Former IGP Harun G. Mahundi IS NO MORE

R.I.P mh Harun Mahundi, Ulikuwa na utumishi uliotukuka wakati ukiwa bado unalitumikia taifa, M/Mungu akulaze mahali pema peponi, nawapa pole sana wafiwa wawe na moyo wa subira, katika kipindi hiki kigumu.
"Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Hakika kwake tutarejea" Ameeeen.
Hivi alikuwa IGP kipindi cha Mzee Ruksa au,pamoja na yote RIP mzee wa kunyumba
 
RIP mzee Mahundi

Jamani poleni sana wanafamilia, ni mwaka juzi tu hii familia ilimpoteza mama yao mpenzi.
Pole sana Flora, Francis, John na Grace, Mungu awape nguvu .
 
R.I.P Mahundi

Duh msiba mzito kwa familia. Nakumbuka Mwanae Agatha Mahundi aliyekuwa Mke wa Kijana wa Familia ya Mkwawa Mhe. Kassim Mkwawa (in Charge Temeke RMS Court) alifariki mwaka 2005 kwa ajali ya Moto pale Sinza.

Mwaka 2010 Mkewe Mzee Mahundi alifariki dunia pia.
sasa Mzee, poleni sana, John Mahundi, Grace Mahundi na Flora Mahundi (Mrs. R. Maabadi)

[h=3]RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA IGP MSTAAFU HARUN MAHUNDI[/h]



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta-Jenerali Saidi Mwema kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Inspekta-Jenerali Mstaafu Harun Mahundi (pichani).


Marehemu Harun Guido Mahundi ambaye alikuwa Inspekta-Jenerali wa Polisi kwa miaka 10 kuanzia mwaka 1985 amefariki dunia leo, Jumatatu, Aprili 2, 2012, mjini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 72.


Katika salamu zake za rambirambi kwa Inspekta- Jenerali Mwema, Rais Kikwete amesema kuwa ameshtushwa na kuhuzunishwa na habari za kifo cha Marehemu Mahundi ambaye katika enzi za uhai wake alikuwa mtumishi mwaminifu, mwadilifu na wa kutumiwa wa umma.


“Nimeshtushwa na huzunishwa na habari za kifo cha Marehemu Mahundi ambaye katika enzi zake nilimfahamu kama mtumishi mwaminifu, mwadilifu na wa kutumainiwa wa umma,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Tokea alipojiunga na Jeshi la Polisi kama Konstebo mwaka 1960 hadi utumishi wake kama Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha na hadi kuteuliwa kwake kuwa Inspekta-Jenerali wa Polisi, Harun Mahundi alithibitisha kuwa mtu wa kuaminiwa katika jamii na katika utumishi wa umma.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Alikuwa pia mfano mzuri wa kujiendeleza katika maisha kama alivyofanya wakati aliposomea na kupata shahada ya sheria mwaka 1978 akiwa ndani ya utumishi wa umma. Hata baada ya kustaafu Jeshi la Polisi aliendelea kuwa mfano wa kuigwa katika jamii katika nafasi zake nyingine kama Kamishna wa Tume ya Uchaguzi na mwanasheria wa kujitegemea.”
Rais amemwambia Inspekta-Jenerali Mwema: “Nakutumia wewe binafsi na kupitia kwako kwa Makamanda na askari wa Jeshi zima la Polisi salamu zangu za rambirambi kufuatia kifo cha Mzee Mahundi.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Aidha, kupitia kwako, naomba uniwasilishie salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia yote ya Marehemu Mahundi. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa na kuwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Wajulishe pia kuwa naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze pema peponi roho ya Marehamu. Amen.”
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
02 Aprili, 2012


download
Dear Members,
It is with deep regrets that we inform you of the untimely death of Tanganyika Law Society (TLS) member Mr. Harun G. Mahundi (Advocate), Roll Number 130. The late Mahundi died today at his home in Tegeta.
The family is currently making funeral arrangements; we will communicate this information to you via e-mail and SMS as soon as it becomes available to us. In the meantime let us all offer our support to the family of our dear colleague, Mr. Harun G. Mahundi, during this time of grief.

MAY THE ALMIGHTY GOD REST HIS SOUL IN ETERNAL PEACE, AMEN.

 
R.I.P mh Harun Mahundi, Ulikuwa na utumishi uliotukuka wakati ukiwa bado unalitumikia taifa, M/Mungu akulaze mahali pema peponi, nawapa pole sana wafiwa wawe na moyo wa subira, katika kipindi hiki kigumu.
"Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Hakika kwake tutarejea" Ameeeen.

Utumishi wake kwa taifa hili ulikua wa kutukuka na mwenyezi Mungu ailaze roho yake peponi amina.
 
Pumzika mkwe wangu....japo ulikataa nisimuoe binti yako kwa vile nina madabwada ,lakini mwanga wa milele uangaziwe wewe mstaafu...Tutakutana paradiso......
Alijua wewe jambazi la mapenzi.
RIP Harun Mahundi
 
RIP Mr Mahundi.

Grace (my former classmate) poleni sana wewe na familia yenu wote.

Mzee Mahundi tokea ateuliwe na hayati JK Nyerere wakti ule wa 1985 hakuwa na makuu na nakumbuka Grace ni siku moja moja mlikuwa mkipanda gari ya kazini kwa mzee wenu. Alitaka mfahamu kuhusu kuishi maisha ya kawaida na mlielewa hivyo.

Mungu awabariki sana.
 
Watu na Wana JF,
Poleni sana Familia ya Marehemu Mahundi, Kazi ya Mungu haina Makosa, tumshukuru kwa kila Jambo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa na Jina la Bwana na lihimidiwe
Amina Amen Amein
Nawakilisha


Kuna taarifa zimenifikia kuwa former IGP Harun G. Mahundi is no more,

Amefia nyumabani kwake tegeta, usingizini, ilijulikana baada ya kuona mzee hajaamka muda wake wa kawaida ndio dereva akaomba msaada wa polisi kuvunja mlango,

will come back with more shortly.
 
Retired Mzee Mahundi alikuwa anaishi Mikocheni, ila ana nyumba kadhaa jijini Dar, jana alikwenda tegeta katika moja ya nyumba zake kuiangalia akiwa peke yake, hakurudi nyumbani kwake hali iliyopelekea wasiwasi kwa walio nyumbani kwani pamoja na kuwa na nyumba kadhaa yeye anaishi katika nyumba yake moja tu ya mikocheni, leo alipotafutwa hakupatikana hali iliyosababisha polisi kuanza kumtafuta na baadaye kumpata dereva wake bwana Ngonyani ambaye alihisi huenda alikwenda tegeta baada ya kuwasiliana na watu wa kwenye familia, polisi walipofika tegeta walikuta gari lake nje na walipofingua mlango walimkuta Inspekta Jenerali Mstaafu akiwa amefariki huku akiwa ameketi katika kochi, baada ya hapo uchunguzi ulianza na hadi sasa hawajatoa taarifa rasmi ya kifo hicho japo taarifa za awali zinaonyesha kuwa amekutwa amefariki huku kukiwa na matapishi sehemu aliyoketi
Marehemu alipoteza mkw wake mwaka jana nchini India baada ya kufanyiwa operationa ya saratani ya titi katika hospitali ya Mbezi na baadaye kuleta complication iliyompeleka India ambapo alihudhuria matibabu lakini alipoteza maisha akiwa huko
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi Amina
 
Back
Top Bottom