Forex Trading yaanza kufundishwa rasmi chuo kikuu

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Habari wasakatonge wenzangu.

Leo asubuhi nilikiwa ghetto maeneo ya Troyes street hapa jijini Pretoria. Nikaona isiwe tabu ngoja nizame mitaa yangu ya zamani nijaribu kicheki na washkaji wa kitambo hiko enzi napiga kitabu huku.

Nikaingia zangu mtaani kwenda kwenye ukumbi wa matamasha wa Miriam Makeba. Kufika nikakuta pako tupu nadhani ni sababu za korona.

Badala yake nika spot wanafunzi kadhaa kona ya ukumbi wakiwa kwenye discussion.

Kuwauliza wanafanya nini pale wakasema wamejiunga na kozi ya masuala ya fedha kwaiyo ndio wana jadili na kuisoma vyema. Walishindwa kunitajia labda walitambua kuwa mimi ni mgeni na pengine sifahamu chochote kuhusu forex.

Kichungulia kioo cha laptop zao nikagundua wanasoma kozi ya Forex Trading inayotolewa kama kozi fupi na chuo kikuu cha Afrika ya kusini yaani UNISA (University of South Africa).

Siku nyingine ntawaleteeni experience yangu kabambe kipindi nasoma hapa UNISA.

Nikawauliza 'Kumbe UNISA wanatoa mafunzo ya FX?'. Wakajibi " ndio kwani nawe pia wafahamu kuhusu hii biashara?" ..Nikawajibu "Ndio, nimekuwa nikifanya FX Trading tangu mwaka 2018.

Wakaanza kuleta swaga za kunitaka nijiunge nao kudiscuss. Nikawadanganya kuwa naenda kumuona mke wangu hospital ya Arrie Ned Eastwood Park ambaye anatarajia kujifungua.

Note:- Vijana dunia inabadilika kwa kasi sana. Jitahidi uenende nayo kwa kasi. Sidhani kama kuna chuo duniani kinaweza kutoa mafunzo ya "KUBET"

Forex is taking over the space now

20210323_155930.jpg
20210323_155932.jpg
 
Bongo hapa forex chuo utasoma tu intro tena ya juu juu sana.....kwa waliosoma international finance au FN basi topic ya kwanza ni forex...humo utasoma bid,ask,spread , option etc...inakua imeisha hyo
Umeenda nje ya mada kidogo. Huenda umeshindwa kusoma vyema, lakini hata picha hujaielewa?
 
Nimeenda nje how...mim nimeongelea scenario hiyo hiyo hapa bongoland kwetu sio huko bonden. Hebu niambie wapi nmetoka nje
Umejaribu kutanabaisha kuwa hata kama ingekuwa inafundishwa bongo isingekuwa inafundishwa kwa namna ipasayo.

Hata hivyo kwanini uwadharau wabongo? Kwani hakuna chuo cha bongo chenye uwezo wa kupata namna ya ushirikiano kutoka UNISA.
 
Umejaribu kutanabaisha kuwa hata kama ingekuwa inafundishwa bongo isingekuwa inafundishwa kwa namna ipasayo.

Hata hivyo kwanini uwadharau wabongo? Kwani hakuna chuo cha bongo chenye uwezo wa kupata namna ya ushirikiano kutoka UNISA..
Aisee umeshindwa kunisoma boss... hebu rudia post yangu vizuri..

Nimeonyesha how bongo tuko nyuma compared na South ndio maana nikasema huku sisi utaishia kusoma bid na ask tu kwenye FN

Kama tukiwa serious basi vyuo vikuu vyetu vitaanza kutoa hii coz... kuna coz pale IFM ya maswala ya investment sijajua module zao zikoje... hope saizi umenielewa
 
Umejaribu kutanabaisha kuwa hata kama ingekuwa inafundishwa bongo isingekuwa inafundishwa kwa namna ipasayo.

Hata hivyo kwanini uwadharau wabongo? Kwani hakuna chuo cha bongo chenye uwezo wa kupata namna ya ushirikiano kutoka UNISA..
Ni kweli wacha ubishi wewe...forex kufundishwa hapa bongo hatuna wataalam ..kwa mtu mmoja mmoja labda uwe umejifunza pekee yako.
 
Ni kweli wacha ubishi wewe...forex kufundishwa hapa bongo hatuna wataalam ..kwa mtu mmoja mmoja labda uwe umejifunza pekee yako

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Umeuelewa uzi.?

Nimejaribu kuweka wazi kuwa forex inafundishwa chuo kikuu huku kwa madiba.

Sijazungumzia habari ya forex kufundishwa tanzania.

By the way. Hata mamlaka zikiamua kuweka fx kwenye mtaala ni rahisi mno. Maana watacho kifanya ni kuiga miongozo ya ufundishaji kutoka vyuo vilivyotangulia kufundisha ilo somo.
 
Ni kweli wacha ubishi wewe...forex kufundishwa hapa bongo hatuna wataalam ..kwa mtu mmoja mmoja labda uwe umejifunza pekee yako

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Hatar mzee wangu..mambo ya capital budgeting.. sio poa
Nina zungumzia forex trading wazee!

Halifanani kabisa na masuala ambayo mmefundishwa madaradani kwenye kozi zenu za vyuo vikuu.

Ni proffesional inayojitegemea na ndio maana ikawa inafundishwa kama short course hapa UNISA.
 
Habari wasakatonge wenzangu.

Leo asubuhi nilikiwa ghetto maeneo ya Troyes street hapa jijini Pretoria. Nikaona isiwe tabu ngoja nizame mitaa yangu ya zamani nijaribu kicheki na washkaji wa kitambo hiko enzi napiga kitabu huku.

Nikaingia zangu mtaani kwenda kwenye ukumbi wa matamasha wa Miriam Makeba. Kufika nikakuta pako tupu nadhani ni sababu za korona.

Badala yake nika spot wanafunzi kadhaa kona ya ukumbi wakiwa kwenye discussion.

Kuwauliza wanafanya nini pale wakasema wamejiunga na kozi ya masuala ya fedha kwaiyo ndio wana jadili na kuisoma vyema. Walishindwa kunitajia labda walitambua kuwa mimi ni mgeni na pengine sifahamu chochote kuhusu forex.

Kichungulia kioo cha laptop zao nikagundua wanasoma kozi ya Forex Trading inayotolewa kama kozi fupi na chuo kikuu cha Afrika ya kusini yaani UNISA (University of South Africa).

Siku nyingine ntawaleteeni experience yangu kabambe kipindi nasoma hapa UNISA.

Nikawauliza 'Kumbe UNISA wanatoa mafunzo ya FX?'. Wakajibi " ndio kwani nawe pia wafahamu kuhusu hii biashara?" ..Nikawajibu "Ndio, nimekuwa nikifanya FX Trading tangu mwaka 2018.

Wakaanza kuleta swaga za kunitaka nijiunge nao kudiscuss. Nikawadanganya kuwa naenda kumuona mke wangu hospital ya Arrie Ned Eastwood Park ambaye anatarajia kujifungua.

Note:- Vijana dunia inabadilika kwa kasi sana. Jitahidi uenende nayo kwa kasi. Sidhani kama kuna chuo duniani kinaweza kutoa mafunzo ya "KUBET"

Forex is taking over the space nowView attachment 1732549View attachment 1732550

Napendekeza Sirjeff aka Ontario awe Tutor au Assistant Professor .
 
Kama imeanza kufundishwa vyuo vikuu basi itaanza kusaidia kuondoa shaka kwa baadhi ya watu wanao ifananisha na "Kubeti".

Tatizo mtu hataki kujifunza mwisho wa siku hela zinaangukia kwa vibaka wa mtandaoni ishu ya forex elimu inahitajika ya kutosha kabisaa ukikurupuka lazma uone kama kubet tu
 
Hizo maforex yenu ni biashara za mabeberu,haziwafai watanzania wanyonge au nasema uongo wajameni, sisi wanyonge tuweke juhudi kwenye kilimo cha kufa na kupona..(. )
 
Back
Top Bottom