Safari hii sigara, bia, soda, juisi havikuguswa. Ila moto wake subiri kwenye kiama cha wenye matenki ya mafuta ikiwemo CCM yenyewe....
My General summary below,
VI. SURA YA BAJETI KWA MWAKA 2015/16
19. Mheshimiwa Spika, jitihada hizi za kuongeza mapato zitatusaidia pia kupunguza utegemezi wa Bajeti ya Serikali kwa fedha za wahisani. Kwa hakika, Serikali imeendelea kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kupunguza utegemezi wa bajeti ambapo kiwango cha utegemezi kimepungua kutoka asilimia 24 mwaka 2004/05, asilimia 17 mwaka 2010/11, na kufikia asilimia 6.4 mwaka 2015/16???????? Katika kifungu cha 106 cha hotuba yake waziri kinaonyesha wahisani watachangia takribani 11%, nini maana yake hapo? Ona mwenyewe hapa chini.
Fuatilia sehemu ya 105 -107 Sumamary ni kama ifuatavyo:
Bajeti ya Serikali ni shilingi bilioni 22,495.5 kutoka kwenye vyanzo vya ndani na nje = Mapato ya kodi na mapato yasiyo ya kodi yanatarajiwa kufikia shilingi bilioni 13,475.6 (60%) + mapato kutokana na vyanzo vya Mamlaka za Serikali za Mitaa yanatarajiwa kufikia shilingi bilioni 521.9 (2.3%) + Washirika wa Maendeleo wameahidi kuchangia shilingi bilioni 2,322.5 (11%) + Serikali inatarajia kukopa kutoka katika vyanzo vya ndani na nje shilingi bilioni 6,175.5(27%).
108. Mheshimiwa Spika, Serikali imekadiria kutumia jumla ya shilingi bilioni 22,495.5 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, matumizi ya kawaida ni shilingi bilioni 16,576.4 ambayo yanajumuisha shilingi bilioni 6,466.5 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali, Wakala na Taasisi za Serikali; shilingi bilioni 6,396.6 ni kwa ajili ya Mfuko Mkuu wa Serikali, na matumizi mengineyo shilingi bilioni 3,713 (nini hii vitumbua na chai posho ya kuhudhulia kikao katika gorofa ya kwanza ili hali anayehudhulia /mtumishi anatoka gorofa ya sita ???. Matumizi ya maendeleo ni shilingi bilioni 5,919.1 bila kujumuisha matumizi ya kawaida yenye sura ya kimaendeleo. Aidha, matumizi ya maendeleo ni asilimia 37.4 ya Bajeti yote ambayo inajumuisha matumizi ya kawaida yenye sura ya kimaendeleo yanayolipwa kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali.
Mikopo ya Kibiashara kutoka Nje
35. Mheshimiwa Spika, mwaka 2014/15, Serikali ilipanga kukopa dola za Marekani milioni 800 sawa na shilingi bilioni 1,320.01 kutoka kwenye vyanzo vya nje vya kibiashara ili kugharimia miradi ya maendeleo. Hadi Aprili 2015, Serikali imekopa dola milioni 300 (sawa na shilingi bilioni 5142)????????? kutoka Benki ya Maendeleo ya China (CDB), kiasi hiki ni asilimia 39 ya kiwango kinachopaswa kukopwa kwa mwaka. Kutokupatikana kwa mikopo kwa kiwango kilichopangwa kwa wakati kunatokana na masharti ya mikopo yanayo badilika mara kwa mara ya soko la fedha duniani na kutokana na mchakato mrefu wa majadiliano. Hata hivyo, taratibu za kukamilisha upatikanaji wa fedha zilizobakia zinaendelea.
Mheshimiwa Spika, ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi pia utaimarishwa kwa kuchukua hatua mbalimbali. Kwanza, ni lazima mfumo wa kieletroniki utumike katika utoaji wa risiti kwa tozo, faini, ada na malipo mengine yote ya Serikali kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakala wote wa Serikali. Narudia. Ni lazima sasa mfumo wa kieletroniki utumike katika utoaji wa risiti kwa tozo, faini, ada na malipo mengine yote ya Serikali kuu, mamlaka za serikali za mitaa na wakala wote wa Serikali. Hii itahusisha pia malipo ya faini mahakamani, faini za usalama barabarani, viingilio kwenye mbuga za wanyama, vibali vya kuvuna maliasili, na kadhalika.
Moja ya hatua muhimu katika hili ni kupitia upya viwango vya posho za safari katika taasisi na mashirika ya umma. Kupunguza ununuzi wa mashangingi vipi?
Hatua iliyofikiwa katika Kukamilisha Zoezi la Nchi Kufanyiwa Tathmini ya Kukopa na Kulipa Madeni
54. Mheshimiwa Spika, majadiliano kati ya Serikali na Kampuni za Moody na Fitch Ratings zitakazofanya kazi ya kutathmini uwezo wa kukopa katika masoko ya fedha ya kimataifa yamekamilika. Ni matumaini yetu kwamba, mikataba baina ya Serikali na Makampuni hayo itasainiwa kabla ya Julai, 2015. MORE DETAILS PLEASE!!??
Changamoto.
(iii) Mashirika mengi ya Umma kuendelea kutegemea bajeti ya Serikali kama vile TANESCO, ATCL, TRL na TAZARA na hivyo kuongeza gharama ambazo zingepaswa kulipwa na mashirika yenyewe kama yangekuwa yanajiendesha kwa faida; PIGA CHINI Directors/Managers!!! If you dont produce do you expect payment??? Asiye fanya kazi na asile, basi! Mnawaendekeza au kwa vile wnachangia chama??
(vi) Mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yamesababisha maafa mbalimbali yakiwa ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ya usafirishaji; ukosefu wa chakula; ukosefu wa umeme unaozalishwa kwa nguvu za maji; na upotevu wa fursa za ajira; Ni Jitihada zipi zenye kuleta tija zilizo chukuliwa na Serikali kulinda na kuendeleza utunzaji wa mazingira ? Hakuna, unategemea nini ??
(vii) Kuimarika kwa dola ya Marekani dhidi ya sarafu mbalimbali, kumeongeza gharama za uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje; Ni jitihada gani / zipi zimechukuliwa na seriakli kukabili fedha ya Tanzania isiporomoke thamani?
Sababu za kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania zimetajwa na hatua zilizo chukuliwa eti ni hizi hapa chini, kweli ??? soma mwenyewe kama pumba utajaza mwenyewe
. Mh !
66. Mheshimiwa Spika, napenda kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge na wananchi wote kuwa Serikali inachukua hatua muhimu za kuhakikisha thamani ya shilingi yetu inaendelea kuimarika. Hatua hizi ni pamoja na kuimarisha Maeneo Maalum ya Kuzalisha Bidhaa za Kuuza Nje (Export Processing Zones) na Maeneo Maalum ya Uwekezaji Kiuchumi (Special Economic Zones). Hivyo ni rai yetu kwa Watanzania kuzitumia fursa hizi ili kuongeza mauzo yetu nje sambamba na kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma zisizo za lazima kutoka nje ili thamani ya shilingi yetu iendelee kuimarika.
(viii) Kubadilika mara kwa mara kwa bei ya nishati ya mafuta kumekuwa kunachangia kuongeza gharama za uzalishaji na bei ya bidhaa mbalimbali za walaji. Hapa hakuna sababu, Mwaka huu bei ya mafuta haikupanda sana. Ilikuwa poa kabisa kuliko kipindi chochote kwa miaka ya hivi karibuni !
Mafanikio :
60. Uwekezaji huu, umesaidia kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme kutoka megawati 788.68 mwaka 2010 hadi megawati 1,226.3 mwaka 2014. Aidha, usambazaji wa umeme vijijini umeongezeka kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA), na hivyo kuongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma ya umeme kutoka asilimia 7 mwaka 2011 hadi asilimia 36 mwaka 2014. Wewe unaye soma mstari huu, hali ikoje kijijini kwenu ? Ni kweli idadi ya watu / kaya zenye umeme ni sawa na asilimia 36 ?????
Nimeipenda hii, 72. Mheshimiwa Spika, misingi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/16 ni kama ifuatavyo:-
(iii) Kuwepo kwa hali nzuri ya hewa nchini na katika nchi jirani itakayowezesha uzalishaji mzuri wa mazao ya chakula na biashara. Hivi Serikali ya Tanzania itafanyaje kuhakikisha hali ya hewa ya Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Mawaliwi, Zambia, Kongo etc inakuwa nzuri ??? Taja namna utakavyo fanya na bajeti yake ya utekelezaji, bila bla bla !