Mods. Please!
Waziri Kivuli wa Fedha ndugu MBATIA amesema kwamba kutokana na deni la Taifa kuongexzeka kila mtanzania sasa anadaiwa karibu Tsh laki 9. Yaani hata yule aliyezaliwa leo anadaiwa. Maana yake km kwenye familia yako mpo 6 maaana yake mnadaiwa mil. 5.4.
Km hiyo haitoshi Mbatia amesema kuwa kiuhalisia waziri wa fedha amewahadaa watanzania kwani bajeti ilyosomwa ni ndgo kuliko ya mwaka jana kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi. Kwa hiyo nyongeza inayodaiwa kuongezeka ni kiini macho.
Amekumbushia ya Escrow na mengineyo. Endelea kusoma:
Ukokotoaji bajeti
Akiwasilisha bajeti hiyo huku akipigia chapuo Ukawa kuchukua nchi, Mbatia alisema kutokana na takwimu za Benki Kuu za Juni 2014 na Juni 2015, thamani ya shilingi moja ya Juni mwaka jana inazidi Sh1.2 ya leo. Kwa hiyo Sh19.85 trilioni za Juni 2014 thamani yake kwa sasa ni zaidi ya Sh24 trilioni za leo.
Alisema tofauti kati ya mwaka 2014/2015 na 2015/2016 ni Dola 1,143.89 milioni za Kimarekani, sawa na Sh2.36 trilioni. "Punguzo hili ni sawa na asilimia 9.5. Hivyo, leo Serikali inapojigamba kuwa bajeti imeongezeka kutoka Shilingi 19.85 trilioni kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 kufikia Sh22.5 trilioni kwa mwaka wa fedha 2015/2016 siyo sahihi.
"Kwani inasahau kuwa thamani ya shilingi ya leo ni pungufu ya thamani ya shilingi ya mwaka jana. Hii ina maana kuwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2015/2016 ni ndogo kuliko bajeti ya mwaka 2014/2015… Kambi ya Upinzani inasikitishwa na kitendo cha Serikali kushindwa kuwaeleza Watanzania ukweli wa ongezeko hasi la bajeti ambalo haliendani na thamani ya Shilingi kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016," alisema.
"Kitendo cha Serikali hii kuwadanganya Watanzania kwa kuwapa tumani hewa ya ongezeko la bajeti ni cha kupingwa kwa nguvu zote na watu wote kwa manufaa ya Mama Tanzania."
Mbatia alisema Serikali hukusanya mapato kutoka kwa walipa kodi, kwa uadilifu na kupanga kutumia mapato hayo, kwa uangalifu; katika maeneo yatakayostawisha jamii nzima na kusema kinyume na matarajio ya wengi, Serikali imeshindwa kutimiza malengo yake, ikiwemo kukusanya kodi bila uadilifu na hivyo kuchochea vitendo vya rushwa, ufisadi na ubadhirifu.
"Kutokana na kashfa ya ufisadi wa miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow, wahisani walisitisha misaada ya bajeti kwa hoja kuwa viongozi wa Serikali walipanga na kufanikisha mbinu za kuliibia Shirika la Umeme (Tanesco) lenye matatizo makubwa ya kifedha," alisema.
"Hadi kufikia Aprili 2015, wahisani waliipa serikali mikopo na misaada ya kibajeti ya Sh406 bilioni ukilinganisha na ahadi ya Sh922 bilioni, sawa na asilimia 40. Serikali imepokea mikopo na misaada ya miradi ya maendeleo Sh 1.4trilion ukilinganisha na bajeti ya Sh2.0 trilioni sawa na asilimia 70 ya bajeti.
"Mikopo yenye masharti ya kibiashara haikupatikana kama serikali ilivyotarajiwa, lakini swali la kujiuliza, kwenye nchi yenye rasilimali za kutosha inawezaje kuweka mikopo kama mojawapo ya vipaumbele cha vyanzo vya uendeshaji wa bajeti yake? Hili ni jambo la aibu kubwa, kuona kuwa Serikali inashindwa kutekeleza miradi yake ya maendeleo kwa kuwa walipoomba kukopa, mikopo hiyo haikutolewa."
Alisema miradi ya maendeleo ndiyo iliyoathirika zaidi kwa kuwa hadi kufikia Aprili 2015 ilikuwa imepata asilimia 40 tu ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge wakati matumizi ya kawaida yalikuwa asilimia 86.
"Swali la kujiuliza, unaendeshaje uchumi ambao hauna fedha za miradi ya maendeleo lakini fedha za mishahara na posho zinaendelea kulipwa?" alihoji.
Serikali imepanga kupunguza utegemezi wa fedha za wahisani hadi kufikia asilimia 6.4 ya bajeti ya mwaka 2015/16, wakati inatarajia kupata misaada na mikopo nafuu ya Sh2,322.5 bilioni kwa mwaka huu wa fedha, kiwango ambacho ni asilimia 10 ya bajeti.
Chanzo: Mwanachi