Kinachosubiriwa ni utaratibu wa kutolewa Segerea.
UPDATES:
=> Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama wa Chadema akiwemo Mbunge Halima Mdee waliofika gereza la Segerea kumchukua Mwenyekiti Freeman Mbowe
=> Wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee na Ester Bulaya, Meya wa Ubungo Boniface Jacob na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar, Henry Kileo wamekamatwa wakati wakifuatilia mwenyekiti wa Chadema kutoka gereza la Segerea
=> Kuhusu Mbowe bado mchakato wa kumtoa gerezani unaendelea maana dereva aliyekuwa na risiti akielekea Segerea naye amekamatwa baada ya Polisi kupiga mabomu.
=> Askari Magereza wametumia silaha za moto na kufyatua risasi hewani kuwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya gereza hilo kumsubiri Mbowe akiachiwa. Baadhi ya viongozi na wananchi kadhaa wamejeruhiwa, akiwemo dereva mmoja wa bodaboda ambaye inadaiwa amevunjika mguu.
UPDATES: 1750HRS
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hatimaye ameachiwa kutoka Gereza la Segerea baada ya taratibu kukamilika. Sasa anaelekea Makao makuu ya CHADEMA mtaa wa Ufipa Kinondoni.