Freeman Mbowe atetemesha Itilima-Simiyu

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe leo ameendelea na ziara yake kwa kuingia kwa kishindo wilayani Itilima mkoa wa Simiyu akitokea mkoa wa Tabora alikohutubia halaiki ya watu Nzega hapo jana.

Mara baada ya kuingia wilayani Itilima Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya upinzani bungeni amelakiwa na msururu wa magari,pikipiki na baiskeli huku wananchi wakijipanga kandokando ya barabara na kupeperusha majani ya miti.

Kwa sasa Mwenyekiti huyo wa Ukawa anahutubia umati mkubwa wa watu katika kijiji cha Legangabilili wilayani humo

Tunaungana na Kamanda Standalone aliyeko kwenye msafara wa Mwenyekiti kutuletea Live updates..

Karibuni...





Kaa tayari kwa picha zaidi wakati wa mkutano,,,,,Umati mkubwa tayari ushaanza kuwasili eneo la mkutano....

Mwenyekiti akipata chakula cha mchana na vijana wa Red brigade waliokuwa wamehitimu mafunzo

Akipata pia chakula na wenyeji wa kata ya Lagangabilili mara baada ya kuzungumza ni vijana hao waliokuwa mafunzoni
 
Last edited by a moderator:
Kamanda Mbowe endelea kusambaza upendo njia nyeupe kwa Ukawa kuingia ikulu.
 
Kamanda Mboye piga kaz ya Mungu ya kuwakomboa Watanzia kwenye dimbwi la umasikin hali yakuwa nchi yao unautajiri wa kutupwa. Piga kaz kamanda wangu wa Anga,
 
Leo Mwenyekiti wa Chadema Taifa yupo Mkoa wa Simiyu katika siku ya pili ya ziara yake.
Yupo katika,
Wilaya: Itilima
Kata: Lagangabilili
Kijiji: Lagangabilili.
Kabla ya kula Kiapo Mwenyekiti Mbowe alipewa baraka na wazee wa kisukuma nabkukabidhiwa mkuki na ngao kwa ajili ya utetezi wa taifa


Mwenyekiti anazindua mpango wa FTP 200 wa Ulinzi na Usalama wa Chama na viongozi na mali za Chama.
Mwenyekiti Mbowe aliwasili katika Kijiji cha Lagangabilili majira ya saa saba mchana akutokea Mkoani Tabora ambapo alizindua mpango wa FTP 200 Katika Wilaya ya Nzega, Kata ya Ndala.

Baada ya kuwasili Lagangabilili- Wilaya ya Itilima Mwenyekiti alikwenda katika Ofisi ya Chadema Wilaya ya Itilima na kusaini Kitabu cha wageni na hatimaye akawasili katika eneo ambalo kuna Kambi ya Vijana ambao wakuwa Kambini wakipata mafunzo katika eneo la wazi ya Ujasiriamali endelevu, Ulinzi Shirikishi, Uzalendo, Kupambana na rushwa pamoja na sheria na taratibu za uchaguzi.

Mwenyekiti alielezwa na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare kuwa vijana hao pia wana mafunzo ya uwakala pamoja na hamasa za kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Wapiga kura.
Akihutubia vijana hao baada ya kula kiapo Mwenyekiti alisema kuwa idadi ya polisi ukilinganisha na idsdi ya watu ni ndogo sana ukilinganisha na vigezo vya Umoja wa Mataifa. Hivyo ni lazima wajilinde.
Aliwataka Msajili wa vyama na IGP kuachana na propaganda za kisiasa kwa sababu kujilinda ni haki ya kikatiba na kisheria.
Mwenyekiti atapata chakula pamoja na wananchi na wahitimu wa mafunzo kwenye uwanja huu ambao ni Kambi.

Picha zina kuja soon usiondoke...
 
Reactions: jme
Hakika Mungu ataendelea kuitwa Mungu.

Mungu mwenye enzi yote ataendelea kuilinda CHADEMA, chama ambacho bila woga wa aina yoyote imeendelea kuwapigania na kuwatetea wanyonge wa nchi hii......

Watanzania wanatambua ngano safi ni ipi, na magugu ni ipi.... Hakika chadema ni mpango wa Mungu.


Mbowe pambana katika vita hii ya haki kuwatetea wanyonge waliokwisha nyanyaswa na maccm na vibaraka wao, Mungu yupo na wewe, Watanzania wanakutegemea.

Mungu Ibariki chadema
Mungu Ibariki Tanzania
 
Hii habari japo hata kwa baadae kidogo ikolezwe na picha tafadhali ili akina naniliii wajionee kwa macho!!
 




Kaa tayari kwa picha zaidi wakati wa mkutano,,,,,Umati mkubwa tayari ushaanza kuwasili eneo la mkutano....
 

Attachments

  • IMG-20150423-WA0040.jpg
    220 KB · Views: 9,090
  • IMG-20150423-WA0037.jpg
    152.9 KB · Views: 9,310
  • IMG-20150423-WA0036.jpg
    162.2 KB · Views: 8,846
  • IMG-20150423-WA0034.jpg
    153.5 KB · Views: 1,252
Standalone
Ccm wakiona hizi picha wanachanganyikiwa kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kamanda Molemo na Standalone kwa kutupatia updates.

Kamanda Mbowe endelea kuchanja mbuga zindua vikosi vya ushindi wakati wao wanafundisha green guards kuiba kura, kuteka, kuua na kujeruhi wapinzani we endelea kufundisha uzalendo na ulinzi wa kura vijana wa CHADEMA. Mwaka huu hakuna cha kura kuibiwa cc cm itapata haki yake na UKAWA haki yake.
 
Tupo pamoja,lazima magamba yameng'unyuliwe
 
Aluta continue makamanda adui yupo Karibu sana hakuna kulala...
 
Hizo picha zinawatisha Mbaya magamba na mawakala wao. Hii nchi imeiva Kwa ukombozi
Ahsante CHADEMA na UKAWA Kwa kuonyesha moyo wa that kutuondolea ccm
 
Mungu ibariki CHADEMA,
Ibariki CUF,
Ibariki NCCR-MAGEUZI,
Ibariki NLD na viongozi wote wa UKAWA.
Aamen!!
 
Karibu tutatoka katika minyororo hatari ya maccm na vibaraka wake bila kusahau akaayatullah zuberi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…