Fumbo pasua kichwa 4: Nani alimuua Bwana Kizito?

Fumbo pasua kichwa 4: Nani alimuua Bwana Kizito?

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
upload_2016-10-12_16-41-42.png


Mnamo tarehe 25 Julai 2010 majira ya asubuhi, tajiri mmoja maarufu aliyetambuliwa kwa jina la Bwana Kizito alikutwa ameuawa nyumbani kwake kwa kupigwa na kitu kizito kichwani alipokuwa sebuleni amekaa akisoma gazeti.

Mkewe aliwajulisha Polisi kuhusu tukio lile na mara askari wa upelelezi akafika katika eneo la tukio pamoja na wataalamu wa kuchunguza eneo la tukio na kuchukua ushahidi.

Katika nyumba ile pamoja na mke wa tajiri huyo, pia walikuwepo Mfanyakazi wa Bustani (Gardener), Mpishi (Cooker), Mfanyakazi wa usafi wa ndani (Maid), na Mfanyakazi wa kuhudumia chakula (Butler)

Wakati wa mahojiano ya awali Mke wa marehemu alidai kwamba likuwa ghorofani kwenye maktaba yao akijisomea, Mfanyakazi wa Bustani yeye alidai kwamba alikuwa akipanda maua bustanini, Mfanyakazi wa usafi wa ndani yeye alidai wakati mauaji yanatokea alikua akipokea bahasha iliyoletwa na kampuni ya kusambaza mizigo ya DHL na mfanyakazi wa kuhudumia chakula yeye alidai kwamba wakati mauaji hayo yanatokea alikuwa akifuta vyombo na kuvipanga kabatini.

Baada ya mahojiano yale mtuhumiwa alikamatwa akiwa ni mmoja wa wale waliohojiwa.

Je ni nani kati ya wale waliohojiwa na Askari wa upelelezi na alimjuaje?
 
Hili fumbo halijakamilika.
Askari walipofika waliukuta mwili wa bwana Kizito wapi?
Nikiwa na maana ya sebuleni,chumbani,jikoni n.k
Ungeainisha eneo ulipokutwa mwili ingekuwa rahisi kuunganisha dots.
 
Hili fumbo halijakamilika.
Askari walipofika waliukuta mwili wa bwana Kizito wapi?
Nikiwa na maana ya sebuleni,chumbani,jikoni n.k
Ungeainisha eneo ulipokutwa mwili ingekuwa rahisi kuunganisha dots.
Unaweza kuwa sahihi, Mwili ulikutwa sebuleni alikuwa amekaa akisoma gazeti
 
mfanyakazi wa Usafi ndie muuaji coz ile bahasha inawezekana iliwekwa sumu
 
Too short to make any conclusion about the real killer.
 
aliekuwa anafuta sahani.alijuaje wakati anafuta hizo sahani alijuaje mauaji yanatendeka
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Kitu kizito kichwani? Kwa hayo mazingira suspect wa kwanza huyo aliyekuwa anapanga vyombo......alimpiga na sahani ngumu kichwani? Ngoja madaktari watatujuza zaidi......hahhaaa.... Mkuu Mtambuzi kweli hili fumbo pasua kichwa
 
Back
Top Bottom