Ok - labda kwanza tujaribu kuongelea ufanisi wa programs hizi...
Wiki chache zilizopita niliangalia show mmoja ya Oprah iliyokuwa inazungumzia jinsi these kids ambao wapo kwenye kids club moja ya Oprah walivyo safiri all the way to Kenya kwenda kujenga madarasa. Hawa watoto walijitolea, na walijenga madarasa mawili kwa mikono yao mwenye. I am talking about 15 - 17 year old kids.
Sasa hebu niambieni kweli tunashindwa kuwatumia Form 6 leavers (ambao ni at least miaka 19+) kujihusisha na ujenzi/ukarabati wa institutions zetu.
Nnakufahamu mkuu,
Lakini hawa vijana hawana skills kama za ujenzi na wanachofanya ni kushiriki shughuli zile ili zimalizike katika muda uliopangwa.
Jambo jema ni kwa serikali kuwalipia gharama za mafunzo ya skills yoyote iwe umeme na ufundi magari kwani si VETA ipo?
Suala hapa ni vipi fwedha za kuwahudumia wananchi zikiwemo fwedha za mikopo yenye riba nafuu zinatumika.
Nikupe mfano wa Ulaya, mtoto anapomaliza A level tayari anakuwa anajua anaenda chuo kikuu kama amefaulu na hata kama hana uwezo atakopeshwa fwedha hizo ambazo always zipo kwa ajili hiyo na sio malumbano.
La sivyo kama kuna mapungufu basi itabidi asome foundation degree ili afanye kazi akiwa chuoni ambapo anakuwa amekaa kwa miaka miwili tu.
Sasa anapomaliza chuo tayari ana nafasi pale alipokuwa akifanya mafunzo.
Pili serikali inayojali watu wake inakuwa imeelekeza funds katika makampuni au viwanda ambapo vijana huweza kwenda kupata mafunzo ya kazi na kuwa na skills zinazohitajika kujisaidia kimaisha.
Hapa nimeongelea suala la wale wa A level tu, kuhusu GCSE ambapo ni sawa na form 4 wa Tanzania, akimaliza shule ana options nyingi tu kwani kuna vyuo lukuki katika kila tarafa zenye kutoka mafunzo mbalimbali kama ushonaji, kutengeza nywele na hata mambo ya muziki.
Kijana anapomaliza kozi yake anajaribu kuingia ofisi zenye funds maalum kwa ajili ya vijana wanaomaliza mafunzo fulani na kuwapa mshiko wa kuanzisha biashara anayotaka.
Hapa nnazungumzia kijana ambae tayari pia amejifunza kutengeneza business plan au atapata msaaada wa kutengeneza moja.
Kwa hio tunakuwa tunarudi kulekule kwamba bila kudhibiti mambo kama EPA na kodi inayokusanywa kutwa kucha, basi fwedha za kusaidia watanzania haziwezi kuonekana.