Fisadi Lowassa na Urais kwa tiketi ya CCM. Yaani hadi raha, Fisadi anayetaka kupeperusha bendera ya Chama chake!!
Kweli Fisadi Lowassa ndiye 'dume la mbegu' la wanaCCM wote 2015.
...ninavyojua' ndani ya chama tawala ni LOWASSA tu' ndiye anayeweza kuiondoa Tanzania ICU.
...na hizi tuhuma, "mwenye EL alishaga sema ukweli wake" Lowassa alijieleza NEC kama ifuatavyo:
"Lowassa akisema kama ni suala la kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, alitaka kuuvunja mkataba kati ya kampuni hiyo na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) mapema, lakini Rais Kikwete aliyekuwa nje ya nchi alikataa kufanya hivyo na badala yake alimwambia kuwa anasubiri ushauri wa makatibu wakuu wa wizara.
Alisema aliamua kujiuzulu nafasi zake katika serikali ili kulinda heshima ya serikali na chama chake, lakini anashangazwa na hatua ya wanaCCM wenzake na si wapinzani kuzunguka mikoani kumchafua wakidai kuwa yeye ni fisadi.
Lowassa alimkumbusha Mwenyekiti kuwa kumekuwa na utamaduni wa kupikiana majungu ndani ya chama na kukumbushia tukio la yeye (Kikwete) kuzushiwa mengi na Daud Mwakawago wakati wa harakati za kuusaka urais kabla ya 2005.
¡°Mwenyekiti wewe unakumbuka wakati Mwakawago alipokuja na rundo la tuhuma za hisia, isingekuwa busara za Rais Mkapa (Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa), wewe usingekuwa hapo ulipo,¡± chanzo hicho kilimkariri Lowassa akisema.
Vyanzo hivyo vilisema kuwa Lowassa alisema kuwa kama Mungu akipenda mtu awe Rais atakuwa kama alivyotaka tu.
Habari zaidi za ndani ya kikao hicho zilisema kuwa Lowassa alikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa kinachomuuma zaidi ni kutukanwa na viongozi wa chama chake kwa miezi saba kwa kuzunguka nchi nzima kwa fedha za chama, bila hata kumpa fursa ya kujitetea.
Alisema alipokutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, jijini Dar es Salaam alimwambia kuwa kuna watu wamenoa mapanga kummaliza kwa sababu ya urais wa mwaka 2015.
Alimtaja wazi Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuwa amekuwa akiendesha kampeni za kumchafua na kumdhalilisha, wakati akijua wazi hakuna mahali katika maazimio ya kikao cha NEC cha Aprili, mwaka huu juu ya kujivua gamba kwa baadhi ya viongozi wa CCM majina ya watu yalitajwa.
Baada ya kutoa madukuduku hayo alisimama aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, na kuhoji kuwa iwapo itathibitika kuwa Lowassa pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, kuwa si mafisadi kama walivyokuwa wanatuhumiwa ni hatua gani zitachukuliwa.
Akijibu swali hilo, Rais Kikwete alisema kuwa watu hao watashughulikiwa."