Kwani Mkuu unadhani walikuwa hawajui kama wamecingiziwa watoto..?
Utajuaje kwa njia zisizo za kisayansi? Utaangalia kama ana fanana na wewe au?
Nadhani wewe unachanganya kujua na kuhisi unless uniambie njia walizokuwa wanatumia kujua. Au hujui maana ya neno kujua?
Sema busara na hekima ziliwapa ujaciri wa kuwa wastahamilivu..
Kuna busara na hekima gani katika kutwishwa ama kujitwisha majukumu ya mtu mwingine ambaye hana sababu ya msingi ya kukwepa majukumu yake? Huo ni ujinga.
Acili ya msemo kitanda hakizai haramu ilikuwa ni ku-justify kosa ambalo kwao lilikuwa linasameheka..
Linasameheka kwa nani? Kwako na kwa wenye mtazamo kama wako? Maana usiongelee kila mtu hapa. Kuna watu kosa kama hilo halisameheki ng'o.
Kwani wewe Mkuu unahitaji DNA kutambua mtoto ni wako au lah..?
Kwa vile sina shaka kuwa ni wangu na hakuna kingine kilichopelekea kuhisi wala kudhani kuwa si wangu, sihitaji DNA.
Lakini vilevile kuna mazingira ambayo hupelekea mtu kuhoji kama kweli mtoto ni wake au siyo wake. Wapo watu ambao hawakuwa na uhusiano kwa muda mrefu (tuseme wiki chache tu) halafu baada ya mwezi mtu unapewa habari za ujauzito.
Na wakati mna-do the do hamkuwa exclusive. Kila mmoja pengine alikuwa ana-do na wengine pia.
Sasa katika mazingira kama hayo kwa nini mtu usihoji? Na kuhoji na kutaka vipimo vya DNA haina maana kwamba unataka kukwepa majukumu au sijui unataka kuanzisha sokomoko.
La hasha! Ni kwamba tu unataka kujirdhisha kuwa kweli huyo mtoto ni wako na kama DNA itathibitisha kuwa ni wako basi uta step-up to the plate na kuwajibika kama mzazi.
Hebu niambie sasa, ubaya uko wapi hapo? What is so unreasonable about it?