RIP Mahundi, Jeshi la polisi lilikuwa na utendaji mzuri. Ni utumishi uliotukuka. Mwenyez Mungu awape nguvu wanafamilia waweze kupita katika kipindi hiki kigumu
MWILI wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali mstaafu Haruni Mahundi unatarajiwa kuagwa keshokutwa katika Viwanja vya Karimjee na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi hayo, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova alisema jana kuwa shughuli za mazishi zitaanzia Karimjee ambapo kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana zitatolewa heshima za mwisho.
Kova, ambaye pia ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alisema viongozi mbalimbali watakuwepo Karimjee na zitaendeshwa shughuli za dini na kijeshi ambapo pia kutakuwepo gwaride rasmi.
Mahundi alikuwa IGP kwa miaka 10 na amefariki akiwa na umri wa miaka 72. Alifariki ghafla Jumatatu wiki hii
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.