Quemu
JF-Expert Member
- Jun 27, 2007
- 984
- 132
Hivi karibuni nimekuwa najiuliza ni vipi nchi yetu inaweza kushirikisha vijana waliomaliza Form VI katika maendeleo ya jamii. Vijana wamalizapo Form VI huwa wana gap ya zaidi ya miezi nane kabla hawajapata nafasi ya kujiunga vyuoni kwa masomo ya juu. Sasa je, tunawezaje kuwashirikisha vijana hawa kwenye maendeleo chanya ya jamii, badala ya kuwaacha wamezubaa tu majumbani wakisubiri muda wa kwenda vyuoni?
Mpaka mwanzoni mwa miaka ya tisini, watahiniwa hawa walikuwa wanakwenda kwenye mandatory army service. Lakini kwa sababu zilizotolewa wakati huo (sizikumbuki), hii service ilikuja kuvunjwa. Matokea yake, vijana wengi hawa wameishia kurandaranda tu mitaani, wakisubiri nafasi za kujiunga vyuoni.
Sasa basi, kwa sababu tuna institutions nyingi mno kwenye jamii ambazo zinahitaji marekebisho ya hapa na pale. Na kwa sababu mahitaji haya hayako kwenye priorities za serikali yetu. Na kwa sababu tuna vijana ambao pengine wana nguvu na muda wa kuanza kulitumikia taifa, kwa hiyo ..
Ningeshauri serikali ianzishe programs ndogo ndogo ambazo zitawahamasisha vijana hawa kujihusisha na ujenzi wa jamii (community service programs). Natumia neno jamii badala ya taifa kwa sababu lengo ni kuanzisha programs ambazo zitawashirikisha vijana hawa kwenye ujenzi wa institutions zinazowazunguka. Of course, jamii ndio taifa lenyewe hilo.
Mfano, kuna institutions kama shule na hospitali/zahanati ambazo zinahitaji marekebisho ya mara kwa mara. Shule mara nyingi zinahitaji upanuzi na ukarabati wa madarasa (ujenzi, upigaji rangi, utengenezaji wa mazingira, n.k.), pamoja na utengenezaji wa madawati, ubao wa kuandikia na vifaa vingine muhimu. Hospitali/zahanati huwa zinahitaji upanuza na ukarabati wa majengo, pamoja na utengezanaji wa vitanda vya wagonjwa na vifaa vingine muhimu.
Sasa basi, kinachotakiwa kufanyika ni kutumia muda na nguvu za vijana hawa katika utekelezaji wa ujenzi wa institutions hizo. Mimi ningependekeza muswada ambao utatunga sheria ambayo itakuwa ni mandatory kwa Form VI Leavers wote kujishirikisha kwenye community service programs kama nilizozitaja hapo juu. Vijana hawa watapaswa kutumia muda wao (kati ya miezi 3 6) kushiriki kwenye community services katika jamii zinazowazunguka. Mfano, vijana wanaomaliza kidato cha sita kwenye shule zilizopo wilaya ya kinondoni, watalazimika kujishirikisha kwenye ukarabati wa institutions zilizoko kwenye wilaya hiyo.
Kwa kutumia njia hii, tutaona kwamba institutions nyingi katika jamii zitakuwa kwenye hali mzuri muda wote. Hii itasaidia kuondoa ukiritimba unaosababishwa na kusubiri huduma za serikali (ngazi zote) katika jamii zetu.
Jamani naomba kuwasilisha!
(NB: Nimejaribu kutafuta njia ya kufupisha bandiko hili, lakini nimeshindwa... Mtanisamehe)