For the IT/Mobile crime security guru

For the IT/Mobile crime security guru

TRACE

Senior Member
Joined
Jul 4, 2008
Posts
120
Reaction score
46
Habari za Jumamosi Wakuu.Nipo hapa kuomba msaada kwa wataalamu kwani hapa ni jungu kuu lisilokosa ukoko.

Nina Ndugu yangu amepoteza Laptop Bag yake ambayo ndani yake kulikuwa na vitu vingine.Walivunja kioo cha Gari na kutoa hiyo bag.

Kati ya vitu vilivyoibiwa ambacho kinaweza kutoa lead kwa upeo wangu ni Modem ya Sasatel ambayo baada ya siku tatu alijaribu ku trace na Sasatel kwa ugumu waliweza kumwambia kuwa ilitumika mara baada ya tukio kuwasiliana kwa njia ya Email.

Najua sio wote wafanyao katika Mobile companies wanauwezo wa kuelewa jinsi ya kum track mtu aliyewasiliana nayo ili tuweze kupata starting point ya investigation ili tuweze kupata na vitu vilivyobakia.

Haiwezekani kama tukipata Email ya Sender na Receiver na kisha tuka trace their IP na other contacts zao au watu wa karibu nao? na kisha kumpata sender?

Ni matumaini yangu nitapata usaidizi katika hili.Nawakilisha
 
Ni possible mkuu.by request from police hao sasatel watakupa details
 
mkuu sijui labda kama hao sasatel wapo juu kuliko Voda, niliibabiwa computer na moderm ya voda nikaenda kuomba wanisaidie kutrace hiyo moderm wakaniambia itakuwa vigumu kama huyo mutu atabadilisha line, nilishangaa sana hapo nimeshawapa EMEI na Serial ya Moderm, hawa batu wa mitandao ni maboga sana!!
 
Haitawezekana unavyofikiri, kwanza I.P ya sender wanaijua sasatel wenyewe. I.P ya receiver probably ni I.P ya Google au ya Yahoo haitakusaidia kitu.

Mwisho Sasatel hawawezi kuwa na I.P ya receiver unless wanarecodi traffic yote inayopita kwenye network yao, yaani bit zote wanazisave, kitu sio tu ambacho ni impractical lakini propably illegal pia. Not to mention baadhi ya email ziko encrypted start to end (Gmail) kwa hiyo hakuna data utakayopata hata ukirekodi traffic.

Kama mwizi anatumia namba ya Sasatel kufanya mawasiliano basi Sasatel ndo wantakiwa wawe na rekodi ya namba ni ya nani, namba zote si zimesajiliwa?
 
Kama unayo IMEI na bado Inatumika inawezekana sana kumpata hata kama atabadili line, shida ni kama ataamua kubadilisha modem hapo utakua umepoteza, polisi na hata hao sasatel wanaweza kabisa kutrace, sema tu process yenyewe ni very involving na chances za wao kukupa majibu ya kukukatisha tamaa ili uachane nayo ni kubwa
 
Back
Top Bottom