nkyalomkonza
JF-Expert Member
- Jun 18, 2012
- 1,154
- 444
Hizo zinasubiri pesa za Wahisani. Budget haina maana kuna Cash. Na Hilo ndilo tatizo la nchi hii, mwaka utaisha na hakuna pesa zitakazotoka.Kumbuka kuwa Marekani mmeshawaudhi kwa kuweka Bendera kwenye Meli za Magaidi.Uingereza wanasubiri na wewe ukubali kuwa Shoga ndio wakupe msaada, Labda utuhaidi kwamba unakubaliana na masharti yao.Wadau,Serikali yetu sikivu, kupitia chama kilichopewa ridhaa ya kuongoza nchi na wananchi weengi, imetangaza bungeni kupitia jemedali MAGUFURI kuwa pesa zimetengwa kwa ajili ya flyover Tazara.Tuiunge mkono serikali ya JK katika kutimiza ahadi.:israel:
Tunajadili ahadi zinazoendelea kutolewa. Tunataka kuona yakitendeka.Kwani hapa tunajadili nini?
Wadau,
Serikali yetu sikivu, kupitia chama kilichopewa ridhaa ya kuongoza nchi na wananchi weengi, imetangaza bungeni kupitia jemedali MAGUFURI kuwa pesa zimetengwa kwa ajili ya flyover Tazara.
Tuiunge mkono serikali ya JK katika kutimiza ahadi.:israel:
Wadau,
Serikali yetu sikivu, kupitia chama kilichopewa ridhaa ya kuongoza nchi na wananchi weengi, imetangaza bungeni kupitia jemedali MAGUFURI kuwa pesa zimetengwa kwa ajili ya flyover Tazara.
Tuiunge mkono serikali ya JK katika kutimiza ahadi.:israel:
Kwani katika jiji zima la Dar wameona junction ya Tazara tu. Vipi ubungo na junctions nyingine kibao zilizopo Dar na hata kwenye majiji mengine?
Hizo wamemuachia nani? Nafikiri wamewaachia chadema waje kuzifanya 2015. Na hiyo flyover ni lazima itajengwa chini ya kiwango maana fedha ni lazima ziliwe. Embu angalia Kilwa road jinsi ilivyooza na ni barabara ya juzi tu.
Ninaiambia serikali kwenda kujifunza kwa wakenya na Waethiopia. Sio kutuletea maendeleo ya "peremende danganya toto"
Watu hamna jema humu khaa! mfanyiwe lipi mpende?
1. Kwamba Kigoma itakuwa ndo dubai ya Tanzania na watajengewa uwanja wa ndege wa kimataifa
{Terminal Three hapo dar Imeshakamiliki si unaona ma AirBus yanavyoshuka hapo}
2. Kwamba Ziwa victoria watanunuliwa meli kubwa mpya
{Meli Dar/zenji zimeshatosha kwani mkondo wa Numgwi ushasikia tena umelamba meli}?
3. Kwamba Folen Daslam itakuwa historia
{Kwani Ipo}?
4. Kwamba Mgao wa Umeme utakuwa Historia
{Kwani ushauona Mgao wewe kwenye awamu hii ya Ari na Kasi na Nguvu}?
.
.
.
.
.
.
na kadha wa kadha
Hapo kwenye Red mkuu umeniongezea machungu. Kweli Watu wa Kagera, Mwanza, Mara na Shinganya tukimchagua hata mbunge Mmoja kutoka CCM mwaka 2015 kweli tutakuwa hamnazo!!!
Wadau,
Serikali yetu sikivu, kupitia chama kilichopewa ridhaa ya kuongoza nchi na wananchi weengi, imetangaza bungeni kupitia jemedali MAGUFURI kuwa pesa zimetengwa kwa ajili ya flyover Tazara.
Tuiunge mkono serikali ya JK katika kutimiza ahadi.:israel:
Kutengewa budget na kujengwa ni vitu viwili tofauti. Kwani ule bajaji/ pikipiki za kubeba wagojwa hazikutengewa budget? na zinafanya kazi?
Kwanza hii serikali si sikivu kwa sababu wananchi tumeshalalamika mambo mengi sana lakini imekaa kimya, na haikuwekwa madarakani na wananchi walio wengi.
BTW..hizo hela zimetengwa mwaka huu na zitatengwa mwakani alafu mwaka wa uchaguzi ndio mtaanza kujenga which means hela za mwaka huu na mwakani za huo ujenzi zitapelekwa kwenye account zenu huko swiss, uk na sehemu mbali mbali..msitudanganye tumeshaamka siku hizi
Fly over tazara bila fly over ubungo haina maana yoyote ni mzaha tupu. Ni sawa na hiyo barar ya mendo kasi inaishia kimara badala ya mbezi. Wakati siku hizi foleni ya kufa mtu inaanzia kimara kwenda mbezi jioni