Fulikunjombe: Mke wa Maswi aliniangukia

Fulikunjombe: Mke wa Maswi aliniangukia

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,058
Reaction score
134,392
Mambo nyuma ya pazia yameanza kufichuka.Deo mjumbe wa PAC ameeleza jinsi mke wa Maswi alivyomwangukia kumtetea mumewe Eliakim Maswi. Pamoja na ujeuri wa mumewe lakini mama huyu alimwangukia makamu asimwanike. Deo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa alipokuwa akisoma maoni ya kumwajibisha waziri mkuu,alimsikia PM Pinda akishusha pumzi nzito sana. Aidha Zitto naye amebainisha kuwa alilazimika kumuita dada yake Dodoma kumpikia misosi akiwa na hofu ya kuwekewa sumu.
 
Hizo sifa na sidhan kama mijitu mingine ina akili timamu,hawahawa ndo walizusha uongo kuwa maswi alikuwepo airport kumpokea kikwete wakati jamaa alikuwepo Dodoma.
 
Hii ni kweli kabisa. Kama Kigoma Malima aliuliwa London UK unadhani watashindwa kumuua Zitto Dodoma? Halafu siku hizi wana viyu vya kukuondoa after 2months....taratibu
 
Hizo sifa na sidhan kama mijitu mingine ina akili timamu,hawahawa ndo walizusha uongo kuwa maswi alikuwepo airport kumpokea kikwete wakati jamaa alikuwepo Dodoma.
unanionea bure,magazeti yameripoti.kama ni udaku hama uzi tuachie sisi "wadaku"
 
Ngoja nimtafute mke wa Maswi nimuahidi kumsaidia mume wake asijuzulu.
 
Ache ujinga wake mke wa maswi alikutana naye wapi hili jamaa jinga kweli lonakula rushwa halafu kazi kujipapatua tu.
 
Hoja na maneno ya wanasiasa wetu kama haya ni kutafuta sifa na hongera za kitoto!.

Kwa hiyo Mhe. Zitto anataka kutuambia baada ya kusoma maazimio ya PAC, hata wasiwasi wa kuuwawa umeisha.

Kwani yeye kama angeuwawa, hata maazimio ya PAC yangeuwawa wakati Kamati ya PAC ilikuwa na wajumbe zaidi ya 18?

Nilishangaa sana kuwasikia eti wanasema hawakulala kwa sababu walikuwa wanalinda repoti isiibiwe. Really?

Hizi ndizo fikra na mitazamo ya kudhani bila mimi hakuna mwingine anayeweza!

Wao wameishatimiza wajibu wao kama PAC, haya mengine ni kutafuta sifa kwa nguvu.

Politics is perhaps the only profession for which no preparation is thought necessary-Robert Louis Stevenson
 
Ache ujinga wake mke wa maswi alikutana naye wapi hili jamaa jinga kweli lonakula rushwa halafu kazi kujipapatua tu.

Nadhani ni Mbunge wa CCM huyu, na hizo ndio tabia zenu pambanuzi
 
Mambo nyuma ya pazia yameanza kufichuka.Deo mjumbe wa PAC ameeleza jinsi mke wa Maswi alivyomwangukia kumtetea mumewe Eliakim Maswi.Pamoja na ujeuri wa mumewe lakini mama huyu alimwangukia makamu asimwanike.Deo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa alipokuwa akisoma maoni ya kumwajibisha waziri mkuu,alimsikia PM Pinda akishusha pumzi nzito sana.Aidha Zito naye amebainisha kuwa alilazimika kumuita dada yake Dodoma kumpikia misosi akiwa na hofu ya kuwekewa sumu.
Filikunjombe nae anaanza kudata.
 
Hii ni kweli kabisa. Kama Kigoma Malima aliuliwa London UK unadhani watashindwa kumuua Zitto Dodoma? Halafu siku hizi wana viyu vya kukuondoa after 2months....taratibu
Mkuu umesimuliwa wapi kuwa Kighoma malima aliuliwa?
 
Akina Deo wanaa za kuchemsha sasa kwa kauli za namna hii
 
Hawa wasanii wa PAC isingekuwa UKAWA kuwa against ma CCM no matter what,wangehadhirika vibaya sana.

Report yao ilikuwa na mapungufu makubwa sana,hakuna la maana waliloongezea kwenye report ya CAG.

Walishindwa kumuhoji CAG ili kupata OBJECTIVE OPINION kama pesa ni za serikali au la,sielewi kazi ngumu wanayosema walifanya ni ipi?
 
unanionea bure,magazeti yameripoti.kama ni udaku hama uzi tuachie sisi "wadaku"

ha ha ha haaaaaa! duh jibu lako mujarabu kabisa. Hakuna la ajabu ktk hilo, tulitegemea haya yangetokea. Usishangae hadi zimetolewa! huh
 
Ache ujinga wake mke wa maswi alikutana naye wapi hili jamaa jinga kweli lonakula rushwa halafu kazi kujipapatua tu.

Weka evidence mezani tupime kama ni kweli filikunjombe alikula rushwa au laa.
Otherwise nakukumbusha kuwa humu tunaongea kwa facts na evidence hatujadili kwa hisia, tunazingatia truth and reality.
 
Back
Top Bottom