Fly Over za Kenya zatufunza nini Tanzania?

Kuwa na flyover si kipimo cha maendeleo, fungukeni kidogo. Kwa kuwa Paris haina majumba marefu kama Dubai haina maana haijaendelea.

comment zako mtu akizisoma zitaiakichefuchefu kumbe ndio ulivyo
 
Wakenya wamejengewa na waChina hii kitu. Wakenya wenyewe wasingeweza kusimami huu mradi bila kula pesa yote

Mkuu.. unataka kusema wachina walitoka huko china na kuvamia kenya na kuanza kujenga bila ya wakenya wenyewe kujua..? Point kubwa hapa ni ubunifu na kuweka mbele maslahi ya umma hata kama Kenya inajulikana kwa rushwa.. Linapokuja suala la maslahi ya nchi wakenya hawana mchezo.. Na ndo maana unaona walikaa na kufikiria na mwisho kuja na wazo ambalo sasa limetekelezwa rasmi.. JK alishaahidi hapa flyovers kupunguza misongamano.. na zitaendelea kuwa ahadi kwa sababu that's one thing JK's good at.. Promises..
 
Hata aje malaika kutawala hatutafikia walipo Kenya ambao wao walishakuwa mbele yetu kwa muda mrefu sana tu! Sisi tukiwa mbele ya Uganda lakini leo hii Uganda juu ya matatizo waliyonayo (ya kutokuwa kisiwa cha amani) especial kaskazini wa uganda wanatupita na kutuacha kiuchumi!

Tatizo letu kubwa sana sisi ni wababaishaji vitabu vitakatifu vimesema Mungu atatupa Viongozi tunaofanana nao. Viongozi kwa maana nyingine wana reflect wananchi wao. Tunawapo wasakama viongozi ifike muda turudi kwenye maandiko tuona Mungu amesema nini. Nadhani sisi ndio wenye matatizo makubwa sana na mabadiliko inabidi yaanze kwetu sisi wananchi.

Wakenya kama wananchi ni watu wenye kujituma na wasiobweteka, wana sifa ya kujisomea na kujiendeleza kusoma tofauti na sisi kusoma na kujisomea nio utamaduni tunaoupenda na ndio maana vijana wetu wanaona wakifeli wataendelea na sanaa ya kuimba bongo fleva! Sisi ni wavivu tuliojaaliwa ardhi yenye rutuba lakini wakenya wenye ardhi ndogo wanalima na ku export maua, mboga mbonga na miraa kwenye nje! Ukisikia mtu ana shamba analima mahindi kule shamba basi ujue ni shamba kweli!

Tuache kulalama tupige kazi tumia muda wako wa lunch kupost comments jf piga kazi ili mwisho wasiku viongozi wajisute kuwa wananchi wao ni wachapa kazi na wao inawabidi wachape kazi!

Mawazo ya kizamani haya , kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba mtu akikutangulia basi wewe unachotakiwa ni kubweteka tu?!!:A S 13: , haya ni mawazo ya mtu aliyekata tamaa, kwamba yeye ndio basi tena hawezi kufanya lolote. chukulia mfano mdogo tu wa Marathon, mshindani wako akikutangulia utakaa chini na kuahirisha mbio au utajitahidi kwa bidii zako zote ili umshinde. kuna Nchi nyingi tu duniani ambazo zilikuwa maskini , lakini ukizitazama kwa sasa ziko mstari wa mbele.
 
Umenikumbusha kitu, kupitisha bakuli huku na huko ndiyo mtindo wa uswahilini kutembelea watu maarufu na kupiga huu mwingi kuwalainisha kisha anaondoka na kibaba cha kupitishia siku kwa mswahili inatosha mradi maisha yanakwenda.

Mafunzo makubwa ni haya yafuatayo:

1) Akili ni rasilimali kubwa inayoshinda rasilimali zote, kushinda madini, mbuga za wanyama, misitu, samaki, ardhi ya kilimo, uwingi wa watu.

2) Uongozi mzuri ni ule wa matendo siyo hadithi na ngonjera

3) Kama kipimo cha uongozi ni kufanya vitu vionekanavyo basi Tanzania hatujabahatika bado

4) Upole wa Watanzania huenda ni ishara ya ujinga kuliko kuwa ni ustaarabu
 
Mawazo ya kizamani haya , kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba mtu akikutangulia basi wewe unachotakiwa ni kubweteka tu?!!:A S 13: , haya ni mawazo ya mtu aliyekata tamaa, kwamba yeye ndio basi tena hawezi kufanya lolote. chukulia mfano mdogo tu wa Marathon, mshindani wako akikutangulia utakaa chini na kuahirisha mbio au utajitahidi kwa bidii zako zote ili umshinde. kuna Nchi nyingi tu duniani ambazo zilikuwa maskini , lakini ukizitazama kwa sasa ziko mstari wa mbele.

Katika hoja yangu nimezungumzia sula la utamaduni wa kusoma na kujisome pengine niende mbali na la ufahamu pia ikiwa umesoma sentensi ya kwanza ya hoja yangu ukakurupuka na kutoa comment mgando hilo ndio tatizo kubwa tulionalo sio wewe tu hata mimi na yule na huyu including viongozi wake hebu check hii ipo kwenye comment yangu nita e quote na kuibold na kuiwekea rangi uione vizuri
Wakenya kama wananchi ni watu wenye kujituma na wasiobweteka

Tuache kulalama tupige kazi tumia muda wako wa lunch kupost comments jf piga kazi ili mwisho wasiku viongozi wajisute kuwa wananchi wao ni wachapa kazi na wao inawabidi wachape kazi!

Ni kweli kuna nchi nyingi zilikuwa masikini lakini wananchi wake wanauzalendo hawatumii muda wa kuhudumia taifa kuselebuka kwenye mitandao ya kijamii! wanachapa kazi kama kazi masaa 8 basi hayo masaa 8 ni ya kufanya kazi! Angalia nchi zinazotuzunguka na hulka ya watu wake husika kisha nenda kwa viongozi wao ndio utaelewa nini nazungumza. Wananchi wenye kujua majukumu yao kama wazalishaji wakuu na watunzaji wa rasilimali za nchi wakitambua jukumu hilo basi bila shaka nchi itasonga mbele lakini sio nchi ya watu kung'oa hata mifuniko ya mifereji ya maji taka kwenda kuganga njaa ya siku moja. Ni lazima tujitume ili kuleta tija.
 
Kuwa na flyover si kipimo cha maendeleo, fungukeni kidogo. Kwa kuwa Paris haina majumba marefu kama Dubai haina maana haijaendelea.

Unataka kusema kuwa tanzania tumeendelea kuliko kenya? Au unamaanisha nini?
Mi nafikir wakenya wametuacha mbali hizo barabara ni kiashiria kimojawapo.
 
Mafunzo makubwa ni haya yafuatayo:

1) Akili ni rasilimali kubwa inayoshinda rasilimali zote, kushinda madini, mbuga za wanyama, misitu, samaki, ardhi ya kilimo, uwingi wa watu.

2) Uongozi mzuri ni ule wa matendo siyo hadithi na ngonjera

3) Kama kipimo cha uongozi ni kufanya vitu vionekanavyo basi Tanzania hatujabahatika bado

4) Upole wa Watanzania huenda ni ishara ya ujinga kuliko kuwa ni ustaarabu

Samahani mkuu hapo kwenye red mimi natofautiana na wewe nina amini kuwa tunao viongozi wenye akili ambayo hushinda rasilimali zote na sisi sio wapole ni watu wajinga na Mwalimu kwa kulijua hilo alitaka kupambana na ujinga. Sisi ni watu wa vijiweni wenzetu wanapiga mzigo we ona mimi na wewe tupo kijiweni sasa hivi tunapiga story wenzetu leo kutwa nzima wamepiga mzigo na wanajua kwa kuwa taifa lao walimpiga adui mjinga kisawasawa na akifanya mchezo atafutwa kazi maana wapo kama yeye hawana job basi ndio kabisa hawezi hata kupoteza sekunde kufanya yale yasiyo natija nae.

Nadhani unaelewa. Tatizo tulilonalo ni sisi tunaotawaliwa na hii ndio reflection kwa viongozi wetu Mungu hakosei kusema atawapatia viongozi wanaofanana na nyinyi.
 
Unataka kusema kuwa tanzania tumeendelea kuliko kenya? Au unamaanisha nini?
Mi nafikir wakenya wametuacha mbali hizo barabara ni kiashiria kimojawapo.

Kiashiria cha pili ni ukiwa na milioni moja ya kenya ni sawa na mwenye milioni 18 ya tanzania pesa yao ipo juu kama kichwa cha twiga na tukae chonjo uganda wanatupita na sijui kama tutawapata.
 
Mkuu niliwahi kusikia kuwa Kenya ndo wanasifika duniani kwa uuzaji wa Tanzanite! Sisi ni mabomu na kiongozi wetu ni bomu. Nahisi jamaa ana kichwa cha dafu! Natamani watu wa pwani tuwapige BAN kwenye kiti cha urais kwa miaka kama 20 hivi.

Mkubwa mswahili si mtu kumpa nchi akaongoza. wao ni uyakhe tuuuu. kenya unafikiri kwa nini hawakubali wadigo na watu wa mijikenda kuongoza nchi. Madafu yanadumaza akili. Nisiseme mengi manake ntaitwa mdini.
 
Kuwa na flyover si kipimo cha maendeleo, fungukeni kidogo. Kwa kuwa Paris haina majumba marefu kama Dubai haina maana haijaendelea.

We hujui hata unaloliongea,moja ya sign ya maendeleo ni advancement of infrastructure,so mpaka hapo uneonyesha huna kitu kichwani!
Pili we unalinganisha quality ya majengo ya paris hata kama sio marefu kama ya dubai na haya ya tanzania yanayodondoka yenyewe?! Rudi kajipange upya
 
Umesahau jambo moja, anashona viatu leo kesho ana grocery anatumia kanuni muhimu sana ya biashara inaitwa "Saving" kisha anafuata kanuni ya pili "Re invest" anapata kitu inaitwa "Expansion". Ila kwasababu wa machungwa anatumia kanuni ya "produce then eat" anabaki na "Vicious Circle of Ngoma". Si umeona mshikaji kila siku sherehe!! Sasa kama mavuno yooote yanaishia kwenye kumnema mwali, lini utapata uwezo wa kujenga nyumba ya bati? Sembuse kigae, thubutuuu!!!!
Atauza machungwa hata miaka 50 kihalali kabisa, lakini hawezi leo kuja kushona viatu, kesho ana grocery, keshokutwa bar. Ukichunguza utakuta katika mali ya huyo asiye wa pwani 99% ni haramu tupu.

Nani asiyejuwa hilo?
 
Tangu lini mswahili alipenda maendeleo. Mtu wa pwani anaweza kufanya biashara ya machungwa kwa miaka hata ishirini. Anachohitaji yeye ni faida itakayomwezesha kupata kibaba cha unga na mboga bila kusahau senti kidogo ya kununua kahawa kijiweni wakati wa kucheza bao. Rais wetu ni mtu wa pwani kwa hiyo sishangai kabisa.

Mkuu umesahau na hili: kuongeza kibinti kigori ktk list ya wake zake....
 
Mnafikiri kujenga fly over ni sawa na kujenga ukuta wa nyumba? Kwa miundo mbinu yetu na ujenzi holela hizo ngumu sana kujenga maana fly over haitakiwi ipite juu ya nyumba za watu, na inatakiwa inyanyuke kwa slope ndogo kuanzia mbali. Mtakubali kuhama mlipwe fidia? Au mtaanza maandamano ? Kipawa tu kupanua airport pale ilikuwa kasheshe watu kuondoka.

Mkuu;
Kwani ulimsaidia JK kuzitaja ahadi hizo? Si amekulia hapa jijini na alitakiwa atoe hali halisi kuliko kuahidi hewa? Ina maana wewe na JK wewe ndiye ulifaa kuwa rais maana umeyaona ambayo JK hadi sasa hajayatia machoni kabisaaa....! Pole na rais wako huyo......kumbe 'nazi'!
 
Back
Top Bottom