya mwingine ....na anadai alikua juu anasoma ingekua hivo asingekua wa kwanza kutoa taarifa yeye
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Ngoja niendelee kufatilia huu uzi kwa ukaribu mana kuna wengine wanatoa maelezo badala ya jibu..mimi nipo baki benja ntajibu badae
 
Back
Top Bottom