Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Coventry nchini Uingereza, wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Irene Glendinning, pamoja na Ukumbi mzima, ulizizima wakati jina la Mtanzania aitwaye Dk. John Pima lilipotajwa wakati wa Mahafali ya wahitimu wa Kozi ya Uzamivu wapatao 11 waliotoka katika Mataifa tisa duniani.
Dk. Pima ambaye alikuwa shuhuda, alieleza kuwa, baada ya jina lake kusomwa ili aende mbele kutunukiwa shahada ya Uzamivu, walipotaja tu John Pima from Tanzania, shangwe ziliibuka wakitaja Magufuli .... Magufuli ... Magufuli ... Tanzania."
Dk. Pima alieleza kuwa, baada ya mahafali, maprofesa na wahitimu wenzake walimfuata na kumuulizia habari za Rais Magufuli wanazosikia kwenye vyombo vya habari wakitaka kujua ni mtu wa namna gani? Wengi walipongeza kasi na msimamo wake wa:
- kukusanya mapato,
- kudhibiti matumizi ya fedha za umma,
- kushughulikia mafisadi,
- ununuzi wa ndege,
- upanuzi wa bandari
- ujenzi wa barabara za juu
- uanzishwaji wa viwanda.