Hongera CDM. Angalienei suala la arusha (umeya) kuna mkono wa nani pale? Tuyamalize tuanza mapya, Lema pls play your part, tumechoka sasa. Moja ya sifa za chama bora ni kuwa na uwezo wa kutatua matatizo kwa wakati.
Hii ndiyo sauti halisi ya wananchi na kweli huyu ni waziri kivuli cha umma wa watanzania kuhusu wizara ya mambo ya ndani. hao akina kagasheki , lukuvi na nahodha ni mawazriri wa serikali hawawezi kuwasemea wananchi zaidi watasema kile ambacho bosi wao anapenda kusikia lakini lema anatumia nafasi yake ya uwakilishi kuwakilisha umma wa watanzania waliowengi.
Nakushukuru,
Baba, Bwana wa mbingu
na nchi, kwa kuwa mambo
haya umewaficha wenye
hekima na akili;
umewafunulia watoto
wachanga; Naam, Baba,
kwa kuwa ndivyo
ilivyokupendeza
You have touched my feeling.
You deserve credit for saying this, but, however we need to act against all form of injustices, which unfortunately our government is its argent
LEMA NI KIBOKO....LAITI CHADEMA WANGEKUWA MADARAKANI WANANCHI WAKIONGOZWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI LEMA HAKIKA WATU WANGEFURAHI...Hofu yangu tu kwa hii hotuba nazani Serikali na wabunge wa ccm wengi inawezekana hawakuelewa bali walikua wakimuangalia kwa jicho la hasira tu. but sisi wananchi wengi Tanzania tumeielewa vema kwa sababu ndio waathirika wakubwa wa ukiukaji wa haki za binadamu.
Wasiwasi wangu waziri husika pamoja uongozi wa Spika wanatumia muda mwingi kusema kuwa Mh Lema amekiuka kanuni na hata kusema anachochea vurugu, lakini kwa maoni yangu hotuba ya Lema inaendena sana na maisha halisi ya watanzania wa leo. Kesi za kubambikizia ni tatizo, FFU wamekuwa kawaida na sasa askari wanatumia silaha za moto.
God bless Godbless Lema....
Ahsante sana Mungu kwa hawa wawakilishi wetu halisi wanaojua wanachokifanya. Mungu azidi kuwabariki sana.
Maneno mengi wameshasema wachangiaji wengine, sikusudii kuyarudia.
Nipo hapa Arusha mjini vijana wamekusanyika kwenye vikundi vikundi wakijadili hotuba ya Mhe. G. Lema aliyoitoa leo bungeni. Wengi wanashauriana kuandaa maandamano kumpokea mbunge wao mara baada ya bunge kumalizika, sababu wanazotoa ni kwamba kaonyesha ujasiri kwa kuiambia serikali bila woga hali halisi ya maisha ya vijana na wananchi kwa ujumla hasa suala la polisi kuwabambikia kesi na mauaji ya raia wasio na hatia. Wanasema hawajashtushwa na Lema kutolewa nje maana wanajua kazi ya kuwasemea waliyomtuma siyo rahisi kama wengine wanavyofikiri. Nauliza ikiwa Chadema Arusha iko tayari kuwaunga mkono vijana hawa, kwangu naona ni suala la heri wanaJF mna mawazo gani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.