Freeman Mbowe: Nguzo na mhimili muhimu kwa ustawi wa CHADEMA

Mawazo yako ni mazuri, ila sasa hili la kutaja jina la zito linanitia mashaka siku nyingine fikiria kwa makini.
 
Kweli Mbowe ni mkomavu wa siasa, na ni right person kuongoza cdm kuelekea 2015.
Na mimi binafsi ningependa aendelee kuongoza cdm. Hoja zake niu nzito, na zilizojaa busara na hekima. He is very strong. Na hii kwa kiasi kikubwa inachangiwa na msaidizi wake slaa, ambaye ana msimamo na anajua nini kinatakiwa kifanyike wapi na wakati gani. Hii combination ni nzuri kwa ustawi wa chama, na pia msingi wa kuelekea ukombozi wa Watanzania.

ZZKabwe asubiri muda wake ufike. ZZK hajakomaa, na inaonekana ana siasa za chuki na za ushindani (kusaka umaarufu). kwa hili sijui kama anatumiwa bila yeye kufahahamu au anajua.

Uvumilivu zito hauwezi. Na jaribu kumlinganisha zito na Mnyika. John ametulia zaidi.

Kama kwa kweli mbowe atakuwepo hio 2013, tumpatie akamilishe ukombozi wetu.

ONYO: WANA CDM TUSIJE TUKAINGIA KATIKA MIJADALA YA MIAKA YA MBELE KIUONGOZI KAMA CHAMA CHA MAGAMBA. TUTAVURUGWA
 
Wakuu ni wazo zuri kufikiria kumwongezea kamamda MBOWE muda wa uenyekiti,lakini tukumbuki magamba wanatuangalia na watakuja na slogan yao ya kuwa cdm ni taasisi ya wachache na ndio maana mwenyekiti amendelea yy hata baada ya muda wake kuisha.
mawazo yangu kiyi achukue SLAA kwani uwezo wake kila mtu hapa jamvini anaufahamu,then kamanda mbowe atengewe nafasi maalum yakushauri baadhi ya mambo pia ni wakati muuafaka kumtafuta MUUSLAM safi aliye vizuri ili kuondoa kale kamsemo kuwa cdm inaukristu,katibu kama watarizia wadau awe LISSU,pro SAFARI ikiwezekamna mm/kiti nawakilisha
 
tuna vichwa vyenye uwezo wa kutosha kama kamanda mbowe, chadema ni zaidi ya chama na utashangaa kuona chama kikipaa hata baada ya kamanda kustafu! VIVYEMA WAKATI HUU TUJADLI CDM TUNAYOITAKA BAADA YA MIAKA 5 - 10 IWEJE NA NINI WAJIBU WETU KATIKA KUFANIKISHA MATARAJIO HAYO!
 
Mbowe apewe tena, ZZK kibaraka wa CCM, ila mbeleni CDM inabidi wawe na democray zaidi, hii taswira ya kifamilia familia na kua chama cha watu wa kaskazini inaweza ikatumiwa na CCM vizuri. mpaka then Mbowe aendelee na u/kiti
 
wako wapi wale wanaosema chadema ni taasisi na si mtu?
kuna mmoja anasema kuwa mbowe aliwatafuta akina zitto na akina mdee? hivi hii ni kweli? mimi nijuavyo chadema ilikuwa na nguvu muda mrefu huko kigoma kabla hata ya umaarufu wa mbowe. kumbuka akini Amani kaburu. Na dhani ni vizuri tusipotoshe ukweli.
 
Hao wanaopinga uwezo na mafanikio yaliyoletwa na Mbowe kwa CHADEMA wanaweza kuwa vibaraka wa CCM.Sisi wana CHADEMA tunaamini na kuthamini mchango wa Mbowe kwa chama na tunasema na tunaelewa kuwa kuna wengine wenye uwezo wa kuongoza kwa nafasi ya uenyekiti.Laikini Mbowe bado anahitajika sana na hatutakubali kumwachia kutokana na propaganda zenu eti aachiwe mtu mwingine wakati tunaowafahamu kuwania nafasi hiyo wengi ni wanafiki na vibaraka wasioweza kuaminiwa.Kama watajitokeza watu makini ni sawa lakini hao mnaowataja kwa sasa hawafai kabisa na watauza chama
 
wako wapi wale wanaosema chadema ni taasisi na si mtu?
kuna mmoja anasema kuwa mbowe aliwatafuta akina zitto na akina mdee? hivi hii ni kweli? mimi nijuavyo chadema ilikuwa na nguvu muda mrefu huko kigoma kabla hata ya umaarufu wa mbowe. kumbuka akini Amani kaburu. Na dhani ni vizuri tusipotoshe ukweli.

kwa hiyo huyo Aman Kabourou wako yuko wapi sasa hivi?
 
Nitoe maoni yangu na mimi. Kwa kweli CDM ni taasisi kubwa.Wapo watu wengi sana wenye uwezo wa kuwa viongozi na bado chama kikasonga mbele maradufu. Hata hivyo tukubali uongozi si sawa na kuachiana shati.Mbowe ni kiongozi aliyetukuka na ni tajiri.Kuwapa watu wenye njaa nafasi kama hiyo hakika CDM inawekwa rehani.Tuliambiwa CDM inajenga chuo cha kufundisha itikadi makada wake.Kwa hiyo CDM iwaachie Mbowe na Slaa waendelee kwa miaka mingine 5 huku ikiwaandaa warithi wake makini watakaopokea usukani mwaka 2018.Ni wazi wakati huo vijana kama Mnyika,Zitto,Lissu nk watakuwa wamekomaa kupokea jahazi. Tukubali CDM sasa ipo katika hatua za mwisho za kukamata dola.Itakuwa ni hatari kubwa kukibadilisha kikosi cha ushindi kilicho mstari wa mbele wa mapambano.
 
Mi labda nianze kwa diagram, maana naamini picha inaongea zaidi...

vyama.jpg

Kati ya kosa kubwa linalofanywa na baadhi ya wanachadema, ni kudhani kuwa mafanikio ya CHADEMA yameongozwa na MBOWE... Sio kweli, mafanikio ya CHADEMA yameongozwa na Mbowe+Slaa+Zitto, na hawa ni sawa na mafiga matatu ambayo kila moja limefanya kazi yake kwa kutegemea jingine.

Kuna upuuzi wa baadhi ya watu wanaleta ushabiki wa kijinga kuwa mara Zito anatumika, mara Mbowe si chochote kwa Zitto... Huu ni upuuzi na litakuwa kosa kubwa sana kuwalinganisha hawa watu kuwa kuna wa kuhimu zaidi katika chama...

Kila mmoja amecheza nafasi yake vyema. Kama 2013 kutakuwa na mabadiliko, fine lakini kama timu inavyosajili wachezaji, huwezi kuwa na uhakika 100% kuwa anayekuja kuchukua namba ya fulani ataweza kucheza kuliko yeye.

Kama kuna ambaye atatoka katika hizo nafasi tatu, basi rearrangement inaweza kufaa, ila kama watabaki wote watatu, then wabaki na nafasi zao kama zilivyo, hadi pengine kutakapokuwapo na madabiliko mabaya kwenye hiyo graph.

Mi namuomba kaka yangu Mbowe, ametuongoza hadi hapa, distance fupi kabla ya kuingia nchi ya ahadi, avumilie tu, najua inachosha lakini kama ameweza kuwa nasi njia nzima, sioni cha kukata tamaa kwa muda mfupi huu uliobaki...
 
Nayachukuki sana mawazo ya kuwatukuza watu kiasi ya kuona kwamba kama watu hao hawapo basi hakuna kinachowezekana. Chama kinaendeshwa na katiba na sera za chama kwa hiyo watu wengine wakipewa fursa ya kuongoza wanaweza wakawa wazuri zaidi kuliko huyo mnaemuona malaika.
 
Chadema sio chama ni kampuni ya mbowe na mbowe anatumia mwamvuli wa kukiita ni chama ili iwe rahisi kupitisha dili zake kutoka nje.lakini inafaa aendelee kua mwenyekiti wa kampuni au NGO kwa sababu zifuatazo(1)alirithi kutoka kwa mkwe wake (mtei)(2)kampuni inaitwa chaga development manifesto na yeye ni mchaga (3)ndani ya kampuni yake kamati kuu inaidadi kubwa sana sana ya wachaga akiwemo lema(4)ni vema akaendelea kua mwenyekiti kwa sababu yale magari mabovu aliyo wauzia chadema bado hajalipwa na chadema wanatumia account ya mbowe kwa hio akiondoka atashindwa kujilipa maana watabadilisha account(5)akiondoka watu kama wakina grace kiweru,suzan limo na wabunge wengine wachaga wa viti maalum hawatakuja kupata tena ubunge (6)chadema watapata wapi mtu mwingine wa kuwanunulia kofia,kadi na bendera china kama sio mbowe(7)akiondoka kwenye uenyekiti si atakua ameharibu lile dili lake la kwamba hua anakikopesha chama(8)tukimtoa tutayamis sana maandamano(9)asipo kua mwenyekiti wakurugenzi kama wakina john mrema,anton komu na wachaga wengine pale makao makuu watafanya kazi gani?(10)anapinga sana watu wanao mpinga kama alivyo mfanyia chacha wangwe(11)asipo kua mwenyekiti anamaanisha atarudisha gazeti la chama tanzania daima alilo jimilikisha yeye binafsi wakati conservative walitoa msaada kwa chama.
 
Kwa kweli Mbowe katufanyia makubwa sana Chama chetu lakini hii haina maana kwamba aendelee kuwa mwenyekiti hadi hapo tutakapomuona ni mzigo kwenye chama. Mimi namshauri is better afuate Principle za Nelson Mandela na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Akiache chama chetu akiwa bado anapendwa na wanachama wote. Yaliyowakuta kina Daniel Arap Moi na Robert Mugabe ni matokeo ya kubaki madarakani kwa muda mrefu. Ukibaki madarakani kwa muda mrefu kawaida unaishiwa mikakati hatimae wanachama wanasahau mema yote uliyoyatenda. Mimi ningependa Kumshauri kamanda Mbowe ni kweli bado tunampenda lakini aangalie uwezekano wa kuondoka kwenye Uenyekiti akiwa bado na Mvuto. Tutaendelea kumuheshimu kama Mzee Edwin Mtei na Bob Makani. Ni lini ang'oke hilo sasa ni lake mwenyewe.

Una mawazo mazuri sana,lakini kwa mwendo ulivyo sahivi ni bora akakipitisha chama kwenye uchaguzi wa 2015.ZZK asubiri 2018 hapo atakua na experience ya kutosha sana.
 
Ninaandika hapa jamvini nikiwa na mawazo lukuki juu ya mustakabali wa cdm endapo kamanda Mbowe ataamua kutogombea tena Nafasi ya uenyekiti wa chama taifa.Hakuna mwana jamvi asiyeelewa ni kwa jinsi gani kamanda na mpiganaji Mbowe amekikbeba chama hiki na kufikia hapa kilipo na kutishia kabisa mustakabali wa ccm.Juhudi, maarifa, kujituma, uthubutu na uzalenda wa kamanda huyu umeweza kuijenga cdm ambayo kwa sasa ni tumaini jipya kwa watanzania.Wengi wetu tunatambua kwamba mwaka 2013 kwa mujibu wa katiba ya chama ni mwaka ambao chama kitaenda kuchagua mwenyekiti mpya wa chama taifa. Mpaka sasa cjaona ni nani ambaye anaweza kurithi nyayo za kamanda huyu siye tetereka na mwenye uthubutu wa hali ya juu.Ni wengi sana wanaoutamani uenyekiti wa chama taifa na wengi wao wakiwa ni wale walio kwenye pay roll ya chama cha mapinduzi, nia na madhumuni yao yakiwa ni kukidhohofisha chama na kuacha upenyo kwa ccm kuendelea kushika atamu.Ninaomba ikiwezekana wale walio na nia njema na cdm pamoja na taifa kwa ujumla tumuombe kamanda Mbowe ifikapo 2013 agombee tena uenyekiti ili cdm iendelee kung'ara kuiondoa ccm madarakani.Nimejaribu kupitia katiba ya chama na cjaona limitation ya muda wa kuwa mwenyekiti.Hofu na mashaka ni kwa nafasi ya uenyekiti kutwaliwa na virus kama Zitto ambao tunajua wapo kwenye pay roll ya ccm.

Hapana shaka kuwa uongozi wa Mbowe umekisogeza sana mbele chama kuliko watangulizi wake. Lakini hilo la kutoona mrithi wake linaweza kuwa linasababishwa na uoni wako hafifu.
 
Ninaandika hapa jamvini nikiwa na mawazo lukuki juu ya mustakabali wa cdm endapo kamanda Mbowe ataamua kutogombea tena Nafasi ya uenyekiti wa chama taifa.Hakuna mwana jamvi asiyeelewa ni kwa jinsi gani kamanda na mpiganaji Mbowe amekikbeba chama hiki na kufikia hapa kilipo na kutishia kabisa mustakabali wa ccm.Juhudi, maarifa, kujituma, uthubutu na uzalenda wa kamanda huyu umeweza kuijenga cdm ambayo kwa sasa ni tumaini jipya kwa watanzania.Wengi wetu tunatambua kwamba mwaka 2013 kwa mujibu wa katiba ya chama ni mwaka ambao chama kitaenda kuchagua mwenyekiti mpya wa chama taifa. Mpaka sasa cjaona ni nani ambaye anaweza kurithi nyayo za kamanda huyu siye tetereka na mwenye uthubutu wa hali ya juu.Ni wengi sana wanaoutamani uenyekiti wa chama taifa na wengi wao wakiwa ni wale walio kwenye pay roll ya chama cha mapinduzi, nia na madhumuni yao yakiwa ni kukidhohofisha chama na kuacha upenyo kwa ccm kuendelea kushika atamu.Ninaomba ikiwezekana wale walio na nia njema na cdm pamoja na taifa kwa ujumla tumuombe kamanda Mbowe ifikapo 2013 agombee tena uenyekiti ili cdm iendelee kung'ara kuiondoa ccm madarakani.Nimejaribu kupitia katiba ya chama na cjaona limitation ya muda wa kuwa mwenyekiti.Hofu na mashaka ni kwa nafasi ya uenyekiti kutwaliwa na virus kama Zitto ambao tunajua wapo kwenye pay roll ya ccm.

Mkuu Kwayu kwanza Lazima nitilie Mashaka Uamuzi wako wa kuanzisha threa hii hasa kipindi hiki, lakini hayo yote ni Mawazo yako na siyo lazima yawe sahihi

Ni Kweli kwamba Freeman Mbowe kwa kushirikiana na timu yake ya CHADEMA wamefanya Mambo makubwa sana kwa CDM. Chini ya kipindi chao CDM imekuwa na imeaniwa na Wananchi kwamba sasa yaweza kushika dola

Mabadiliko ndani ya CDM hayaepukiki kama CDM inaamini katima Demokrasia na ninaamini kabisa kwamba Ndani ya CDM kuna watu wanaweza kuwa kama Mbowe au Zaidi ya Mbowe inategemea tu Kocha umeteua timu ya Namna gani.

Kama CDM inataka iendelee kuaminika basi inahitaji Mtu atakayemrithi Mbowe awe ni Zaidi ya Mbowe na si kama Mbowe. CDM ikifanikiwa kumpata Mtu Zaidi ya Mbowe akateua timu nzuri ya Kufanya Nayo Kazi basi CCM itakuwa na wakati Mgumu sana

Naamini CDM ina utaratibu Mzuri wa kuwaandaa Makada wake kushika Nafasi Mbalimbali za Uongozi katika Chama,Mwenyekiti ni Lazima awe Mwaminifu na awezaye kuunganisha Nguvu ya Vijana ambao naamini ndio mtaji mkubwa wa CDM

Naamini Mbowe atapumzika na atakumbukwa sana na atakuwa ameweka Changamoto kubwa sana kwa Mwenyekiti wa CDM atakayemrithi
 
Back
Top Bottom