Front Page ya Gazeti la Uwazi

Front Page ya Gazeti la Uwazi

sijalisoma gazeti lakini nahofia wakaongea kitu tofauti na kichwa cha habari.hope kama ni tofauti basi nao ni uhalifu kama uhalifu mwingine
 
Katika free country huwa hawafungii magazeti.
Kama unaona gazeti limeandika sio facts,nenda mahakamani ku li sue.
 
anacheza na vitu vya vatican huyu mwandishi anadhani pengo ni kikwete?
haya ngoja tusubiri
 
Kanisa katoliki act
immediately, huu ni udhalilishaji wa hali ya juu sana. Kwa hakika nchi
iko pabaya kila mtu anakifanyia analotaka. Fungueni kesi ya madai. It is
too much of this!!

Hapana,Tuandamane bwanaaa!
 
Inasikitisha sana kuona Tanzania Daima nalo limejiunga kwenye magazeti ya UDAKU.
Lakini unalipenda sana....tuki search hapa umetaja Tanzania Daima mara ngapi kwenye uandishi wako tutakuta umeandika mara 100K plus!
 
Binafsi huwa siyafatilii sana magazeti ya Global Publisher. Hivi kuna mwandishi wa habari kutoka Global publisher aliyepata Zawadi kwenye Tamasha la juzijuzi la waandishi wa habari?
 
Hapana,Tuandamane bwanaaa!

Wakatoliki na jamii ya Wakristu huwa ni watu wa amani. Ingekuwa ni wenzetu wameandikwa ungekuta Shigongo leo anachomewa nyumba. Katoliki ni dhehebu la viongozi wa wasomi wanaofuata kanunu na sheria za kanisa na za nchi husika.
 
SHIGONGO NI S**** NAkuna jamaa kapangiwa nae nyumba mitaa ya kati pale
mpigaji mlokole mwongo mpenda starehe za hovyo kabisa
 
Kinachoendelea ni simple, wanaona watanzania kama mizuzu. Wameanza Rwakatale kwa Video editing software tukanyamaza. Sasa wameona kila mtu ni mpuuzi. Lkn, viongozi wa dini wajue ubaya wa CCM kwa watanzania.
 
Inasikitisha sana kuona Tanzania Daima nalo limejiunga kwenye magazeti ya UDAKU.

ZeMarcopolo, Tanzania Daima ni gazeti la Watanzania wenye mapenzi meme na nchi hii. Uliza kwa wauza magazeti Gazeti halina return hata kidogo. Kuwa Objective mkuu.
 
ZeMarcopolo, Tanzania Daima ni gazeti la Watanzania wenye mapenzi meme na nchi hii. Uliza kwa wauza magazeti Gazeti halina return hata kidogo. Kuwa Objective mkuu.

Magazeti ya UDAKU siku zote yanaongoza kwa mauzo.
 
View attachment 89617


Kwa aina hii ya uandishi tunaelekea kubaya!

Tatizo ni kubwa.Watu wanajiandikia tu.Ila ukweli hawa wana njaa.Wananunuliwa na watu fulani. Wanataka watu waache mambo ya msingi ya kufanya na kushughulikia kama kueneza neno la Mungu na kusimamia kanisa.Nadhani unanielewa.Kwanza kwa akili tu ya kawaida habari nzito kama hii haiwezi kutoka kwenye magazeti haya uchwara. Na pili hushughulikiwa na vyombo husika sisi tukaona matokeo tu.
 
mkuu kama umelisoma hebu tupe brief ya kilicho andikwa!

UWAZI LABAINI SIRI NZITO ILIYOTAWALA KWA MWAKA MZIMA, LAPEKUA ORODHA YA VIGOGO VINARA WA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA
Na Mwandishi Wetu
SKENDO kwamba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, anafanya biashara ya madawa ya kulevya, ilitikisa kisha ikapoa, ila sasa Uwazi lipo kwenye nafasi nzuri ya kupasua jipu.
Januari mwaka jana, Pengo ndiye alikuwa wa kwanza kutamka hadharani kuwa anaambiwa anauza ‘unga’, kipindi hichohicho, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ambaye alisema wanafanya kazi kisayansi.
“Kama jina la Pengo tunalo kwamba anauza madawa ya kulevya au hatuna, siwezi kutamka kwa sasa, hatutaki kupindisha ushahidi au kuvuruga upelelezi wetu,” alisema Nzowa.
Hata hivyo, hivi karibuni, Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa vigogo wa jeshi la polisi nchini, aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, akasema kuwa suala la Pengo lina utata ila siyo zito.
“Labda mimi nipasue jipu kwamba jina la Pengo halionekani katika orodha ya viongozi wa dini wanaochunguzwa kutokana na kashfa ya madawa ya kulevya,” alisema kigogo huyo.
Aliongeza: “Hata kwenye ule mkanda uliokwenda bungeni, ukionesha wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, Pengo haonekani. Tulishangaa sana aliposema anaambiwa anauza madawa ya kulevya.”...
 
View attachment 89617


Kwa aina hii ya uandishi tunaelekea kubaya!

Shigongo anatumwa na wale wale walioitwa tumaini la Mungu aibu tupu, haina tofauti na video ya Nchemba kwa Lwakatare na Chadema, vitisho na mauaji ya viongozi wa dini si bahati mbaya ni mipango ya watu waliofilisika kisiasa. Kwanini watu wanazushiwa tu wanapotofautiana na wanasiasa au watawala? Watanzania tuamke maana wanasiasa na watu waliofilisika kifikra wana tuharibia nchi yetu. Pole sana Baba Pengo.
 
UWAZI LABAINI SIRI NZITO ILIYOTAWALA KWA MWAKA MZIMA, LAPEKUA ORODHA YA VIGOGO VINARA WA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA
"Labda mimi nipasue jipu kwamba jina la Pengo halionekani katika orodha ya viongozi wa dini wanaochunguzwa kutokana na kashfa ya madawa ya kulevya," alisema kigogo huyo.
Aliongeza: "Hata kwenye ule mkanda uliokwenda bungeni, ukionesha wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, Pengo haonekani. Tulishangaa sana aliposema anaambiwa anauza madawa ya kulevya."...
hawa waandishi bwana!!sasa wanaosoma vichwa vya habari na kutengeneza habari wenyewe si wamepotea!
 
Tumbo huwenza kumfanya mtu akawa kama punguani. Na huyo ndio E J Shigongo. Akili kaweka mfukoni.
 
Back
Top Bottom