From analog to digital | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

From analog to digital

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by anania, Jul 20, 2010.

 1. anania

  anania Member

  #1
  Jul 20, 2010
  Joined: Jul 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimesikia kuwa Tanzania ilijiwekea mkakati ku kumaliza utaratibu wakumaliza kuhamsha urushaji wa matangazo kutoka analog kwenda digital ifikapo 2012 badala ya 2015.TBC ni mojawapo ya makampuni matatu yaliyopewa jukumu hilo na wameshaanza kwa mgongo wa selikari,na kampini nyingine nimesikia ni AGAPE na nimeskia kuwa wameshaanza kutoa huduma.Kama kuna mwenye kujua zaidi kuhusu AGAPE na hiyo kampuni nyingine iliyo bakia naomba kujua zaidi.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,171
  Trophy Points: 280
  Hiyo Agape ni ya wapi?
   
 3. D

  Dick JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Agape ndiyo ATN ya Venon Fernandes iliyopo Mbezi beach kituo cha jogoo, ni ya kidini (kilokole).
   
 4. minda

  minda JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  suala la msingi hapa siyo kujua agape au startimes; kama kuna mtu anaweza kutoa kwa lugha ya kawaida maelezo ya mabadiliko hayo kutoka analogue kwenda digital ingekuwa vizuri zaidi.
   
 5. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hii kampuni ya Agape wanajiita TING, ni kweli tayari wako hewani. Nilipotembelea SABASABA nilipata bahati ya kutembelea banda lao na wakanipa kipeperushi. Gharama ya decoder yao ni 100,000/=, ila charge yao kwa mwezi ni 7,500/=. Uzuri wao wanarusha karibu channel zote za Bongo zinazopatikana hapa mjini (Dar), na sehemu ya channel zinazopatikana Star times.
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Mkuu naomba ufafanuzi kidogo hapo. Unaposema 'karibu channel zote za Bongo zinazopatikana hapa Bongo' Ina maanisha nini? kwamba nikinunua hiyo nitapata DTV, Channel 10, ITV, TBC, Star TV, EATV na kadhalika? Kwamba kwa Decorder moja unaweza kupata channel zote hizo tofauti na hawa wamiliki wa vituo vua TV wanaotaka kila mtu awe na decorder yake? mwenye uzoefu na Ting atuhabarishe tafadhali.
   
 7. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kwenye package ya TING kuna hizi zote, ikiwa pamoja na STAR, MLIMANI, TUMAINI n.k
   
 8. M

  Marwam Member

  #8
  Sep 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Vipi coverage ya hizi decorder za TING ikoje?, Maana hawa startimes hawafiki nchi nzima pamoja na matangazo ya kujinadi mengi.Mnaojua tafadhali nifahamisheni,mimi niko Tanga!
   
 9. bhageshi

  bhageshi JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 264
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli hii teknolojia ya digital binafsi imeniacha njia panda sana maana nitanunua ving'amuzi vingapi? kila TV station inachagua kampuni ya kuingia nayo mkataba wapi wapitishie matangazo yao. Startimes, TING, DsTV na nyinginezo na kila king'amuzi utakuta lazima kuna channel ambayo unaipenda na hapatikani katika king'amuzi kingine. Nafikiri kuna haja tume husika kutoa kipaumbele kwa TV stations za bongo kupatikana katika ving'amuzi vyote
   
 10. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hapa umelonga mheshimiwa, nimekugongea thanks.
   
 11. Mchana

  Mchana Senior Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 181
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mku tafadhali tunaomba utuwekee kipeperushi au nambari za simu za kuwasiliana na hawa wahusika ili tuipate hiyo TING
   
 12. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ting ina local channel nyingi kuliko startimes na ni rahisi na kavareji yake ni kubwa pia
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hivi serikali inaweza kubadili kutoka analog to digital bila ya kutoa taarifa kwa wananchi walau kwa kipindi cha miaka mitatu?

  nimeona wenzetu wa nchi zilizoendelea walipotaka kubadilisha, ilikuwa matangazo kila siku kwenye tv kwa miaka 2 kuwa kutakuwa na mabadiliko. Suala hilo lilijadiliwa bungeni na hadi kukubalika kuwa kwa wale wataoashindwa kubadili tv zao walipiwe hivyo ving'amuzi na serikali za mitaa.

  huko kwetu wanatarajia watu tv zao za analog zitumikeje?
   
 14. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Gaijin,
  Umeuliza shwari zuri, ila pia labda utusaidie kwa nyie mliotangulia kwenye ulimwengu huu wa digital mnapataje matangazo?. Nauliza hivi kwa sababu huku nyumbani digital inaonekana ni kununua dekoda, kitu ambacho hata kinafanya isiwepo tofauti ya tv ya analog au digital. Zote unaangalia kwa kutumia AV cable, hebu tujuze.
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  I think kazi kubwa ya digital broadcasting iko kwenye Transmission. Upande wa TV receiver kama haina inbulit decoder ua kupokea digital casting nadhani zinaweza kununuliwa as separate equipment.
   
 16. Mnwele

  Mnwele Senior Member

  #16
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mi nadhani wadau wote hapo juu mmejaribu kueleza japo very shallow wa namna hii kitu ilivyo.
  Ukifuatilia mjadala utaona ni namna gani watu wangependa kufahaamu hizi concept za Analog na Digital. Kwa tafsiri ya kikwetu ni kama kuondokana na mfumo wa zamani na kuingia mfumo mpya na bora wa kisasa, lakin hapa tabu ya sisi ni about the a,b,c, ya hii move. Nini maana yake, atahri zake and why now??
  Lakini jambo lingine ambalo mdau mwingine kaeleze ni kuhusu uwajibikaji ama nafasi ya TUME ( TCRA ) hawa jamaa wa kusajili chip za simu. Inakuwaje? Mbona hawawaelezi watazania, wanaona gharama hizi?? Ina maana hakuna tena FTA services katika mawasiliano? Umasikin hauwezi kwisha maana ni wachache tu wataweza kupata habari na kujua changamoto za kimaendeleo, TCRA najua wanafahamu kwamba upashanaji wa habari is more of starehe but more important in powerful tool ya kuequip wate kupata taaluma na taaarifa za kimaendeleo--ebu semeni kidogo tujue mpo!
  Nasema hivi kwa sababu..tayari STARTIMES/TBC wanatoza 6,000/mwezi kurun king'amuzi chao, ATN ni 7,500 na wengine waliopata ni hawa joint venture ya ITV na STAR TV ( Bado hatujui itakuwa gharama gani but lets put 6,000) Mtanzania wa kawaida atahitaji kuwa na around 24,000 kupata channel zote anazozihitaji....Hatuwezi kuwa nchi ya namna hivyo. TCRA kazi yenu ninini jamani, nyie si ni kama EWURA and agency/ama mamlaka zingine kama TFDA?? sasa mbona HAMTETEI walaji wa huduma zenu?:A S angry::tape:
   
Loading...