Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
umeona eeehhhh!hahaha, nimeipenda hiyo ya kukimbiana. Lol, unamuona mtu yuko online wakati alikuaga anaenda syria na hatopatikana. Ukimuuliza badae anakuambia sikuona msg. Kukimbiana kubaya sana aisee.
hii iliwahi kutokea kwa marafiki zangu wa karibu sana. Mdada alikuwa rafiki yangu sana....akasafiri....akaja mkaka hapo kwa ofisi akawa rafiki yangu sana. aliporudi mdada nikamtambulisha kwa mkaka basi tukawa marafiki watatu..... wakaanza kupeana hizo benefits bila mimi kujua....watu walikuwa wananiambia lakini mimi nawatetea mno kuwa hawapeani hayo makitu, ni marafiki tu....... siku hizi wananipa wakati mgumu sana, maana hatuwezi kutoka wote watatu.... wanakimbiana ni balaa..... sasa mimi najishangalia tu maana siwezi kuuliza kilichotokea maana na mimi ni mtu mzima.....
Mimi nimejiwekea kautaratibu kangu..... wewe kama ni rafiki yangu basi tutaishia kwenye urafiki.... benefits labda za kununuliana drinks, hugs, kupelekana disco/movies, nikisafiri au birthday/xmas..... kununuliana zawadi baaaaasiiiiiiiiiiiii