Flyover itangulie TAZARA au Ubungo?

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Nimemsikia PM aki-wind up budget speech yake kwa kuzungumzia hatua za kuondoa msongamano wa magari jiji la Dar es salaam. Kasema karibuni utaanza ujenzi wa flyover Tazata, ninalojiuliza wapi kwenye umuhimu na haraka zaidi kujengwa flyover kati ya tazara na ubungo. Ubungo ndiyo barabara kuu ya kutoka/kuingia nchi zote jirani na mikoa yote ya Tanzania kutoa mtwara na lindi. Kutoka morogoro mpaka dar umbali usiozidi 200km ni mwendo wa masaa matatu(3) katika hayo masaa matatu, mbezi mpaka ubungo 11km inachukua saa moja na nusu au zaidi nyakati za jioni. Kuanzia saa 10 jioni kutoka shekilango mpaka ubungo mataa ni zaidi ya saa moja.

kwa maelezo hayo ni dhahiri ubungo mataa ndiyo penye kero kubwa zaidi kuliko crossroad yoyote nyingine jijini Dar, criterion iliyotumika kuanza na Tazara ni ipi? Au mkitoka ulaya(airport) msipate tabu?
 
Flyovers mpangilio kwa umuhimu;
1. ubungo
2.tazara
3.mwenge
4.moroco
 
wameona waanze na tazara ili mapinduzi yatakapowadia 2015 waweze kukimbia mapema njia panda ya ulaya aka airport
 
Jamani kuwa fair kabisa. TAZARA ni sehemu korofi sana kwa uzoefu wangu lakini sababu kubwa ni kutumika kwa askari muongoza magari badala ya Taa za Bararani. Ubungo kwa sasa tatizo ni Morogoro Road,. Mandela Roada sio tatzo sana baada ya kuondolewa kwa Wamachinga
 
Back
Top Bottom