Fly Over za Kenya zatufunza nini Tanzania?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Bongo tumezoea longolongo. Ah mwenzangu maisha bora kwa kila mtanzania mjomba ati. Madaraja ya juu kwa juu ilikuwa kauli mbiu ya Kikwete kwenye kampeni uchaguzi Mkuu uliopita. Kwa sasa imebaki kauli mbiu ya Magufuli isiyotekelezeka bali kauli za kuwazika na kufikirika.

Watani wa jadi ambao ni majirani zetu Kenya ndio watekelezaji wa kauli mbiu za fikra za kuwazika Tanzania na kutekelezeka maisha bora kwa kila Mkenya.

P1030947.JPG

P1030936.JPG

P1030938.JPG

P1030940.JPG

Picha kwa hisani ya Michuzi blog
 
Tangu lini mswahili alipenda maendeleo. Mtu wa pwani anaweza kufanya biashara ya machungwa kwa miaka hata ishirini. Anachohitaji yeye ni faida itakayomwezesha kupata kibaba cha unga na mboga bila kusahau senti kidogo ya kununua kahawa kijiweni wakati wa kucheza bao. Rais wetu ni mtu wa pwani kwa hiyo sishangai kabisa.
 
Umenikumbusha kitu, kupitisha bakuli huku na huko ndiyo mtindo wa uswahilini kutembelea watu maarufu na kupiga huu mwingi kuwalainisha kisha anaondoka na kibaba cha kupitishia siku kwa mswahili inatosha mradi maisha yanakwenda.
 
Hizo Overpass zinatakiwa kuwepo katika makutano ya Ubungo, Mwenge, Tazara, Magomeni na Morocco.
Serikali inashindwa kununua Gloves, bandage, panadol na nyembe kwa madaktari itawezekana kweli hata kuwa na michoro ya Overpass??? Sembuse kuzijenga?

Tunahitaji serikali mpya ya chama kipya chenye watu wenye mawazo ya mlengo mpya yenye maono ya kuona mbali.

Sisi tunisubiri 2015 ili kwa mara nyingine tutumie hahi yetu ya kupiga kura kuiondoa CCM na serikali yake!
Kikwete naye anaisubiri 2015 ili muda wake uishe kwani joto ya jiwe kalioni hata nyani angepiga yowe la nguvu.
 
Kazi tunayo. Hivi kenya wao si wanategemea chai na kahawa tu kuingiza hela za kigeni.

sikujua kama chai na kahawa ina dhamani kuzidi almasi,dhahabu na tanzanite.

Tanzania Tanzania nchi yenye vilaza wengi wakiongoza nchi tajiri.

Umeongea iliyo kweli tupu, sina chakuongeza hapo
 
Tangu lini mswahili alipenda maendeleo. Mtu wa pwani anaweza kufanya biashara ya machungwa kwa miaka hata ishirini. Anachohitaji yeye ni faida itakayomwezesha kupata kibaba cha unga na mboga bila kusahau senti kidogo ya kununua kahawa kijiweni wakati wa kucheza bao. Rais wetu ni mtu wa pwani kwa hiyo sishangai kabisa.

Atauza machungwa hata miaka 50 kihalali kabisa, lakini hawezi leo kuja kushona viatu, kesho ana grocery, keshokutwa bar. Ukichunguza utakuta katika mali ya huyo asiye wa pwani 99% ni haramu tupu.

Nani asiyejuwa hilo?
 
Kuwa na flyover si kipimo cha maendeleo, fungukeni kidogo. Kwa kuwa Paris haina majumba marefu kama Dubai haina maana haijaendelea.
 
Kazi tunayo. Hivi kenya wao si wanategemea chai na kahawa tu kuingiza hela za kigeni.

sikujua kama chai na kahawa ina dhamani kuzidi almasi,dhahabu na tanzanite.

Tanzania Tanzania nchi yenye vilaza wengi wakiongoza nchi tajiri.

nyie wa2 wa bara munajua nini km baba yenu alikuja na kaptura akazikwa na suruali
 
Mnafikiri kujenga fly over ni sawa na kujenga ukuta wa nyumba? Kwa miundo mbinu yetu na ujenzi holela hizo ngumu sana kujenga maana fly over haitakiwi ipite juu ya nyumba za watu, na inatakiwa inyanyuke kwa slope ndogo kuanzia mbali. Mtakubali kuhama mlipwe fidia? Au mtaanza maandamano ? Kipawa tu kupanua airport pale ilikuwa kasheshe watu kuondoka.
 
Kazi tunayo. Hivi kenya wao si wanategemea chai na kahawa tu kuingiza hela za kigeni.

sikujua kama chai na kahawa ina dhamani kuzidi almasi,dhahabu na tanzanite.

Tanzania Tanzania nchi yenye vilaza wengi wakiongoza nchi tajiri.

wana utalii pia mkuu tena kwao wanakuja zaidi ya milioni moja wakati kwetu laki saba na nusu.
 
Kazi tunayo. Hivi kenya wao si wanategemea chai na kahawa tu kuingiza hela za kigeni.

sikujua kama chai na kahawa ina dhamani kuzidi almasi,dhahabu na tanzanite.

Tanzania Tanzania nchi yenye vilaza wengi wakiongoza nchi tajiri.

Mkuu niliwahi kusikia kuwa Kenya ndo wanasifika duniani kwa uuzaji wa Tanzanite! Sisi ni mabomu na kiongozi wetu ni bomu. Nahisi jamaa ana kichwa cha dafu! Natamani watu wa pwani tuwapige BAN kwenye kiti cha urais kwa miaka kama 20 hivi.
 
Tanzania isyokuwa na dira itafikiria jambo lolote la maana kweli; sisi tumeozowea boa liende.
 
Tangu lini mswahili alipenda maendeleo. Mtu wa pwani anaweza kufanya biashara ya machungwa kwa miaka hata ishirini. Anachohitaji yeye ni faida itakayomwezesha kupata kibaba cha unga na mboga bila kusahau senti kidogo ya kununua kahawa kijiweni wakati wa kucheza bao. Rais wetu ni mtu wa pwani kwa hiyo sishangai kabisa.

Mkuu, umempiga marungu makali sana mkuu ya kaya, lakini hebu tukumbuke, rais wetu si ana mawaziri na washauri wengine? They could show him the way.....
 
Hizo Overpass zinatakiwa kuwepo katika makutano ya Ubungo, Mwenge, Tazara, Magomeni na Morocco.
Serikali inashindwa kununua Gloves, bandage, panadol na nyembe kwa madaktari itawezekana kweli hata kuwa na michoro ya Overpass??? Sembuse kuzijenga?

Tunahitaji serikali mpya ya chama kipya chenye watu wenye mawazo ya mlengo mpya yenye maono ya kuona mbali.

Sisi tunisubiri 2015 ili kwa mara nyingine tutumie hahi yetu ya kupiga kura kuiondoa CCM na serikali yake!
Kikwete naye anaisubiri 2015 ili muda wake uishe kwani joto ya jiwe kalioni hata nyani angepiga yowe la nguvu.

Make sure vijana wa mitaani ambao ndio wa kulete haya mabadiliko wanajiandikisha kupiga na KULINDA kura. Otherwise, yatakuwa yale yale ya kumsukuma Mrema then kura hazitoshi.
 
Mkuu niliwahi kusikia kuwa Kenya ndo wanasifika duniani kwa uuzaji wa Tanzanite! Sisi ni mabomu na kiongozi wetu ni bomu. Nahisi jamaa ana kichwa cha dafu! Natamani watu wa pwani tuwapige BAN kwenye kiti cha urais kwa miaka kama 20 hivi.

yes, hii ni kweli. Madini tunachimba wenyewe, na bado tunawauzia wakenya.
The same goes to
1) Mbao za Mufindi and Njombe: exported through Mombasa port, wakenya wanapata foreign exchange sisi tunacheza bao

2) Kahawa ya bukoba: significant ammount is sold through Uganda, which has a significant share on the exported Robusta coffee.

This is the reality of Tanzanians, including you and I!:thinking:
 
Tangu lini mswahili alipenda maendeleo. Mtu wa pwani anaweza kufanya biashara ya machungwa kwa miaka hata ishirini. Anachohitaji yeye ni faida itakayomwezesha kupata kibaba cha unga na mboga bila kusahau senti kidogo ya kununua kahawa kijiweni wakati wa kucheza bao. Rais wetu ni mtu wa pwani kwa hiyo sishangai kabisa.
umenena , mfano mzuri we fikiria tu mkoa wa pwani kama kuna maendeleo, watu wanaishia tu kukaa vibarazani, hawana wanachofanya na kufikilia zaidi ya kuhudhuria ngoma na sherehe za kila wiki.
 
Sisi bado tunashughulikia matatizo ya migomo. Tukimaliza tutaanza ujenzi labda mwaka 2050
 
Mnafikiri kujenga fly over ni sawa na kujenga ukuta wa nyumba? Kwa miundo mbinu yetu na ujenzi holela hizo ngumu sana kujenga maana fly over haitakiwi ipite juu ya nyumba za watu, na inatakiwa inyanyuke kwa slope ndogo kuanzia mbali. Mtakubali kuhama mlipwe fidia? Au mtaanza maandamano ? Kipawa tu kupanua airport pale ilikuwa kasheshe watu kuondoka.

Mkuu kwa hiyo unamtetea boss wako kwamba aliyoyaahidi kwenye kampeni ilikuwa ni uongo tu ili apate kura ila hakuna mpango wa kujenga hizo fly over? Kama Kenya wameweza sisi tunashindwa nini? Kwani Kenya wamewezaje kunyanyua hizo slope ambazo Tanzania hatuwezi? Twambie ni nani amekataa kulipwa fidia ili kutoa nafasi kwa fly over kujengwa?

Usilete story za kwenye kahawa hapa, tunataka hizo fly over ili angalau tuepukane na foleni zisizo za lazima!!!!

Tiba
 
Back
Top Bottom