Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,034
- 132,807
Sisi wengine tupo mbali hivyo hakuna aliyeko Pemba angalau akatupa ya huko?
Shalom, ukishaanzisha thread hapa JF, inakuwa ni ya wote, hakuna thread ya mtu, hivyo mwache MS naye atupe yale ya upande wake.Asante Pasco tupe habari. Malaria sugu acha kumwalibia pasco thread yake, huwa tukishakuona wewe kila kitu kinaonekana kama mzaha hivi
Na jee kuna mawakala wa vyama katika vituo vya kura??
Mshirazi, hali ni ya utulivu wa hali ya juu, Wilaya ya Kaskazini Unguja huku kwa Shamhuna ndiko nilikobahatika kupita hapa na pale. Hili nin eneo la manazi wa CCM, sikuamini niliposhuhudia kura za hapana nyingi kuliko za ndio.Pasco binafsi ningependa zaidi kusikia habari za maeneo ya kaskazini Unguja,,,hasa hasa Donge,, Mkwajuni na Chaani,,hali halisi ikoje huko??
Mshirazi, hali ni ya utulivu wa hali ya juu, Wilaya ya Kaskazini Unguja huku kwa Shamhuna ndiko nilikobahatika kupita hapa na pale. Hili nin eneo la manazi wa CCM, sikuamini niliposhuhudia kura za hapana nyingi kuliko za ndio.
Nimekubali kweli Wanzanzibari ni kiboko! yaani watu wa misimamo isiyoyumba, siamini baada ya kampeni yote ya Karume kuhamasisha kura ya Ndio, bado kuna majimbo yamepiga kura ya Hapana!.
Kibunango, ni kweli kuna uwezekano huu utulivu pia umechangiwa na uchache wa waliojitokeza, lakini pia ukumbuke huu ni uchaguzi usio na ushindani, wana CCM hawakujitokeza kwa wingi kutokana na kukatishwa tamaa na muafaka.Pasco, utulivu ulio kutana nao hautokani wapiga kura kujitokeza kwa uchache? nafikili kuna jumla ya watu laki nne waliojiandikisha kupiga kura leo. Je hawa wote wametimiza lengo la kipiga kura?