Francis Godwin Alivyofanyiwa unyama na Polisi iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Francis Godwin Alivyofanyiwa unyama na Polisi iringa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 6, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Awali ya yote ninapenda kumshukuru Mungu aliyenileta duniani na atakayenitoa hapa duniani,Ndungu zandu na wadau zangu wapendwa nitakuwa si mpiganaji wa kweli kama nitabaki na siri hii ya kukamatwa kwangu na jeshi la polisi na pia sitakuwa muungwana kama nisipowashukuru wote kwa dua zenu hadi nimeachiwa huru.

  Ninaomba kwa sehemu niweze kuelezea yaliyonikuta hadi nikakamatwa na polisi ilikuwa ni jumanne ya Mei 31 majira ya saa 7.45 eneo la shule ya sekondari Tosamaganga wakati nikitoka kufuatilia sakata la mgomo wa wanafunzi ndipo nilipokamatwa na askari wa upelelezi watatu . Dalili za kuwepo kukamatwa zilianza kujionyesha toka jumatatu ya mei 30 eneo la Mseke wakati nikiwa na mwenzangu wa Radio Ebony Fm ambapo mkuu wa polisi wilaya ya Iringa alitupiga stop kuendelea kufuatilia sakata la FFU kuwapiga mabomu wa wanafunzi wa sekondari ya Tosamaganga bila kuwa na kibali cha polisi . kutokana na kiongozi huyo wa polisi wilaya kututaka kuomba kuifanya kazi hiyo tulilazimika kuondoka na kwenda kuripoti tukio la wanafunzi hao kugoma katika vyombo vya habari ukiwemo mtandao huu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima.


  " Kabla ya kuondoka eneo la tukio kijiji cha Mseke mpakani mwa Iringa vijijini na mjini ambako wanafunzi hao zaidi ya 1000 walitawanywa na FFU kwa mabomu tulipata kumuuliza mkuu huyo wa Polisi aina ya vibali ambavyo vinatolewa na jeshi la polisi kwa waandishi wa habari wanapotakiwa kufuatilia tukio " Hata hivyo siku ya pili ambayo ni jumanne Mai 31 majira ya saa 7.45 nikiwa katika shule ya sekondari Tosamaganga kufuatilia hali ya mgomo huo ghafla alizingirwa na polisi wa upelelezi ambao waliziba barabara na kunishusha katika gari kwa nguvu huku wenzangu wawili akiwemo wa Radio Ebony na ITV wakiachwa .

  "Pamoja na madai hayo nilishangazwa hatua ya askari mmoja ambaye anaitwa Mrisho kwa kuanza kunitukana matusi ya nguoni na kudai kuwa mimi nimejifanya mjuaji na kupitia gazeti la Tanzania Daima na blogu ya Francis Godwin nimeonyesha tukio la wao kuwapiga mabomu wanafunzi hao na tukio jingine alilonihusisha ni lile la madai ya polisi kudaiwa kumpiga kwa risasi mwanamke mmoja mkazi wa Don Bosco " Pamoja na askari huyo Mrisho kutishia kuwa angempiga sana ila hakuweza kufanya hivyo baada ya kuwasiliana na wakuu wake ambao wamemtaka asinipige wala kunitesa kwa namna yeyote ile.


  Baada ya kukamatwa nikiwa eneo la shule hiyo alipelekwa kituo kidogo cha polisi Tosamaganga na baadae kupakizwa katika gari iliyokuwa na askari wa FFU zaidi ya 10 huku wakipiga king'ora mfano njia nzima na kumfikisha kituo cha polisi mfano wa jambazi sugu amekamatwa na baada ya kufika mkuu wao aliagiza niwekwa mahabusu bila maelezo kwa zaidi ya masaa mawili.

  Majira ya saa 12.49 ndipo mwandishi wa habari za Chanel Ten mkoa wa Iringa Daud Mwangosi na mwandishi wa gazeti la Majira mkoa wa Iringa Eliasa Ally walifika kituoni hapo kwa ajili ya kuniwekea dhamana na ndipo nilipotoa maelezo yangu kuelezea mazingira ya kukamatwa japo katika maelezo hayo sehemu ya kosa haikujazwa chochote zaidi ya askari aliyokuwa akichukua maelezo kudai kuwa kosa ni kuwaonyesha wanafunzi hao zaidi ya 1000 askari wawili wa upelelezi na dhamana ya shilingi milioni 1 ipo wazi.

  "Nikiwa ndani ya gari ya FFU baadhi ya askari walikuwa wakinihoji ili kujua kama ni mfuasi wa Chadema na kuwa wao walielezwa kuwa nimetumwa na Chadema katika shule hiyo huku wengine wakitoa vitisho kuwa yaliyompata Jerry Muro na Said Kubenea ndio wanayotaka kunifanyia mimi"

  Maelezo ya polisi na yale ya kamanda wa polisi mkoa kwa vyombo vya habari yalionyesha kutofautiana baada ya polisi kudaiwa kuwaonyesha wanafunzi askari wa upelelezi na kuhatarisha maisha yao huku kamanda wa polisi akidai kuwa sababu ya kushikiliwa na polisi ni kuchochea mgomo wa wanafunzi.

  "Hata nawashukuru wanahabari ndani ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kwa kulishughulikia suala hilo kwa uzito wake pamoja ....pia namshukuru mkuu wa polisi wilaya (OCD) Semunyu kwa kuniachia huru na kunitaka kuendelea na kazi yangu kwa amani"
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,946
  Trophy Points: 280
  hawa askari si ndio wanaishi kwenye mabanda ya mabati?
   
 3. n

  niweze JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania inaendeshwa na sheria za kikwete na jeshi. Watanzania bado hatujua na kukubali haya na matokeo yake sio haya tunaona sheria zilivyo na zinavyofanya kazi. Tufanye kazi kubwa sasa kuziondoa kwa nguvu kuanzia leo na wiki hii nzima.

  Fundisho la kikwete ndio wiki hii mjulishe mwenzio na hakikisha uwajulishe hata ndugu zako kwenye jeshi la polisi waelezeni wasiende kazini wataajiriwa upya kwenye serikali mpya ya Tanzania baada ya serikali mpya.
   
 4. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Pole sana mkuu ila naona kama umeandika kuhusu mtu mwingine na sehemu nyingine umeandika kwamba ni wewe so hapo sijaelewa ila zaidi pole sana, na huyo askari kama angekuwa mwenyewe ungemchapa makonde tu maana hawana adabu kabisa..........
   
 5. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Ndio hao hao....
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Duh, pole mkuu. Kwa mtu ambaye hajawahi kukutana na mkono wa polisi daima atawatetea polisi kwamba wanafanya kazi nzuri. Lakini kwa mtu kama mimi niliyewahi kukamatwa bila kosa, nikalala rumande na siku ya pili nikatolewa kwa hela, ninawachukia polisi kupita kawaida. Maana huwa sioni kabisa msaada wao zaidi ya kuongeza foleni za magari tu wanapoamua kujifanya taa za barabarani. Yaani polisi wa tanzania ni aina nyingine ya majambazi tunaotakiwa kuanza kukabiliana nao. Maana wanashindwa kukamata vibaka na majambazi wanaishia kukamata watu wasio na hatia na kuwaua pamoja na kuwasababishia stress zisizo za lazima.
   
 7. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  pole sana mkuu!!
  ipo siku, inshallah!!!
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Pole sana God
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu. Ila uliyemtaja kwenye heading ni tofauti na unayemzungumzia.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hizi sera za utanda wazi ni porojo au ni mask? Kama vyombo vya dola vinafanya haki kwa nini vizuie vyombo vya habari kufuatilia habari za matukio?
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Yeah mkuu ni vizuri kama angechange heading maana hata mimi hapo juu sijamuelewa vizuri.....
   
 12. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pole sana kaka Mungu akutie nguvu na hiyo iwe filimbi ya kusonga mbele kwa haki zaidi; hakuna historia inayoandikwa kwa mtu kuwa lelemama au goigoi; ndio maana hata akina kimweri; kinjekitile na wengineo wanakumbukwa maana walisimama imara bila kujali; after all hata wenye mibunduki watakufa tena kifo kibaya tu siku moja huenda wakakuacha au ukawaacha njia ni moja; pole sana mkuu
   
 13. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Godwin ukiona hivyo ujue ujumbe umefika na since unafanya kazi kwa Maslahi ya Watanzania songa mbele tupo nyuma yako na kazi yako tunaikubali sana.
   
 14. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  Polisi wanajifanya kana kwamba wao wana ishi maisha standard sana, kumbe wanaishi kwenye mabanda ya kufugia njiwa tena vyumba vyenyewe utazania ni gest.

  Wao wanafanya kazi kwa minajiri ya mafisadi na hamna wanacho faidi. Wakimbizi wa kule ngala wanaishi sehemu nzuri kuliko hawa mapolisi wetu.
   
 15. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii andika barua kwa KOVA. Alafu tutaendelea kufuatilia hili swala kwa hali na mali...
   
 16. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais JK anaendekeza udini.
  Watu wanauwawa TARIME,MBEYA na ila haimuumi kwa sababu wanaokufa si waislam wenzie

  Maeneo hayo yana wakristo kwa wingi so ni sawa kabisa kusema rais haumizwi na vifo vya wasio waislam.
  Alipokufa sheikh yahya (mtu mmoja ) rais alihudhuria mazishi kisa UISLAM.

  mimi ni CCM damdamu ila sipendezwi na move za udini wa JK.ikilazimu ntahamia NCCR
   
 17. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  ..aluta continua, ukombozi umekaribia, soon uta-enjoy harakati zako mkuu, siwezi kukupa pole, ila nakuomba uzidishe harakati!!!!
   
 18. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Pole mkuu,tuko pamoja
   
 19. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Polisi ni kama mbwa tu, wameumbwa kwa ajili ya kukimbia kimbia na kukimbiza binadamu wenzao, siamini kamawana uwezo wa kufika hata kwenye hii mitandao ya kijamii, watu wana lala nje maisha yao yote hawana tofauti na wanyama, ni heri walipwe misha hara duni ili wasijikimu kimaisha waendelee kuzaa mapolisi wenginie sidhani kama kwa msha hara wao kama wana hata uwezo wa kusomesha watoto wao, wana ishi kwa rushwa tu hawa, na kutii amri. Its only dog that he who obey, they dont get time to value their opinion
   
 20. p

  pointers JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  pole sana mkuu ukitaka kujua jinsi askari wetu wanavyotumia tumbo kufikiri badala ya ubongo ndo hapo
  kama traffic anaweza kuacha eneo lake la kazi na kuhangaika na mtu mmoja siku nzima na kuacha wengine wakivunja sheria
  kisa tu anataka sh elfu 10 ,,,,,
   
Loading...