From Goatherd to Governor, Edwin Mtei's Autobiography

Ndipo wanapotushinda viongozi wa nchi nyingine,,,, Mtei kaonyesha njia ..na hata abudl jumbe mwinyi nafikiri anacho kitabu pamoja na kuwa sio autobiograph..but at least...tunataka watu kama ali hassan Mwinyi, Salim, Mkapa, Mrema, Warioba, Sumaye, Cleopa, Kawawa[kile alichoandikiwa hakiendani na hadhi yake...],... watu kama Hashim Mbita na historia za ukombozi...wote hawa wanahitaji kuachia watanzania uridhi wa vitabu...

Nampongeza mzee Walter Bgoya ..huyu hata mwalimu alikuwa akimtumia ...nafikri yeye na baadhi ya marafiki wa mwalimu walikuwa na mradi wa kuandika auto ya mwalimu na walishaaza kuandaa...nadhani ni bora kwakuwa mama Maria bado yupo watoto... na marafiki zake wapo... wamalizie ule mradi na kutoa kitabu... tena bahati mbaya juzi mmoja wa watu waliokuwa kwenye mradi wa auto ya mwalimu Haroub Othman kafariki...sasa ni vema waliobaki wamalizie kile kitabu ,,,ilikuwaa ndoto ya muda mrefu ya mwalimu kuwa akifa kitoke,,..
 
Huyu mzee hakuwa gavana kwa merit bali alibebwa na nyerere ndio maana uchumi ukafa.kwenye hicho kitabu kaeleza alivymzuia zitto kabwe ili mwanawe awe mwenyekiti?

Ni kitabu cha kikabila zaidi kuliko utanzania.ndio maana mengi amepewa nafasi kubwa.huyu mzee anatapata tu

unajua juzi nilisikia kua zaidi ya asilimia 4 ya Watanzania ni vichaa bila wao au jamii zao kujua, ila ukiwa makini na matendo na kuangalia vikra zao utagundua viwango vyao vya wehu na ukichaa.
 
Kweli kabisa ndugu yangu wala usikisogelee maana hata lugha iliyotumika hutaielewa. Kisije kikakupunguzia upumbavu uliokujaa.
 
Huyu mzee hakuwa gavana kwa merit bali alibebwa na nyerere ndio maana uchumi ukafa.kwenye hicho kitabu kaeleza alivymzuia zitto kabwe ili mwanawe awe mwenyekiti?

Ni kitabu cha kikabila zaidi kuliko utanzania.ndio maana mengi amepewa nafasi kubwa.huyu mzee anatapata tu
hata kama alibebwa au laah hii ni historia ya maisha yake, sikitabu cha siasa tu.
Sasa kujua kama aliyaelezea hayo mambo ya Zito sijui , hapo ndio pakukisoma hicho kitabu, au ndo ile silika ya Mtanzania kuogopa kujisomea na kusubiri kuhadithiwa.
 
Ku excel zamani au sasa hakuna kipindi iliwahi kuwa rahisi,acha uvivu na visingizio,piga kazi tafuta pesa.

Wapo waliosoma manzese kwa mfuga mbwa na ngeli wanaichapa vizuri tu,tatizo wewe ulikuwa unaona soo kuongea kiingereza kwa kuogopa utakosea na kuchekwa ndiyo maana hujui.

Wabongo tuache haya mambo ya visingizio,elimu hii hii unayoiona mbovu kuna watu wanatoka na wanakamata position nzuri tu na hawajasoma international wala hawajawahi hata kwenda ulaya before kupata elimu "bora".

Kiingereza hata ukiamua serious sasa hivi kujifunza in one year time utakuwa mbali sana. Acha visingizio, komaa utafika tu. Naweza kukupa mifano ya watu waliosoma St. Kanumba na wana position nzuri ambazo wamepata bila upendeleo.

Tatizo letu wabongo tunapenda visingizio wakati uzembe ni wetu wenyewe. Kipindi kile secondary tunavalishwa kibao shingoni ukiongea kiswahili tulikuwa tunaona kama upuuzi. Walimu walikuwa wanajua kiswahili cha kuongea na kiingereza cha kuandika tunajua kiasi,ila walitaka tujue kiingereza cha kuongea pia ambacho tunakijua kwa practice.

kaka unathibitisha ulivyo mbinafsi na roho mbaya, nyie ndiyo mkipewa uongozi wa nchi mnaeleza uliyoyasema.Mimi nimetoa hali halisi ya maisha ya sasa, unasema wajisomee, how they can buy a book, wakati hawana hela?

Niliyeandika hapo ni lecturer mlimani, siyo kuwa lugha inanishinda, mpaka hapa niko matawi ya juu.Ila napata homa, nikiona watoto wetu wanauza maandazi masaa ya shule, wanaenda shule hamna walimu, who can tell them that English is essential?

Kuna watoto wanaenda shule hawajui hata umuhimu wa shule!

Mkuu, ulikurupuka kujibu kutokana na pendo lako la dhati kwa mtei, mwenzako nimeeleza hali halisi, undeniable truth.Hata mtoto wako huwezi ukamwambia hivyo mkuu, unamtayarishia njia na mazingira, hata hao waliosoma zamani, bado wazazi wao walikuw na uwezo, usifikiri mtu kama Mengi ni familia ya kimaskini

duh! umenishtua kwa roho yako mbaya, ya choyo, isiyo na aibu wala chembechembe za kunusa ukweli wala kuangalia hali halisi, au ndiyo wewe chongo huita kengeza?

Bila aibu unasema kipindi kile mlikuwa mnavalishwa vibao, siku hizi je?? hivi umempenda sana Mtei mpaka ukose kuona hali halisi,Mtei nani yako wewe? unatutisha!!

Mtei alikuwa na sifa gani kuwa gavana wa benki?
 
Waasisi wengine wafuate mfano huu.wa Mzee Edwin Mtei,tusije danganywa bure na wapenda sifa.
 
Huyu mzee hakuwa gavana kwa merit bali alibebwa na nyerere.....

Mtei alikuwa na sifa gani kuwa gavana wa benki?

Haya maswali wangefaa waulizwe magavana wa Afrika (African Caucus) wa mwaka 1979 waliomchagua Mtei kuwa Chairman of board of governors of IMF and World Bank for the 1979/80 fiscal year. Hamna gavana Mtanzania amewahi kuchaguliwa kushika hii nafasi tena!

Hongera sena Mzee Mtei mambo uliyoyapigania kimataifa wakati huo miaka ya sabini ukiwa gavana matunda yake tunayafaidi leo.

.
 
Tuondoe fikra za ukabila maana tukianza kuulizana kila marafiki tulio nao tutarudi kule kuleee alikosema mwalimu. " ukabila ni dhambi kubwa sawa na kula nyama ya mtu ukishaianza huwezi kuiacha". Hawa alio waita ni marafiki zake na haikatazwi mtu kuwa na rafiki toka kabila analotoka. Hapo Kaduma si Mchaga, wala Ulimwengu. Mbowe ni Mkwewe( Mkaza mwanae) sawa na mwanae Lilian. Kunaubaya gani kuwaalika kwenye uzinduzi wa kazi hii kubwa?

Mzee ametoa mchango mkubwa sana kwa taifa na lazima tuuheshimu. Nimiongoni ya wachache waliokua na uwezo na uthubutu wa kumwambia mwalimu hapa umekosea na ndo mana hawakuweza kudumu pamoja. Alikua na merits za kuwa gavana na hata waziri mana alikua miongoni mwa wasomi wachache wa kwanza wa Tanganyika huru. 1960 BA nchini hazikufika mia ulitaka nani apewe ugavana wakati hapakua na wasomi?

Nivyema tusome tujifunze ni kazi kubwa an nzuri kwa wakati wao na tuiboreshe misingi hiyo kwa kuzingatia hali halisi ya sasa.

Wakuu nani mwenye taarifa tunapoweza kukipata kitabu hiki?
 
Kanda2, mkabila ni wewe na wala si Mtei. Tunapongeza mzee kutoa biography yake. Toa mfano jinsi Mtei alivyobebwa na Nyerere na ni sifa gani aliyokosa kuwa Governor wakati wake huo? Thibitisha pia jinsi alivyoua uchumi. Acha unafiki na chuki binafsi. Jifunze kuwa positive na mafanikio ya wenzio ama kwa juhudi zao.
 
Kitabu kipo kwenye maduka makubwa ya vitabu (kwa Dar sijui huko mikoani) na vilevile mtandaoni.
 
Hongera sana Mzee Mtei kwa kuonyesha njia. Kina Mbowe, Zitto nadhani pia waanze kifikiria kuandika!

Hivi autobiography ya Kingunge itakuwaje? I am just curious!
 
kanda...tutajie mtanzania mmoja au hata east africa amabaye alikuwa na qualifications walizo nazo wasomi wa sasa ...mtu mwenye akili timamu atajuwa kuwa kadri miaka inavyokwenda ..ushindani wa kielimu kwenye kazi unazidi....

kuna mzee wangu mmoja alikuwa ni standard 12 ya mkoloni ...alikuwa regional manager wa taasisi moja nyeti sana na kwa mafanikio makubwa ...alipostaafu kijana aliyequalify kuchukua nafasi yake baada ya ushindani alipita mwenye Bcom.,postg.finance,MBA....NA still hajafikia mafanikio ya mtangulizi wake...sijui siku hizi tumekuwa na elimu lakini tunakosa UZALENDO.....

LEO hiii pale BOT ukimpa mtu ambaye hana ,,PhD watakushangaa...kwani phd holders ni wengi mnu pale...kuacha mmoja tu ambaye imebidi apewe ana ADVANCE DIPLOMA,mba...Kwa ajili ya kuwakilisha upande mmoja wa muungano ....baada ya candidate mwenye PHD Upande huo kuonekana ni mPEMBA....Wakuu wa huko wakatuletea jina lake....

mmeona juzi tumepata mwanasheria mkuu mwenye degree zaidi ya tatu...but miaka ya sabini na 80"s ..AG walikuwa just LLB"S...

So mtu anayeweza kuhoji uwezo wa MTEI kwa enzi zake na mafanikio aliyofikia .....anakosa uwezo wakufikiri jambo kwa wakati..
 
..Mtei hakuwa na hizo BCom au BEcon lakini naweza kusema alipopewa hizo nafasi alijifunza na aliwatumia wataalamu waliomzunguka. sasa huo ndiyo UONGOZI.

..kuwathibitishia kwamba ni mtu mwenye kujifunza ndiyo maana akayamudu vizuri madaraka yake kama Gavana, Waziri wa Fedha, na hata Executive Director wa International Monetary Fund.

..miaka 4 baada ya kuwa amemfukuza kazi Mtei, Mwalimu Nyerere alikuja kubadili msimamo na kufuata mambo yaleyale aliyoshauriwa na Mtei na akayakataa.

..nampongeza Mzee Mtei kwa kuandika kuhusu maisha yake na utumishi wake serikalini. huu ni mwanzo mzuri ambao ungefaa kufuatwa na wengine.

NB:

..kinachosikitisha sana nchi hii ni kwamba wale ambao walikuwa the most qualified na wakapewa nafasi za kutumikia kwa makusudi kabisa wamehujumu nchi hii na kututia kwenye matatizo makubwa.

..hebu angalia utendaji wa Dr.Daudi Balali, Dr.Kighoma Malima, na Dr.Idris Rashidi.
 
Namkumbuka huyo Mr Walter Bgoya alimsaidia sana ndugu yangu alikuwa anataka kutoa kitabu chake,watu wa kazi yake wapo wachache sana Dar maana unaweza kutafuta mji mzima usipate sijui kwanini?
 
..actually Mzee Mtei amelizungumzia hili suala la yeye kupewa madaraka makubwa akiwa bado kijana mdogo tu.

..kuna mahali Mtei amesema hivi: " During that time, vacancies applied for candidates, rather than candidates applying to fill vacant posts."

..kuna wazee wengi sana walikwaa posting nzito-nzito wakati wa zoezi la Mwalimu Nyerere la AFRICANIZATION. zoezi hili lilihusisha Waafrika kuchukua nafasi za kiuongozi na kiutawala toka kwa Waingereza.
 
Huyu mzee hakuwa gavana kwa merit bali alibebwa na nyerere ndio maana uchumi ukafa.kwenye hicho kitabu kaeleza alivymzuia zitto kabwe ili mwanawe awe mwenyekiti?

Ni kitabu cha kikabila zaidi kuliko utanzania.ndio maana mengi amepewa nafasi kubwa.huyu mzee anatapata tu

Ama kweli majina yanashabihi watu walivyo. Kweli ni "Kanda mbili"
 
Huyu mzee hakuwa gavana kwa merit bali alibebwa na nyerere ndio maana uchumi ukafa.kwenye hicho kitabu kaeleza alivymzuia zitto kabwe ili mwanawe awe mwenyekiti?

Ni kitabu cha kikabila zaidi kuliko utanzania.ndio maana mengi amepewa nafasi kubwa.huyu mzee anatapata tu
Acha chuki binafsi..andika chako basi tujue wewe umelifanyia nini taifa!
 
..actually Mzee Mtei amelizungumzia hili suala la yeye kupewa madaraka makubwa akiwa bado kijana mdogo tu.

..kuna mahali Mtei amesema hivi: " During that time, vacancies applied for candidates, rather than candidates applying to fill vacant posts."

..kuna wazee wengi sana walikwaa posting nzito-nzito wakati wa zoezi la Mwalimu Nyerere la AFRICANIZATION. zoezi hili lilihusisha Waafrika kuchukua nafasi za kiuongozi na kiutawala toka kwa Waingereza.

Jokakuu:

Hao wazee ndio waliojenga misingi mibovu. Short cut ya Africanization imeharibu kila kitu.
 
[/COLOR][/SIZE]

unajua juzi nilisikia kua zaidi ya asilimia 4 ya Watanzania ni vichaa bila wao au jamii zao kujua, ila ukiwa makini na matendo na kuangalia vikra zao utagundua viwango vyao vya wehu na ukichaa.

Mkuu hapa umefanya kuniwahi tu nilishataka kushuka na hoja hii hii dhidi ya juha huyu!
 
Hongera mzee Mtei kwa kuandika , viongozi wengine waige mfano huu wa kutueleza yaliyopita ambayo ni vigumu kuyapata kwa vizazi vijavyo... alikuwa na msimamo baada ya kutofautiana na JK kwenye masuala ya uchumi na kujiuzulu kwenye serikali miaka hiyo ya nyuma, aliyomshauri JK baadaye walikuja yachukua.... ,viongozi wengine hawana courage ya hata kukosoa kitu chochote bali ni watu wa YES man ...

Big up Mzee Mtei ...
 
Back
Top Bottom