Hii nayo kali. Manyerere na Muhingo sasa waseme tena bisi wao si fisadi wakati wame operate illegally. ROSEMARY MWAKITWANGE anajua mengi na atueleze kuhusu hilo la usajili. na je kwa nini alikimbia NHL?
Madame Rose tuambie!
Nadhani hawakukosea waliomuita King Maker, anaweza hata kutengeneza na viking vidogovidogo.
Kudos ka-inzi
Msanii,we WOS
umeshawahi kuionja ladha yake??? muulize Bangusilo
Its a proof that politics is a dirty game..
here is a political clout cocktail recipe
:Ingredients & Method
Warning coz the cocktail can be deadly:Before you attempt this, make sure the power is well connected and you have the balls!
mix together in a large shaker the main ingredients:
cronism,corruption, abuse of power and authority,shake well
add a little boldness, continue shaking
then wait and see, if no changes in the consistency of the mixture...
add some clean blackmailing,shake even more
then the cocktail is ready for use....
N.B. You can improvise as per your need and taste
Kazi nzuri sana Inzi. Kwa ufupi, hizi paragraph tatu zinaelezea vema yote juu ya nia ya Salva kumuandikia hii barua Rostam.
Fundisho kwetu;Kwa wale wanaotaka JK apewe miaka mingine 5 wajitokeze na kutueleza apewe kwa uzalendo upi alionao?
- Serikali ya JK iliingia madarakani kwa msaada mkubwa sana wa Rostam na wapambe wake. Hivyo JK hawezi kumchukulia RA hatua yoyote licha ya kelele za wa TZ wengi ikiwemo Mengi aliyeamua kujitoa mhanga.
- Kama wengi wa walio madarakani wameingia kwa kujuana na sio sifa za utendaji wao, au hata kama zifa wanazo, watawajibika vipi ili kuendeleza nchi badala ya kutunisha kilichowavutia kwenye utumishi wa nchi yaani vibaba vyao?
- Hivi ni kwa nini JK aendelee kuwa raisi kama yeye na mafisadi ni timu moja?
- Je bunge letu linasemaje au watasubiri mpaka nchi ifilisike au tuchinjane ndio wamchukulie hatua JK?
Kama hii barua ni kweli ya Rweyemamu na ilimfikia Rostam ina maana Rostam ana uwezo wa kumuunganishia kazi mtu akawe presidential spokesman, nimekoma na Rostam Aziz.
By the way, to be the devil's lawyer for a minute, kama ungekuwa ni wewe Kikwete halafu kina Rostam na kina Rweyemamu ndio hao waliku propell into power kama Salva anavyosema humo, ungefanya nini wakija wanaomba na kuombeana kazi, ungejifanya huwajui? Sijui kama Kikwete atapokea tena favor ya mtu uchaguzi wa 2010. Labda 2011 Rais Kikwete hatakuwa mfukoni mwa kina Rostam na CCM financiers wengine.
Naona pia Salva kamtukana Johnson Mwambo kwamba ni "ki-mbwa cha J.U." akimaanisha Jenerali Ulimwengu, maana Ulimwengu ndie kibosile pale Raia Mwema. Salva Rweyemamu mwana haramu, kama ni barua yake hii.
Tatizo ni kuwa tayari tumeshaona ngoma zikipigwa (Mzee Malecela) kuwa JK aendelee kwa miaka mingine 5 tena bila kupingwa.
Kwa alivyoboronga, sidhani kama anastahili hata zaidi ya wiki moja, ila cha kushangaza ni kuwa hakuna mbunge hata mmoja anayezungumzia kumfukuza JK kwa kushindwa kazi, ingawa kikatiba uwezo huo wanao. Hata wale wa upinzani wako kimya kulizungumzia hilo. ..........Why??[/QUOTE]
Hujui kwa nini!! hebu kumbuka JK alivyoenda kulihutubia bunge alichoonge kilikuwa nini?; wengi tulidhani kuwa patakuwa hapatoshi kwamba Rais wa nchi anakwenda kulihutubia bunge. Lakini cha ajabu akaishia kuwaeleza kuwa serikali yake imewaboreshea mafao kwa kuongeza bajeti ya wabunge maradufu. Si umesikia walivyomuwakia Dr. Slaa pale aliposema kuwa wabunge wanalipwa mishahara mikubwa, hivyo inapaswa ipunguzwe. Nani atampinga JK?
unashangaa Salva as a journalist?
Hivi ushasoma kiingereza cha Kubenea? au yule mwandish mwingine anyeishi UK?
Mimi sijaisoma kwa sababu haifunguki, lakini kwa jinsi nilivyofuatilia michango mbalimbali ya wachangiaji wakiwemo ninaowaheshimu sana, hali ni mbaya zaidi kuliko tunavyoiona katika bandiko hilo.
Kama unataka kuamini angalia jinsi serikali inavyopambana na kutisha wa juu ya kuvuja kwa "nyaraka za siri" hii nayo inaweza kuwa moja wapo ya hizo "nyaraka za siri", sijui.
Wataficha sana lakini atakuja kichaa mmoja ambaye atazianika hizo "siri" zao, siwamesema eti nyingine zinachukua miaka 20 kuharibiwa n.k, wajifunze kutoka kwa Obama na jinsi anavyowaanika walioficha uovu wao kwa kutoa memos zao.
Swali, je Tanzania tutafika huko lini? namanisha tutampata Obama wetu kabla ya miaka 20 kupita wasije ziharibu? kama kweli wanafuata huo utaratibu. Manake nimekuwa nikisikia mara file imepotea mahakamani, file imepotea Brela n.k, au ndo zinavyoondolewa/zitavyoondolewa kutoka mfumo rasmi wa kuziona.
Mungu atusaidie watanzania tuamke kutoka katika usingizi huu.
Heshima mbele Enigma
Hivi tuna uhakika gani kama ni kweli ni Salva ndie kaandika yote hayo?