Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,639
- 29,512
Wadau,
Jana nilipita pale Tazara kuelekea maeneo ya Uwanja wa ndege nikitokea Mjini. Kufika karibu na traffic lights za Tazara nikaona Bango la Ujenzi ambalo linaonyesha Picha ya jinsi Fly Over ya Tazara itakavyokua. Nililiangalia hilo Bango nikaona picha imegeuzwa, yaani ukitaka uielewe hiyo picha inabidi na wewe upinde pia. Wewe unaetokea Mjini kama ndio unaiangalia ile picha kama ramani yako basi utajikuta upande wako uliko wewe pengine ndio iko picha inayotokea Ubungo.
Bahati Mbaya wakati wa kurudi nikiwa natokea Airport napo nikakutana na Bango pale pembeni ya Tazara. Nalo ukiliangalia unaona limepinda. Yaani picha iliyoko pale kwenye Bango inaonyesha barabara ya kwenda kulia ambako ni Uwanja wa taifa tuseme, kwenye picha ndio imeonyeshwa ya kwenda Mjini. Ile ya kunyoosha ukitokea vingunguti ambayo ndio ya kwenda mjini, katika picha imeonyeshwa kama ya kwenda Ubungo, ili uilewe inabidi na wewe ujipinde,
Hata ukiwa unatoka Ubungo/Tabata ukafika pale tazara basi ile picha ya kwenye bango lazima itakupoteza tu.Maana imeonyesha upande wa Airport ndio kulipo Mjini.
Nimeshuhudia watu wakipindisha vichwa ili kuipata hasa ile view ya pale ikoje kitu ambacho ni hatari. Nilidhani kwamba wangeweka picha tofauti kulingana na mtu anatokea upande upi ili kwa atakaekua akiangalia lile bango basi apate picha halisi pale patakuaje akitokea upande aliopo, badala ya kuweka picha moja tu kwa pande zote nne ambazo zinamchanganya mpita njia.