Dah! Uzi unaanzishwa baada ya mechi kuisha! Kweli hali ni mbaya.
Sema niliyojifunza kwenye hii mechi ya leo ni haya yafuatayo:-
1. Timu haina kocha wa kuipeleka timu mbali Kimataifa. Goncalves, hakuna kocha pale. Jamaa anabahatisha tu. Ili umgundue kwa urahisi, angalia sub zake.
2. Wachezaji wa kigeni wenye sifa ya kubakia msimu ujao ni 6 tu (Djugui Diarra, Duke Abuya, Prince Dube, Pacome Zouazoua, Max Nzengeli na Allan Okello). The rest hawawezi kuisaidia Yanga kuchukua ubingwa wa Afrika. Yule DEPU pamoja na kubebwa na kocha wake, bado haendani na mfumo wa uchezaji wa Yanga.
3. Ukija kwa wachezaji wazawa, ndiyo usiseme! Wachezaji kama Farid Mussa, Aboubakar Salum (Sure Boy), wale Wazanzibari wawili (Casemiro na Ninju sijui) na wenzao wengi walitakiwa nao kupewa mkono wa kwaheri.
Kama hayatafanyika maboresho ya msingi mwishoni mwa msimu huu, basi msimu ujao ubingwa utachukuliwa na simba.