Fridge la mtumba v\s la dukani

Wakuu hivi yale mafridge ya mtumba tunayouziwa pale Magomeni traventina na yale ya dukani Kkoo yapi bora hata umeme ukikatika na yapi yanadumu kwa uimara.
Huwa namsikitikia sana mtu anayenunua friji ya mtumba.hivi ni baadhi ya vitu vya mtumba vya kuviacha kabisa.ni hiv hiyo ya mtumba haina gerentii.inaweza waka leo na kesha ikazima na hakuna kwa kuipeleka zaidi ya kwa fundi.pili umeme zinakula sana hizi vitu za mitumba aisee.

Mafriji ya dukani yapo ya bei rahisi na ya kufaa kulingana na ukubwa.so ushauri wangu wewe nunua mpya.utakaa nayo muda mrefu
 
Nashukuru mkuu
 
Samsung wana fridge nzuri mno nilinunua yangu mwaka 2015 mpka leo haijawahi kuharibika chochote kwanza iko na built-in stabilizer.

Mtoa mada nakushauri tafuta fridge mpya iwe ya brand yoyote unayopenda ila iwe non frost..pia ucheki na ulaji wake wa umeme.
 
Hatari nikajua zinatoka viwandani
Mimi mzee wangu alinunuaga friji lakawaida milango miwili kwa sh 300,000tena waliletewa kutoka kiwandani Korea na mwajir wao bila kulipa kod yoyote mwaka 2000, je Sasa hiv uangize friji kutoka kiwandan mpaka bongo kwa kod za Sasa si utalinunua kwa 800000

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu hivi yale mafridge ya mtumba tunayouziwa pale Magomeni traventina na yale ya dukani Kkoo yapi bora hata umeme ukikatika na yapi yanadumu kwa uimara.
Kitu kipya ni kipya ufanisi wake ni asilimia kubwa,kuriko ambacho kimeishstumika,
Imani kwamba Cha nyumba ni bora na original kuriko kipya,ni imani potofu,kwani hakuna kinachokuwa mtumba kabla hakijawa kipya,
 
Nakumbuka enzi za TV chogo nilinunua TV za mtumba mara mbili na zote zikaharibika tena ndani ya muda mfupi tu.

Baadae nikajipinda nikafuata kitu hitachi na boxi lake, sasa ni mwaka wa ishirini na nane unaenda ngoma ipo na inapiga kazi....niliitoa stoo nikawapelekea Mafundi waisafishe wakaanza kunisomesha niwauzie lakini sikuwa tayari.

Kwa hivyo vitu vya mitumba ni risk, bora ujikusanye ufuate kitu kipya dukani
 
Friji jipya linadumu sana,Mimi nilinunua friji aina ya Boss huu mwaka wa 6 hakuna cha fundi wala nini!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ