Freeman Mbowe: Nguzo na mhimili muhimu kwa ustawi wa CHADEMA

Mtoa mada ana hoja ya msingi ....Lakinimuda utafika nalo litapita ......sisi nimfano wa kuigwa katika demokrasia na uongozi wa kutukuka.....kwa hiyo tupunguze hofu.....na tukumbuke siasa ni sayansi
 
Ninaandika hapa jamvini nikiwa na mawazo lukuki juu ya mustakabali wa cdm endapo kamanda Mbowe ataamua kutogombea tena Nafasi ya uenyekiti wa chama taifa.Hakuna mwana jamvi asiyeelewa ni kwa jinsi gani kamanda na mpiganaji Mbowe amekikbeba chama hiki na kufikia hapa kilipo na kutishia kabisa mustakabali wa ccm.Juhudi, maarifa, kujituma, uthubutu na uzalenda wa kamanda huyu umeweza kuijenga cdm ambayo kwa sasa ni tumaini jipya kwa watanzania.Wengi wetu tunatambua kwamba mwaka 2013 kwa mujibu wa katiba ya chama ni mwaka ambao chama kitaenda kuchagua mwenyekiti mpya wa chama taifa. Mpaka sasa cjaona ni nani ambaye anaweza kurithi nyayo za kamanda huyu siye tetereka na mwenye uthubutu wa hali ya juu.Ni wengi sana wanaoutamani uenyekiti wa chama taifa na wengi wao wakiwa ni wale walio kwenye pay roll ya chama cha mapinduzi, nia na madhumuni yao yakiwa ni kukidhohofisha chama na kuacha upenyo kwa ccm kuendelea kushika atamu.Ninaomba ikiwezekana wale walio na nia njema na cdm pamoja na taifa kwa ujumla tumuombe kamanda Mbowe ifikapo 2013 agombee tena uenyekiti ili cdm iendelee kung'ara kuiondoa ccm madarakani.Nimejaribu kupitia katiba ya chama na cjaona limitation ya muda wa kuwa mwenyekiti.Hofu na mashaka ni kwa nafasi ya uenyekiti kutwaliwa na virus kama Zitto ambao tunajua wapo kwenye pay roll ya ccm.

Huku ni kubaka demokrasia. Unadhani Zitto atakubali tena kuuachia uenyekiti wa CHADEMA?
 
Waroho wa madaraka wanajivika mwamvuli wa democrasia ili kutimiza malengo yao, Jamani mbowe kaongoza vipindi viwili tu na ametuongoza vzr sana, Hatuna sababu ya kufanya trial and error 2013, kwa kufanya hivyo mjue kuna hatari kubwa ya kushindwa kuchua nchi 2015 na kupeleka safari ndefu tena ya kuujenga upinzani imara.

Bora aendelee kupata faida lukuki ya kukodi Helkopta kwa fedha kidogo halafu apige mabilioni akidanganya anakikopesha chama akiwa Mwenyekiti.
 
km kweli CDM wanataka kuendelea kuwa mfano wa kuigwa wa demokrasia hakika watajipanga vyema kumpata mrithi wa Mbowe!napendendekeza asiwe wa kanda ya kaskazini na awe muislamu,toka CDM ianzishwe hakuna muislam aliyeongoza,kwa kufanya hvyo itaondoa maneno ya udini,ukanda na ukabila ndani ya chama

Acha mawazo ya kijinga! Kwani uongozi ndani ya chama unapokezana kwa dini za watu!? Hizi ni fikra mbovu kabisa zinazopandikizwa na ccm na kuhubiriwa misikitini na Radio iman zinakuadhiri hata wewe unayejiita great thinker! Wake up!
 
Akikosekana tutaomba hata padre au mchungaji aliyeiva km askof laizer au prof.baregu.
 
Haya mambo ya demokrasi ya kupisha hata kama bado una nguvu, njozi na uwezo wa kutekeleza majukumu, ina walakini kama ilivyo kukaa madarakani kwa muda mrefu hata kama ulikwisha pauka.
 
Mbowe, slaa naq Tundu Lisu wanaaminika kwa msimamo Chadema sim kama Zitto na Shibuda ambao ni Popo.
 
Nyie mpeni tena uwenyekiti aendelee kuwauzia magari mabovu.Kweli CHADEMA ni chama cha watu wa dili
Deal kuliko richmond,iptl,net group solution,rites,ticts,buzwagi,epa,kagoda,kilimo kwanza etc?kwa taarifa mbowe ataendelea kuwa mkiti mpaka ccm itakapoondoka madarakani
 
Tumpongeze Mh Mboye na uongozi mzima kuanzia Taifa hadi shina kwa kazi nzuri wanazozifanya. Sisi tuliopo nje tunaona ni kazi rahisi lakini ukiingia kwenye hicho kiti pana moto jamani. Sisemi kwamba hakuna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza wapo wengi tu. Watanzania wote wanajua kuongoza na ndio maana wanaitaka tanzania itoke huko mikononi mwa mafisadi mpaka wengine wanafikia kupoteza roho zao walivyo na uchungu.

Mtazamo wangu jamani, jamani, chonde chonde tusiguse hapo juu. Hawa watu wanafanya kazi kwa ushirikianao na niwawazi wakisoseana wanasameheana. Tukisema tubadilishe mwenyekiti au makamu au katibu au naibu tutambue tunarudi tena kuanza moja. Mpaka ajeawe na speed aliyonayo Mh Mboye tutachukua muda, kwa sababu kila mmoja ana aina yake ya uongozi. Sasa hivi tuwaache huru tutafute wapiga kura 2015.

Hapa vile vile tuwe makini CCM wanataka kujua upepo ulivyohuku chadema ili ikifikia watafute mamluki wao ili agombee lakini tukiwa busy na shughuli zetu hawatajua ni nini malengo ya CDM. Mfano wakati wa Mrema, Mbatia alikuwa ni namba moja alikuwa anamshambulia Mrema sasa tujiulize ameweza kukiongoza chama cha NCCR zaidi ya kumfia?
 
km kweli CDM wanataka kuendelea kuwa mfano wa kuigwa wa demokrasia hakika watajipanga vyema kumpata mrithi wa Mbowe!napendendekeza asiwe wa kanda ya kaskazini na awe muislamu,toka CDM ianzishwe hakuna muislam aliyeongoza,kwa kufanya hvyo itaondoa maneno ya udini,ukanda na ukabila ndani ya chama
Mkuu Tafadhali! Naomba nikupinge sana on the highlighted above. Tukitafuta viongozi kwa mujibu wa dini au kabila tutaishia kuongozwa na viongozi wabovu maisha yetu yote. Dini wala kabila isiwe kigezo cha kupata kiongozi, hilo liweke akilini ni muhimu sana. Uangaliwe uwezo wa anayetaka uongozi si kabila lake wala dini yake. Hata CHADEMA ikiendelea kuongozwa na wenyeviti wakristo wachagga, kama wana vigezo na uwezo wa kiuongozi mm hilo halinipi tabu.
 
Mkuu Tafadhali! Naomba nikupinge sana on the highlighted above. Tukitafuta viongozi kwa mujibu wa dini au kabila tutaishia kuongozwa na viongozi wabovu maisha yetu yote. Dini wala kabila isiwe kigezo cha kupata kiongozi, hilo liweke akilini ni muhimu sana. Uangaliwe uwezo wa anayetaka uongozi si kabila lake wala dini yake. Hata CHADEMA ikiendelea kuongozwa na wenyeviti wakristo wachagga, kama wana vigezo na uwezo wa kiuongozi mm hilo halinipi tabu.

Unaonaje ikiwa muislam na mtu wa kusini na ana vigezo..litakupa tabu mkuu? au
 
Mwenye CV ya Mwenyekiti wa CDM, Freeman Mbowe, tunaomba atuwekee humu Jamvini
 
Huku ni kubaka demokrasia. Unadhani Zitto atakubali tena kuuachia uenyekiti wa CHADEMA?

Ndugu yangu si mpaka achaguliwe na wahusika? Hata mboye atagombea na ndio maana tunataka tumwombe agombee. Na ukilinganisha hata TUNDU LUIS atagombea na wengine wengi wanauhuru wa kugombea, kidemokrasia.
 
Ieleweke ndani ya CDM tuaangalia sifa za mtu anauwezo wa kuiongoza CDM hatuangalii kaongoza muda gani ieleweke hivyo kwahiyo hata Mbowe kama itadhibitika kabisa kabisa uwezo bado anao wa kutosha kabisa hasa kuidhibiti CCM isipate mwanya wa kuivuruga CDM kama ilivyo sasa maana huo ndio moyo wa CDM unaoifanya iwe tishio kwa CCM maana haivulugiki kirahisi pamoja na kuwa CCMwameweka mapandikizi yao humo CDM lakini hayaonekani kufanya kazi kwani yamedhitiwa sawasawa.
 
Kwa kweli Mbowe katufanyia makubwa sana Chama chetu lakini hii haina maana kwamba aendelee kuwa mwenyekiti hadi hapo tutakapomuona ni mzigo kwenye chama. Mimi namshauri is better afuate Principle za Nelson Mandela na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Akiache chama chetu akiwa bado anapendwa na wanachama wote. Yaliyowakuta kina Daniel Arap Moi na Robert Mugabe ni matokeo ya kubaki madarakani kwa muda mrefu. Ukibaki madarakani kwa muda mrefu kawaida unaishiwa mikakati hatimae wanachama wanasahau mema yote uliyoyatenda. Mimi ningependa Kumshauri kamanda Mbowe ni kweli bado tunampenda lakini aangalie uwezekano wa kuondoka kwenye Uenyekiti akiwa bado na Mvuto. Tutaendelea kumuheshimu kama Mzee Edwin Mtei na Bob Makani. Ni lini ang'oke hilo sasa ni lake mwenyewe.
 
Unaonaje ikiwa muislam na mtu wa kusini na ana vigezo..litakupa tabu mkuu? au

Mbona waislam tumeshindwa kumchagua mufti msomi mwenye uwezo wa kuongoza umma wa waislam na hatujui lini ataondoka labda afe,halafu sisi tunaona mbowe kakaa sana ktk uenyekiti?ritz,jasu,ms,ff tafakarini
 
Back
Top Bottom