FT: Dodoma Jiji 0-2 Yanga | Ligi kuu NBC | Liti

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,830
Baada ya vibe la kombe la dunia huku Argentina akiwa haamini macho yake, ligi kuu Tanzania Bara leo inarejea. Kuwa nami nikujuze yanayojiri kutoka kwenye dimba la Liti mkoani Singida.

Dodoma Jiji wamejigamba leo wanaenda kuuvunja mwiko na hamna mtu atasimama dakika ya 46 kushangilia unbeaten, Wataweza?

Dodoma Jiji VS Yanga

========

00' Shughuli imeanza dimba la CCM Liti

08' Moloko anaingiza mpira kati lakini mlinda mlango wa Dodoma anasimama imara

18' Kibwana Shomari anaachia mkwaju mkali kutoka nje ya 18, unapaa juuuu

19' Moloko anawekwa chini, Yanga wanashindwa kutumia vizuri mpira wa adhabu ndogo

23' Kisinda anaipangua beki ya Dodoma na kuachia mkwaju, mlinda mlango anaiakamata barabara

25' Mayele anaingia ndani ya 18, anapiga lakini mlinda mlango anasimama imara na kuudaka

41' ⚽ Fistooon Mayele, anamalizia pasi maridadi kutoka kwa Tuisila Kisinda. Wachezaji wanatetema hapa dimba la Liti

67' Mayele anaweka goli la pili

90+3' Mpira unatamatika dimba la Liti

Yanga inarejea kileleni na kuendeleza rekodi yake ya kitofungwa.
 
Anthony Mvunde mla mihogo lialia ameshatoa maelekezo kwa vijana wake kama Mzee wa tozo alivyotoa maelekezo majuzi.
 
Back
Top Bottom