Frederick Sumaye na Cecil Mwambe: Miamba iliyoitikisa CHADEMA kwa kugusa maslahi ya chama ndani ya chama

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
FREDERICK SUMAYE NA CECIL MWAMBE,MIAMBA ILIYOITIKISA CHADEMA KWA KUGUSA MASLAHI YA CHAMA NDANI YA CHAMA.

Leo 12:15pm,16/02/2020.

Kilele cha Mafanikio ya Chadema kama Chama Cha Upinzani kilikuwa ni mwaka 2015 chini ya Edward Lowassa aliyekuwa Mgombea Urais na Freeman Mbowe akiwa Mwenyekiti wa Chama.

Pengine watu wengi waliowaza na kuyataka mabadiliko walimuunga mkono Edward Lowassa aliyebeba ajenda ya mabadiliko kwa kuahidi Mabadiliko kila paliposhindikana katika awamu zote nne za CCM,kumbuka Edward Lowassa alitokea CCM na ajenda hiyo na kwenda nayo Chadema.

Toroka uje ilikuja baada ya wana CCM kumfuata Edward Lowassa alipohamia Chadema,Ule ulikuwa ni upepo wa kisiasa, kwa sababu mwaka 2015 ulionekana kama mwaka rahisi zaidi wa kuiangusha CCM, jambo hilo likashindikana,

Hivi sasa tuna Msemo mwingine "Nyumbani kumenoga na wana CCM na wasio wana CCM wote wanarudi CCM baada ya kuona Rais John Magufuli ameyatenda vyema mageuzi na maono ya Mabadiliko aliyoyaota Ndugu Edward Lowassa.

Hii inatupa picha kuwa malengo makuu ya viongozi wengi walioondoka CCM kuelekea upinzani hayakufanikiwa.Hii ni sababu Rais John Magufuli ametambaa na kutembea sawia katika sera zao za Mabadiliko,kupiga vita kila aina ya upumbavu uliokuwa ukitendwa hata watu kutaka Mabadiliko,

Rais John Magufuli ameibadili nchi na kuielekeza kuelekea uchumi wa kati kitu ambacho kilishindwa kufanyika katika Awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete.

Rais John Magufuli amekomesha upuuzi wa Madawa ya kulevya baada ya takwimu za mwaka 2013 kuonyesha idadi ya waathirika wa madawa ya kulevya ni sawa na nusu ya Jeshi letu na kutoa ishara ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa la Tanzania.

Rais John Magufuli amepiga vita rushwa na Ufisadi ambao ndio ilikuwa ajenda kubwa ya Chadema na kuwafanya Chadema kukosa ajenda na kuanza kulinda maslahi ya watu ndani ya Chadema,

Kitako cha andiko hili ni kuonyesha jinsi Chadema ilivyokosa sera mbadala baada ya Serikali ya CCM ya awamu ya tano,chini ya Rais John Magufuli kubeba sera zao zote na kuzitendea haki kwa kuzitekeleza kwa asilimia mia moja 100%.

Sera za Chadema na Upinzani kwa ujumla ziliegemea kwenye madhaifu ya utekelezwaji wa Sera za CCM,kwa ufupi Sera zote za Chadema na Upinzani zilikuwemo ndani ya Sera za CCM,shida kubwa ya CCM ilikuwa ni utekelezwaji wa asilimia mia moja wa Sera hizo,

Rais John Magufuli kama Mwenyekiti wa CCM ameweza kuzitekeleza sera za CCM za Awamu ya tano kwa asilimia mia moja na ishirini 120%,kwa namna hiyo wana CCM waliokwenda Chadema na "Toroka Uje" hawana cha kufanya upande wa upinzani hasa Chadema tena baada ya kuona uwepo kwa Chadema ndani Chadema,

Jambo la kuiona Chadema ndani ya Chadema liliwafanya kuitazama ile Chadema iliyo ndani ya Chadema kwa jicho la tatu la kiroho na kifalsafa na kutaka kuiingia,hapo ndipo walipotenda kosa kubwa sana kwa kugusa maslahi ya Chama ndani ya Chama.

Kinachojiri hivi sasa ndani ya upinzani na hasa Chadema, ni kile kile nilichojiri CUF na ndicho hicho kitachojiri ACT hapo baadae,

Mapambano makubwa ya madaraka, kuhodhi madaraka na kukosa mipango endelevu na ya muda mrefu ni matokeo ya kukosa sera mbadala.

Tumeona Waziri Mkuu Mstaafu akiombwa katika Wilaya yake kugombea nafasi ndogo ya uongozi ndani ya Chadema, uenyekiti wa kanda ya Pwani,

Lakini siku ya Uchaguzi akapigiwa kura ya hapana,Mbaya zaidi hakuwa na mpinzani. Walichomfanyia wapiga kura ni kile kinachoitwa demokrasia ya uchaguzi lakini ambacho wengi tunajua ni ‘figisu za uchaguzi’.

Kiuchambuzi, wajumbe wa kikao husika kilichomkataa Sumaye walifanya hivyo si kwa sababu hawamtaki, la hasha! Sababu halisi ambayo mtu yeyote aliyewahi kufanya siasa za upinzani Tanzania atakwambia ni kosa la kugusa maslahi mapana ya chama chake.

Siasa za upinzani za Tanzania ni kuwa na chama ndani ya chama,kunakuwa na Chama cha nje ambacho kila mwanachama anaamini ni sehemu yake lakini chama cha ndani ni kile cha wenyewe.

Nikurudishe nyuma kwenye Siasa za ndani ya CUF, kwa hakika upande wa Tanzania Bara kulikuwa na CUF inayoonekana kwa kila mtu lakini ndani yake kukiwa na CUF ya ndani ambayo inaongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba.

Na upande wa Zanzibar kumekuwa na CUF ambayo wananchi wote wanaiona hadharani lakini kwa ndani kuna ile CUF ya Maalim Seif.

Siasa za chama ndani ya chama ni moja ya mambo yanayovifanya vyama vya upinzani vya Tanzania kuwa dhaifu, na visivyoweza kukabili mapambano ya kisiasa pindi wanapokosa hoja.

Sasa nikurudishe ndani ya Chadema,Ndani ya Chadema kuna chama ndani ya chama. Yaani,Chadema inayooneka wanachama kindakindaki iliyosajiriwa na Msajili lakini ndani yake kuna chadema nyingine ndani ya Chadema iliyosajiriwa na Msajili.

Ili uwe salama kwenye vyama vyetu vya upinzani, unapaswa kuwa mwanachama wa chama cha nje kilichosajiliwa,na kuacha Chama cha ndani ya chama, ukihoji ya ndani ni kosa.

Kosa kubwa ambalo mtu yeyote aliyeko upinzani anaweza kulifanya, ni kujisahau na kugusa maslahi yoyote ya chama ndani ya chama, au chama cha wenye chama. Maslahi hayo mara nyingi yanahusu kuhoji matumizi ya fedha na kugombea nafasi nyeti kama Uenyekiti wa kanda na Uenyekiti wa Taifa.

Kwa vinywa vyao ndugu Frederick Sumaye na Ndugu Cecil Mwambe wamekiri kupigiwa kura za hapana na kukataliwa na Wanachama wa Chadema baada ya kugombea Uwenyekiti wa kanda zao huku wakionekana kuchukua fomu ya kugombea Uenyekiti wa taifa,

Jambo kuchukua form ya kugombea Uenyekiti wa Taifa linaangukia kwenye yale masuala machache ambayo ukiyafanya upinzani huwezi kubakia salama.

Kwa upinzani ziko nyadhifa ambazo ni za kudumu kwa watu fulani, hadi pale watakapochoka wenyewe na waweze kupata watu wa kuwaachia nyadhifa hizo,

Wakikosa watu wa kuwapa huwa ni rahisi kumwaga mboga na ugali na kuvunja chama, kama ilivyotaka kuvunjika CUF.

Ni dhahiri vyama vya upinzani vinatumia nguvu kubwa mno kupambana ndani ya vyama na kulinda nafasi za watu fulani, kuliko nguvu zinazotumiwa kwenye siasa za jumla za kitaifa.

Haya yaliyowakuta Sumaye na Mwambe leo, yameikuta orodha ya makumi na makumi ya viongozi wa upinzani ambao waliwahi kugusa maslahi ya chama ndani ya chama kwa wenye chama rejea Chacha Wangwe na Zitto Kabwe baada ya kutangaza kuchukua form za kugombea Uenyekiti wa Chadema.

Kama Upinzani ungechukua nchi 2015 tungekuwa na Chama kimoja cha kipimbi sana kinachotuongoza kijinga kuanzia kuamka mpaka kulala. Sio siri ukiitoa CCM hakuna Chama kingine Tanzania ambacho kimefuzu kuiongoza Tanzania,Rejea Viongozi waandamizi wa Upinzani Zitto Kabwe na Tundu Lissu ambao wanazunguka Ulaya kulamba miguu ya wazungu.

Nimalizie kwa kushukuru utendaji wa kutukuka wa Rais John Magufuli ambao umemrudisha CCM,aliyekuwa Mgombea Urais wa Chadema 2015,Ndugu Edward Lowassa,

Utendaji makini wa Rais Magufuli umewarudisha CCM wale wote waliondoka na Toroka Uje kwa Upepo wa Edward Lowassa.

Utendaji makini wa Rais John Magufuli alimrusisha CCM,Dr Wilbrod Slaa aliyekuwa Katibu wa Chadema akizunguka Tanzania nzima kuijenga Chadema katika misingi ya hoja na kubeba Sera za Kitaifa.

Utendaji wa Kizalendo wa Rais John Magufuli,umeiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake zote.

Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumbariki Rais wetu John Magufuli.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Walioukosa uenyekiti ili waibomoe wakastukiwa hivo hawana cha ziadi zaidi ya kurudi walipotumwa kutoa ripoti
 
Kwa akili yako hata ungekuwa na elimu ya chekechea,huko walikoludi CCM watapewa nafasi ya uenyekiti CCM Taifa?
Wasithubutu hata kuuwazia huo uenyekiti,si wa Taifa,Mkoa hata wilaya.Hawawezi kupewa maana hawana mkia.
 
Mimi nime watambua kwenye media hawajanitikisa ' you can look by the face if upstairs working perfect'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu..umeandika kama mfuasi wa Chama fulani . Hapo ndipo ulipoharibu hoja yako...ulitakiwa uwe neutral hapa ili hoja yako iwe elimu mujarabu kwa kila asomae...
Kiukwl siasa inayochezwa hapa nikwambie ukweli sasa hivi biashara ya utumwa imerudi indirectly ila wenye fikra ndyoo wanajua...na inaskitisha wasomi kwl kwl tuliowategemea kukemea biashara haramu wanakubali kuwa slaves!!..Mkuu a mini u siamini utumwa umerudi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chali mbaya
IMG_20200219_122948.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom