Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,321
- 219,633
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , Yule Mwamba wa siasa za Kisasa kwenye eneo la Maziwa Makuu , Freeman Mbowe , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama kikubwa zaidi na kinachoungwa mkono na wananchi wengi zaidi Nchini Tanzania , anatajwa kuwa ndiye Kiongozi wa Kisiasa aliyejadiliwa zaidi kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu kwa Mwaka 2023 , akiwaacha Mbali wanaomfuatia , Rais wa DRC Tshishekedi na Dikteta Paul Kagame wa Rwanda
Magwiji wa siasa kwenye eneo hilo wanataja sababu kuu ya mtu huyu ambaye pia anajulikana kama Ustaadh Aboubakar Mbowe kujizolea umaarufu huu , ni pamoja na Karama ya Ushawishi aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu , huku jambo kubwa lingine likiwa ni kukisimika chama chake Nchi nzima , vikiwemo vijiji vya Dodoma na Ruvuma, ambavyo kwa miaka mingi viliamini kwamba CCM ni kama dini na kwamba ukiiacha ni sawa na kutenda dhambi
Msimamo wake katika Kupigania haki kwenye Nchi yake , ndio nguzo kuu ya Imani ya Wananchi kwake binafsi na kwa Chama chake , Matajiri wengi wa Tanzania na nchi nyingi za kiafrica hujiambatanisha na Watawala kwenye ukandamizaji wa Raia , Wananchi wanashangaa imekuwaje Bilionea Mbowe yeye yuko na Wananchi tu badala ya kushirikiana na watawala kunyonya rasilimali za Taifa .