Four cylinder Vs six cylinder

Hiyo ni kweli kabisa ndio maana injini ya 3s ya rav 4 au Noah sr40 ukiangalia ulaji wake wa mafuta hautofautiani sana na injini ya 1G ya GX 100 au GX 110 ya mark 2 lakini watu wengi hawalijui hilo ila wanachoangalia ni six tuu
ebu fafanua vizuri mkuu.
 
Six cylinder ina nguvu sana na inakimbia kukiko 4 cylinder! Na six cylinder inakunywa mafuta madogo kiasi ukilinganisha na 4 cylinder.
Tengeneza scenario vzuri mkuu, sijakupata unachomaanisha
 
Siyo nadra, hilo halipo!!! Huwezi kukuta gari mbili zenye idadi tofauti ya cylinder lakini CC ni sawa!! Hivi vipimo viko standard!!
kwann usikute ...suzuki 2nd generation kuna 2000cc v6 na third generation kuna 2000cc i4 ....
 
Na engine ya 3s au 5L sjui, ni nn hivi vitu au ndo cylinder zenyewe??

VVTI nayo inatajwa sana na wanunuzi, tuwekane sawa ni kitu gan?
 
good pia six mara zote huwa haitoi muungurumo mkubwa km four na hii inachangiwa na kuwa na cyrinder nyingi zaidi ya gari zenye four. chukulia mfano pikipiki yenye piston moja au mashine ya disel yenye piston zilivyo na kelele
Kwa maana hiyo treni labda haina cylinder kabisa....mbona inakelele nyingii
 
V6 Haitoi mlio kivipi mkuu, wakati hizo engine ndio huwa zina mshindo mkali mno kuliko v4. Mfano mlio wa gx100/110 ukilinganisha na mlio wa corrolla limited?
v4 v6 ....hizo "v' zinamaanisha ni idadi ya piston au?
 
Na hapa ndipo penye hoja ya fuel consumption na sio idadi tu ya cylinders bali pamoja na ukubwa wa hizo cylinders na technology inayotumika katika generation ya nishati kuzungusha crank shaft.
Ukubwa wa cylinder nao tunaujuaje sasa wakat wa kuchagua gari? Au tuseme cylinder ndogo kabisa na kubwa kabisa vipimo vyake vinasomekaje kama unajua mkuu
 
v4 v6 ....hizo "v' zinamaanisha ni idadi ya piston au?
V ni mpangilio wa piston katika cylinder block.

Actually hamna mpangilio wa V kwa piston 4. Isipokuwa kuna kwa piston 6 zilizo na mpangilio wa v
 
Mkuu nimekuelewa sana, otherwise mleta mada atuambie piston zinatofautiana ukubwa
 
5.7L hii inamaanisha nn kitaalam
 
5.7L hii inamaanisha nn kitaalam
Samahani mkuu; gari langu lilinunuliwa Marekani ambako ukubwa wa injini zake unapimwa kwa lita (L), siyo kwa cubic centimeters (cc). Wewe badilisha kutoka lita kuwa cubic centimeter utapata uhusiano.
 
Hizi nondo safi sana kwa kupata japo basics knowledge ya magari..hongera mtoa post..ngoja tuchimbe kdg na sisi!
 
Ukubwa wa cylinder nao tunaujuaje sasa wakat wa kuchagua gari? Au tuseme cylinder ndogo kabisa na kubwa kabisa vipimo vyake vinasomekaje kama unajua mkuu
Ukubwa wa cylinder unapimwa kwa cubic centimeter (cc) ikiwa ni diameter ya bore ama kipenyo cha kinu husika kinachokabili mshindo wa cylinder katika mchakato wa kuchoma mafuta.

Kila cylinder ina mzunguko wa kupanda na kushuka katika kinu chake mithili ya mtu anavyotwanga kisamvu kwenye kinu isipokuwa tu cylinder inakuwa iko direct proportional na kinu chake kwa vipimo so its almost inagusa kingo za kinu haichi nafasi pembeni.

Sasa ishu ya cc ndio hasa inadetermine ukubwa wa cylinders. Kivipi?
Mfano gari inayoandikwa V6 with 3.5L ina maana hii gari ina cylinders 6 zenye jumla ya cc 3500 zilizo katika mpangilio wa V kwa maana tatu zimelala kulia na tatu zilizobaki zimelala kushoto katika angle ambayo zikipishana zinatengeneza umbile la herufi V.

Katika hizo cc 3500 kila cylinder bore inabeba kiasi flani cha mafuta. Ili kupata namba kamili utachukua 3500 gawanya 6 kisha utapata kiwango cha mafuta ambacho kila cylinder bore inabeba. Hesabu itakupa ni kama cc 583.3 kwa cylinder moja.
 
Very professional,nice.
 
Hii nimeielewa kabisa. Inamana gari zenye cc sawa ila idadi ya cylinder tofauti inamana yenye cylinder chache itakua ina nguvu kubwa, speed ndogo na tutegemee kwamba kwenye safar ndefu itakunywa sana mafuta coz itatumia muda mrefu kufika but inafaa kwa safar fupi za mjin
 
Hivyo kama zote zina cc zinazolingana basi ile ya 4 cylinder itakuwa na inachoma mafuta mengi kwa kila piston moja ukilinganisha na piston ya 6 cylinder.

Cylinder 4 mafuta mengi kwa kila piston lakini ina piston chache. Kwa hiyo bado hakuna conclusion engine ipi itatumia mafuta mengi zaidi.
 
Hewala, gari ikiwa na cylinder chache inatumia nguvu sana kwenye kupata speed kubwa hivyo mafuta mengi yatalika ili kuipata speed kubwa tofauti na gari yenye cylinder nyingi hivyo haifai sana kwa matumizi ya mwendokasi.

Pia gari yenye cylinder kubwa haitatumia nguvu sana kupata speed kubwa/kuchanganya na hivyo haitakula mafuta mengi ikiwa kwenye speed tofauti na yenye piston chache. Hivyo ina ufanisi zaidi kwenye speed kubwa zaidi kuliko kwa uendeshaji wa speed ndogo.
 
cumins!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…