FT: Simba SC Vs Yanga SC (0-1)| Simba yashindwa kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu uwanja wa Benjamin Mkapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Naaaam..!

Hujambo na Karibu kwenye Matangazo ya Habari za Michezo, Burudani na Uchambuzi.

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Jumamosi ya July 3, 2021, ambapo mchezo unaobeba hisia za mashabiki wengi Tanzania na nje ya Tanzania kati ya Watani wa Jadi, Kariakoo Derby, Simba SC dhidi ya Yanga SC. kukabiliana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba SC na Yanga SC ni Derby bora Afrika pamoja na zile za Orlando Pirates Vs Kaizer Chiefs, Ahly Vs Zamalek, Raja Vs Wydad, Club African Vs Esperance Tunis.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote ambapo Simba SC wakiwa katika nyakati bora kabisa huku Yanga SC wakipata matokeo mazuri mfululizo.

Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, amesema kuwa mchezo utakuwa mgumu kutokana na Timu ambayo wanakutana nayo lakini lazima washinde kwa sababu wanahitaji ubingwa.

"Nia yetu ni kutetea vikombe vyetu vyote, tunajua siku zote mechi ya Derby si rahisi na sisi kwa kutambua ugumu wake tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi". Amesema Matola.

Kocha wa magolikipa Razack Siwa, amesema kuwa wamejianda vizuri kupata ushindi mchezo wa leo

Tumejiandaa vizuri sana juu ya mchezo wa huu na hakuna asiyejua ukubwa wa Derby hii kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi, kwahivyo tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi". Amesema Siwa.

Endapo Simba SC watashinda mchezo huu, watakuwa Mabingwa wa Nchi kwa msimu huu wa 2020/21 kwa mara ya Nne mfululizo.Yote kwa yote dakika 90 za jasho na damu kuamua kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kumbuka mchezo huu ni kuanzia saa 11:00 Jioni. Usikose Ukasimuliwa

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.

..... Ghazwat na Crew Mzima ya JF Karibu....


===========

Naaaam..Tukiwa tunahesabu masaa kadhaa kuelekea kwenye mchezo wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga.

Mashabiki na wadau mbalimbali wanazidi kujitokeza kwa wingi, wengine wakiwa ndani na nje kwenye foleni ya kuingia Uwanja wa Mkapa, huku kukiwa na tambo kwa pande zote mbili, ngoja tusubiri kuona inakuwaje..!

Vikosi vya timu zote tayari vimefika Uwanja wa Mkapa tayari kabisa kwa mtanange huu hapo saa 11: 00 Jioni.

Kikosi cha Simba SC;

Manula, Kapombe, Hussein, Onyango, Wawa, Lwanga, Morrison, Nyoni, Chama, Bocco Miquissone.

Akiba;

Kakolanya, Kennedy, Mzamir, Bwalya, Dilunga, Kagere, Mugalu.

Kikosi cha Yanga SC;

Shikalo, Kibwana, Adeyum, Job, Mwamnyeto, Mukoko, Mauya, Tusila, Kaseke, Feisal, Yacuoba.

Akina;
Kabwili, Paul, Said, Farid, Ntibazonkiza, Nchimbi, Fiston.

Timu zipo uwanjani zikipasha misuli ili kujiweka sawa kimwili na kiakili.

00' Naaaam mpira umeanza Uwanja wa Mkapa. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amefika Dimbani

Vodacom Premier League VPL | Simba SC 0-0 Yanga SC


02' Yanga wanapata Kona mbili ambazo haikuzaa matunda huku umiliki wa mpira ukiwa upande wa Yanga SC.

05' Kipute kinaendelea kwa kila timu kusaka ushindi huku kukiwa hakuna bao | Simba SC 0-0 Yanga SC.

12' Mauyaaa Goooooooooaaal Goooooooaaal

Mpira ulipigwa kwa mbali na Zawadi Mauya unambabatiza Kapombe na kumpoteza maboya golikipa Manula na kutinga wavuni | Simba SC 0-1 Yanga SC.

17' Shambulizi la kwanza kali limefanywa na Simba SC lango la Yanga, Hussein anakosa nafasi ya kufunga.

20' Umiliki uko upande wa Simba sasa wakijaribu kutafuta bao la kusawazisha huku Adeyum akionyeshwa Kadi ya Njano baada kumchezea Madhambi Kapombe ni faulo kuelekea Yanga.

25' Mpambano ni mkali, huku kila timu ikitumia maarifa na umakini zaidi uwanjani | Simba SC 0-1 Yanga SC

28' Yanga wanapata Kona ya sita huku Simba wakipata kona moja lakini zote haikuzaa matunda, Kibwana yupo chini baada ya kupata rabsha.

35' Shambulizi kali watafanya Simba kupitia John Bocco, lakini shuti lake linadakwa na Shikalo, ilikuwa kazi nzuri ya Chama.

40' Mpira unaendelea huku Simba wakisaka bao na Yanga wakitaka kuongeza bao, Shambulizi la Morrison linashindwa kuzaa matunda | Simba SC 0-1 Yanga SC.

45+3' Kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa Mkapa ambapo Yanga wapo mbele kwa bao moja kwa bila dhidi ya Simba huku kukiwa na tafarani za hapa na pale.

Naaaam mpira ni mapumziko | Simba SC 0-1 Yanga SC

VPL, HT: Simba SC 1-0 Yanga SC

Kipindi cha pili kimeanza huku Simba wakifanya mabadiliko. Ametoa Nyoni na ameingia Bwalya na upande wa Yanga hakuna mabadiliko.

Mpira umebadilika sasa mashambulizi kadhaa kwa kila pande huku Simba wakikosa nafasi ya kufunga kupitia Bocco pamoja na Yanga pia.

52' Simba wanatakata sasa kwake Kapombe, Morrison anapigaaaa looo anakosa nafasi ya kufunga ilikuwa hatari sana lango la Yanga.

56' Mukoko anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kupoteza muda | Simba SC 0-1 Yanga.

60' Free Kick iliyopigwa na Miquissone inagonga ukuta wa Yanga na mpira kuokolewa huku Yanga wakifanya mabadiliko ametoka Kaseke ameingia Nchimbi.

70' Miquissone anapiga shutiiiiii kali lakini linapaa nje ya lango. Simba wanafanya mabadiliko ametoka Chama na ameingia Kagere.

78' Shikalo anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kupoteza muda | Simba SC 0-1 Yanga SC

Bocco anaruka kichwa ndani ya six lakini mpira unaokolewa. Kipindi cha pili umiliki wa mpira ni upande wa Simba SC

80' Kope Mutshimba Mugalu anaingia kuchukua nafasi ya Lwanga Simba wanaongeza mashambulizi

Ametoa Feisal na ameingia Juma Makapu upande wa Yanga SC huku mashabiki wa Yanga wakiinuka kwa shangwe.

Kagere anakosa nafasi ya kufunga bao kusawazisha kwa shutiiiiii lake kutoka nje.. Ametoka Tuisila na ameingia Ntibazonkiza upande wa Yanga.

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Simba wakisaka bao kwa udi na uvumba lakini kwa dakika hizi sidhani Japo mpira ni dakika 90.

Kona kuelekea Yanga, huenda ukawa mpira wa mwisho kwenye mchezo huu.

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Yanga wanaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Simba

FT VPL; Simba SC 0-1 Yanga SC

... Ghazwat......
 
Mikia wameshanasa kwenye Camera 📷
ae18a54cfb4845babdf2ce249d6a1b68.jpg
 
Back
Top Bottom