FULL TEXT: Hotuba ya Lema bungeni

Salama kama hizi nadhani waachie CCM, inatosha kushukuru wapiga kura, chama na ofisi ya Bunge; Huo ndio ushauri wangu.

Otherwise CDM wamejipanga kuliko hata serikali iliopo madarakani sijui kwanini hawataki kupisha ili hili hii nchni isonge mbele.

Nakupinga kwa hili, shukrani ni uungwana mkubwa sana. Bila mkeo kukupa sapoti na amani katika nyumba, kamwe hutafanya lolote la muhimu.

As for Lema, I salute you guy!
 
welcome back home Lema, utatukuta hapa disemba kwenye kijiwe chetu cha garage...
 
NANI KAMA MHESHIMIWA LEMA ???????????

Tatizo letu Watanzania ni kwamba huwa tunachukua MUDA MREFU sana kumjua Mtanzania mwenzetu ambaye ni mwema kwetu, anayeumwa na umasikini wetu, aliye tayari KUTUPIGANIA sisi walalhoi nchini hadi darini.

Japo kamwe siwezi kuwasahau Magwiji wengine wenye uzalendo wa kweli, ujasiri wa kuthubutu, na uchungu wa kweli kwetu kama vile Waheshimiwa Samwel 6, Mwakyembe, Anna Malechela, Ole Sendeka, Hassy Kitine, Augustino Mrema, Prof Lipumba, Mama Tibaijuka, lakini kw kusema ukweli Mashujaa hawa wengi wao wako ndani ya chama cha siasa kinachoitwa CHADEMA.

Hongera sana Mhe Lema, hongereni sana Wenzetu wa Arusha mliotuchangulia kiongozi huyu, hongereni saaaaaaaaaaaaana MACHALII wote Tanzania kwa mshikamano kila kukicha kuleta mabadiliko makubwa na ya kweli bila unafiki wa ki-CCM nchini mwetu.

Mungu ibariki Tanzania na sisi wananchi wake,
Mungu kibariki CHADEMA kutufikisha huko tunakotamani saaaaana,
Mungu wabariki mashujaa wetu wote ndani na nje ya CHADEMA!!!!!!!!

Nipo hapa Arusha mjini vijana wamekusanyika kwenye vikundi vikundi wakijadili hotuba ya Mhe. G. Lema aliyoitoa leo bungeni. Wengi wanashauriana kuandaa maandamano kumpokea mbunge wao mara baada ya bunge kumalizika, sababu wanazotoa ni kwamba kaonyesha ujasiri kwa kuiambia serikali bila woga hali halisi ya maisha ya vijana na wananchi kwa ujumla hasa suala la polisi kuwabambikia kesi na mauaji ya raia wasio na hatia. Wanasema hawajashtushwa na Lema kutolewa nje maana wanajua kazi ya kuwasemea waliyomtuma siyo rahisi kama wengine wanavyofikiri. Nauliza ikiwa Chadema Arusha iko tayari kuwaunga mkono vijana hawa, kwangu naona ni suala la heri wanaJF mna mawazo gani.
 
Umeona eeehhh! I hate this kind of slogan....wengine hushukuru hata vimada wao na walevi wenzao......

Nakupinga kwa hili, shukrani ni uungwana mkubwa sana. Bila mkeo kukupa sapoti na amani katika nyumba, kamwe hutafanya lolote la muhimu.

As for Lema, I salute you guy!

Bwana au Bibi MESTOD hakuna mpumbavu wa kubisha na wewe hapa, kama ndicho kilicho kuleta hapa JF tafuta hao hao wenzio ubishane nao. Huo ushauri haujapewa wewe.

By the way kwanini husipingane na huo ushauri utangaze kupingana na mimi, nyie ndio mlifanya Mrema akakosa Urais 1995 kwa ushabiki wa kipuuzi?
 
Hii ni hotuba iliyoangaza hali halisi ya Mtanzania anayekabiliwa na uozo wa utawala mbovu na rushwa ya kitaasisi.
 
Nakupinga kwa hili, shukrani ni uungwana mkubwa sana. Bila mkeo kukupa sapoti na amani katika nyumba, kamwe hutafanya lolote la muhimu.

As for Lema, I salute you guy!

Stupidity has no price tag ...Lizzy, 2011
 
Mi nafikiri haina maana ya kujikusanya na kwenda kumpokea.......labda tu kwasbabu hatuna kazi za kufanya.........hayo ni mambo anayotakiwa kuyasema mara kwa mara na kuikosoa serikali na kuwakosowa wenzake pale wanapokosea ................NO BIG DEAL
 
Nipo hapa Arusha mjini vijana wamekusanyika kwenye vikundi vikundi wakijadili hotuba ya Mhe. G. Lema aliyoitoa leo bungeni. Wengi wanashauriana kuandaa maandamano kumpokea mbunge wao mara baada ya bunge kumalizika, sababu wanazotoa ni kwamba kaonyesha ujasiri kwa kuiambia serikali bila woga hali halisi ya maisha ya vijana na wananchi kwa ujumla hasa suala la polisi kuwabambikia kesi na mauaji ya raia wasio na hatia. Wanasema hawajashtushwa na Lema kutolewa nje maana wanajua kazi ya kuwasemea waliyomtuma siyo rahisi kama wengine wanavyofikiri. Nauliza ikiwa Chadema Arusha iko tayari kuwaunga mkono vijana hawa, kwangu naona ni suala la heri wanaJF mna mawazo gani.

Mheshimiwa Lema baada ya kuishi maisha ya kawaida na watanzania wenzake, na kisha kupigania kuingia ndani ya baraza la kutunga sheria ameona mengi na kupata ujasiri wa ajabu ambao wataka moyo mkuu.

Lema ameiona serikali yetu sasa na kisima cha maji ambacho unaona maji maangavu lakini ndani kuna vyura, konokono na viluilui vya kila aina.

Lema kaamua kwa dhati kuingia ndani ya kisima na kutifua yaliyofichika ndani ya maji sasa konokono, viluilui na vyura wanaelea juu ya maji. Kazi kweli kwali wajamani.
 
Niliwahi kusema huko nyuma kuwa wabunge wa ccm wanatumia wingi wao bungeni kupambana na CHADEMA wakidhani kuwa CHADEMA ni chama cha siasa tu. Hii ni fikra potofu na naweza kusema CHADEMA ni 'Movement' ya watanzania waliopigika kimaisha chini ya utawala mbovu wa ccm. Na kwa maana hiyo CHADEMA (wananchi wa kawaida) ni wengi kushinda hiyo idadi ya ccm bungeni na mbaya zaidi ni wananchi hao wenye kauli ya mwisho juu ya nani arudi bungeni. CCM wanaweza kutumia kiti cha spika (DODOMA) kuzima hoja za wabunge wa CHADEMA lakini huku mtaanni hawawezi kuzima CHADEMA - Poeple's power. Hii hatari kubwa sana kwa ccm and the sooner they realize this the better.

Nashauri baada ya mkutano wa bunge kuisha Dodoma, CHADEMA ipite kila mahali kuelimisha umma wa Tanzania kile kilichopitishwa kwenye bajeti ya kila Wizara ili wananchi waweze kuwabana wala rushwa kwa karibu zaidi. Chambueni bajeti moja hadi mwisho na mapungufu yake na semeni waziwazi ni wapi hoja nzuri ilikatiliwa ili wapiga kura wajue wawakilishi wa kweli ni wepi na FEKI ni wepi.
Ni sawa kabisa mkuu,
Nadhani Mh. Rais (JK) anao uelewa wa kinachoendelea kuhusu CDM ndiyo maana kila muda unakuta anashangaa (Mfano Dodoma kwenye semina alisema "mbona serikali ya CCM imeleta maendeleo mengi tu na sijui kwa nini viongozi wa serikali hawayasemi?"), tatizo lilopo kwa viongozi walio wengi ni kufanya kazi kwa kuogopa kivuli cha walio juu yao badala ya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni.
 
Mi nafikiri haina maana ya kujikusanya na kwenda kumpokea.......labda tu kwasbabu hatuna kazi za kufanya.........hayo ni mambo anayotakiwa kuyasema mara kwa mara na kuikosoa serikali na kuwakosowa wenzake pale wanapokosea ................NO BIG DEAL

Tumekuwa na wawakilishe wetu miaka yote hii hakuna anayefunua uchafu wote huu na jinsi serikali inavyoshindwa kuridhia sheria ya umoja wa mataifa kuhusu haki za raia.

Kujitokea kumpokea nakumwunga mkono maana yake tunakubaliana na kazi tuliyomtuma na ni kichocheo kwa wabunge wengine waone mtu unapotetea maslahi na haki za raia unakubalika zaidi na umma.
 
Safi sana Lema, watanzania wengi wanajivunia usmart wenu. Sio kama akina Ndugai na mawazo ya kindugai yeye anaona sifa kutumia cheo chake wakati ni dhamana tu na ni fedheha kwake baadae maana ameudhi maeleu ya watu, sijui jimboni kwake amewapa nini hata wakamchagua.
 
sioni tija ya yeye kupokelewa kama shujaa wakati vita ndio kwanza inaanza
<br />
<br />
ni ipi njema kati ya ile ya LOWASA kupokelewa kama shujaa baada yakujiuzulu au Hii ya LEMA?
 
Maskini hawa askari wetu kumbe wanakatwa 5000/= kila mwezi za kuandaa mazishi yao.
Natamani maandamano ya kudai warudishiwe pesa zao yaje upesi nione nani atatupiga mabomu.
 
Mi nafikiri haina maana ya kujikusanya na kwenda kumpokea.......labda tu kwasbabu hatuna kazi za kufanya.........hayo ni mambo anayotakiwa kuyasema mara kwa mara na kuikosoa serikali na kuwakosowa wenzake pale wanapokosea ................NO BIG DEAL
<br />
<br />
That is part of motivation and not only to him it's for all MP's
 
Back
Top Bottom